Kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania

Anfaal

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
1,154
0
- Mkuu Aanfal, heshima yako sana Malecela sio malaika isipokuwa haters wake hawana facts za kutosha kuthibitisha mapungufu yake kiuongozi, sasa unashauri nini mkuu kwamba kwa vile hakuna facts na anaonekana kama Malaika, basi ahukumiwe tu kusulubiwa maana bila hivyo itaonekana kama yeye ni malaika, is that why we here at JF?

- Kwanini mkuu na wewe usijitume ukaleta facts za mapungufu yake, kwani ni wapi nimemlazimisha mtu hapa kuamini uongo wangu mimi ninaweka facts tu, Malecela aliposema kwamba ufisadi ni hoja ya CCM sio ya Dr. Slaa, nilisema wazi kwamba he is wrong yeye na Mama kilango wamekosea kwa sababu facts zilikuwa wazi, otherwise sikulazimishi wewe wala member yoyote hapa kuamini uongo wangu wa kumtetea anybody licha ya Malecela tu kama ninavyofanya siku zote.- Ni vizuri sana tukawa wakweli maana hii forums inasomwa na wananchi wengi sana, sasa tukiwapotosha itakuwa sio vyema kuweka historia iliyopinda, otherwise heshima zangu kwako kwa kuwa very fair!

Respect.

FMEs!
FMEs I like the way unavyoapproach mjadala na unavyojua kusimamia ishu. Binafsi huwa naepuka kujadili mambo ya miongo mingi iliyopita kama hayawezi kuwa intergrated kwa hali ya sasa. Sina sababu ya kuanza kumchimba Mzee Malecela.
Ukizipia hoja za watu wengi woote inaonekana wamesikia kupitia vyombo vya habari au hata simulizi ambavyo vyombo hivyo vimekuwa vikitumika kama source zetu mbalimbali ingawa wakati fulani NAVYO HUTELEZA.
Hoja yangu sasa; wewe mwenyewe umetoa ushahidi kupita kwa jamaa wa karibu wa Melecela na wale waliokuwa wanafanyakazi chini ya shirika ambalo Malecela alikuwa akilisimamia (Tafsiri nzuri mgongano wa maslahi). Unadhani ushahidi wa maneno yako kutoka kwa kundi la watu unajitosheleza kukuamini? Nadhani hukuwa na haja ya kutoa list ndefu ya watu walikuwa chini ya Malecela. Kimsingi hoja yako ya kudai ushahidi kwa waliomtuhum ndiyo ilikuwa imara otherwise objectivity inakuwa impaired.
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665

- Sasa naona tumerudi kule kule kwenye logics badala ya facts, ule ule mchezo wako wa kurudia facts zangu kutengenza debate on logic zake, samahani sana ni waste of people's time, halafu naona unahangaika sana kubadili badili maandiko vipi kunani huko?

- Saa ya kulala sasa, na ninaomba kupumzika na huu mjadala maana hauna mbele wala nyuma ila ni hating tu as usual.
Respect.

FMEs!
 
Bongolander

JF-Expert Member
Jul 10, 2007
5,068
2,000
Katika kutafakari hali ya siaza za Tanzania nimekumbuka baadhi ya kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania. Kauli hizi zinawaelezaje wahusika? Na ili kuweka mambo sawa hebu tujaze mazingira na mwaka wa kauli hizi.

1. Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe- Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha wakati wa kikao cha bunge la bajeti mwaka 1989

2. Hata ikibidi watanzania kula nyasi ndege ya rais itanunuliwa - Mramba akiwa waziri wa fedha, mwaka.......

3. Watanzania wana wivu wa kike- Benjamin Mkapa akiwa Rais, mwaka.....

4. Watanzania wavivu wa kufikiri- Rais Benjamin Mkapa akiwa Rais, Mwaka..

5. Kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, Rais Kikwete, Mwaka...

6. Atakayegombea na Kikwete atakufa ghafla, Sheikh Yahaya Hussein, akiwa anapiga ramli Channel Ten, Mwaka.....

Baada ya kuziweka kumbukumbu vizuri tujiulize, hivi kauli zao hao wahusika zinawaeleza vipi?. Kwa maoni yangu kauli 1 na 2 zinawaeleza mawaziri wa fedha kama watu wasiokuwa na huruma. Kauli zingine zinawaelezaje wengine?

