gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,045
Baada ya Tundu Lissu kuipinga ile ripoti ya pili ya madini maarufu ripoti ya makinikia ya Prof Osoro na kuiita uchafu wa kitaaluma, Rais wa Tanzania mh John Magufuli alinukuliwa na vyombo vya habari akitamka maneno ambayo aliona kuna mtu anakwamisha juhudi zake za kupambania rasilimali za nchi
Mh Rais Magufuli alitamka maneno haya "hatuwezi kuwa vitani halafu askari aliye mbele ageuke na kuanza kushambulia wenzake, huyo hatumwachi salama, hawezi kitugeuka tukamwacha" haya ni maneno ya hatari sana kwa Tanzania ijayo yenye umoja wa kitaifa.
Kuna clip inasambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoaminika ni ya Naibu Waziri wa Tamisemi Mwita Waitara naona naye karejea maneno yenye kufanana sana na ya Rais Magufuli
Waitara anasema tuko kwenye vita ya kiuchumi anapotokea mtu anataka kutukwamisha lazima tumuwahi
Anasema kuna mtu anazurura huko nje kukwamisha juhudi za rais Magufuli, hivyo dawa yake ni kumtanguliza
Anasema tumepanda kwenye mtumbwi ambapo mmoja ameanza kuutoboa ili tuzama, anasema mtu huyo dawa yake ni kumtanguliza ndani maji
Hizi kauli za hawa viongozi ni kauli za hatari sana japo watu wanaweza kuona ni kauli zisizo na athari zozote kitaifa kwa wakati huu
Sent using Jamii Forums mobile app