Kauli za rais ni kuwadhalilisha waliopata mimba za utotoni, tusijadili mimba bali watia mimba

fakhbros

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
329
1,000
Naamini mtazamo wa raisi Magufuli haiwezi kuitwa sheria ya nchi

Naamini kama itatokea mtoto wa hakimu au advocate akapata ujauzito na mwalimu mkuu akawa na kiherehere cha kumfukuza shule hiyo itakuwa imekula kwake sababu mtu kupata mimba sio kosa la kikatiba

Kusema ukipata mimba umenajisi KATIBA ya nchi

Naamini kabla ya Magufuli wapo waliopata pata mimba shuleni kwa kupewa na walimu wao au ndugu zao au wanafunzi wenzao bado walisoma nakuhitimu masomo,

Kauli za rais ni kuwadhalilisha waliopata mimba za utotoni

Kusema serikali yake haiwezi kusomesha wazazi wakati vyuoni na kwenye corter alizozijenga watu wanawapenzi wao humo na serikali inatoa pesa za kuwasomesha

Kama kauli ya Magufuli ilikusudia kwa watoto wa form four hapo tunaweza kukaa na kutafakari matukio kulingana na uzoefu

Tusijadili mimba Bali tujadili na watia mimba
Mara nyingi waathirika ni watoto wakike lakini wakiume wao hubaki salama baada yakutokuwepo ushahidi sahihi juu ya muhusika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom