Katiba yetu inampa Rais mamlaka makubwa sana nchi hii. Rais ni kama Mungu kwa mujibu wa katiba yetu.
Mawaziri wanatwezwa lkn hawana cha kufanya. Wakijuzulu "mungu" anaweza kutafsiri hatua hii kama dharau na kuamua kuwashughulikia. Wanalazimika kuipokea kauli ya "mungu mtu" kwa mikono miwili.
Rais Magufuli aliwaita mawaziri Dr. Philip Mpango na Prof. Kabudi WAPUMBAVU mbele ya hadhara. Wakapokea kauli hii kwa mikono miwili. Sote tukabakia tumeduwaa. Ni kwasababu hawakuwa na la kufanya mawaziri hawa. Walimwogopa "mungu" na malaika wake
Rais Samia ametamka hadharani kwamba uamuzi wa Prof. Mkenda kuzuia sukari toka nje ni NONSENSE. Sote tumebaki tumepigwa na butwaa. Hana la kufanya Prof. huyu. Akirogwa kujiuzulu "Mungu" ama malaika wake watamshughulikia.
Tuiangalie upya Katiba yetu inayomjenga mtu kuwa "Mungu".