Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa wa ajabu sana. Maana ukilinganisha na chaguzi zilizopita mwaka huu ni vituko na mambo ya ajabu sana.
Okiondoa uchaguzi wa mwaka 2015 miaka ya nyuma wapinzani walikuwa na hoja. Na mikutano yao ilikuwa na hamasa. Nakumbuka mwaka 2010 alikuwa akisimama Dk Slaa unaona uwanja mzima unasisimka. Maana mbali na kuibua madudu ya ufisadi lakini alikuwa anatoa nondo za maana juu ya namna gani atalifanyia taifa letu kama angelishinda.
Mwaka huu ni dalili kuwa CHADEMA hawakuwa na utayari wa kuja kupambana na Ccm ili kuchukua dola.
Mgombea wa CHADEMA anatoa hoja za ajabu sana kiasi kwamba anatia aibu. Mfano anadiliki kusema eti sababu Tanzania ni nchi ya kitropiki basi mradi wa JNHP hauna tija na kuwa hautakuwa na ufanisi,sababu tu mvua sio nyingi. Hivi hii inaingia akilini! Yaani anasema kuwa bora tungeendelea kujenga uzalishaji umeme wa gas pale Kinyerezi. Hivi hajui Kinyerezi phase 1& 2 ni kama MW 200 tu. Ujenzi wake umechukua muda mrefu.
Lakini JNHPP inajengwa kwa miaka mitatu na itapokamilika mwakani ni Mw 2100 zitazalishwa kwa mkupuo. Na hoja anazotoa kuwa umeme wa gas una gharama kidogo kuliko wa maji ni ukakasi na zinamuondolea sifa za kuwa kiongozi.
Mimi binafsi nilitarajia ampongeze JPM kwa kujenga mradi kama ule kwa pesa za ndani kuliko kuleta habari kama hizi ambazo zinashangza sana. Ila mimi siwezi kushangaa maana huu mradi hata mabeberu walikuwa wanaupinga na mgombea wa Chadema anajinasibu kuwa yupo karibu na Mabeberu
Je, kwa hoja kama hizi zisizo na kichwa wala miguu CHADEMA mlistahili kuwa na mgombea kama huyu? Kwanini msingeziua tu na kutafuta madiwani na wabunge kama hamna mgombea!