Ilinisikitisha sana kwa kuwa ukweli ni kwamba tuliishia kubeba mizigo yao huku tukiendelea kubeba ya kwetu. Lakini ni ukweli unaouma, mpaka sasa watu wanaenjoy jasho letu kwa kutumia hela za walipa kodi kama wanavyopenda. And it seems that it will be so for a very long period of time.
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,193
2,000
"Nimepokea maombi ya wapiga kura wengi kutoka ktk majimbo ya uchaguzi ya Kinondoni,Kigoma Mjini,Kigoma kaskazini,Geita na Kahama wakiniomba nikagombee"-Mbunge Zitto Zubeir Kabwe!
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0
Ilinisikitisha sana kwa kuwa ukweli ni kwamba tuliishia kubeba mizigo yao huku tukiendelea kubeba ya kwetu. Lakini ni ukweli unaouma, mpaka sasa watu wanaenjoy jasho letu kwa kutumia hela za walipa kodi kama wanavyopenda. And it seems that it will be so for a very long period of time.

- Ndio maana nimeamua kuwahi ubwabwa Soho kwenye St.Patric Parade ni bora zaidi! Bwa! ha! ha! ha! maana tukianza kufuatilia walio enjoy hela zetu za kodi bila ruhusa yetu wananchi, tutafukua wengi sana maana sijawahi kusikia bajeti ya wakimbizi wa kisiasa toka nchi zingine, kwa hiyo ina maana majambazi wa CCM walikuwa wakichota hela zetu za kodi bila ruhusa na kuyatunza yale makimbizi na kuyasomesha matoto yao, I mean talking about walio-enjoy jasho letu yaani weee acha tu!

- Mkuu Bongolander inauma sana na mizigo tuliyowahi kubeba hili taifa!
waambie hawa!

FMEs!
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0
"Nimepokea maombi ya wapiga kura wengi kutoka ktk majimbo ya uchaguzi ya Kinondoni,Kigoma Mjini,Kigoma kaskazini,Geita na Kahama wakiniomba nikagombee"-Mbunge Zitto Zubeir Kabwe!

- Mkuu wangu Malafayale siku hizi unanifurahisha sana jinsi unavyoakta ishus kiroho mbaya, saafi sana!

FMEs!
 
Nurujamii

JF-Expert Member
Jun 14, 2007
414
195
''Mimi sijawahi kuwashambulia mafisadi lakini inashangaza nimekuta jimboni mwangu wamesambaza mamilioni" - Victor Mwambalaswa (Mb-Lupa CCM), December, 2009.

Hii nimeipenda! Lol; mbavu zangu jamani! Asante Gabu!
 
MotoYaMbongo

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,065
2,000
Mkuu nyingine ya naibu waziri wa elimu aliowaambia wanafunzi wa ualimu wa chuo kimoja kusini kuwa "anayeona ualimu haulipi akasomee kozi ingine" kisa, wamemuuliza swali kuhusu maslahi ya walimu. Huyu ni Mwatumu Mahiza kama sijakosea jina. Ingine alisema Hawa ghasia mwaka sikumbuki kuwa "walimu mnataka mishahara mikubwa kwa kazi gani kubwa mnayofanya?".
 
Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,971
0
Katika kutafakari hali ya siaza za Tanzania nimekumbuka baadhi ya kauli za kisiasa zilizowahi kuwaudhi sana Watanzania. Kauli hizi zinawaelezaje wahusika? Na ili kuweka mambo sawa hebu tujaze mazingira na mwaka wa kauli hizi.

1. Kila mtu ataubeba msalaba wake mwenyewe- Cleopa Msuya akiwa waziri wa fedha wakati wa kikao cha bunge la bajeti mwaka 1989

2. Hata ikibidi watanzania kula nyasi ndege ya rais itanunuliwa - Mramba akiwa waziri wa fedha, mwaka.......

3. Watanzania wana wivu wa kike- Benjamin Mkapa akiwa Rais, mwaka.....

4. Watanzania wavivu wa kufikiri- Rais Benjamin Mkapa akiwa Rais, Mwaka..

5. Kelele za mpita njia hazimnyimi mwenye nyumba usingizi, Rais Kikwete, Mwaka...

6. Atakayegombea na Kikwete atakufa ghafla, Sheikh Yahaya Hussein, akiwa anapiga ramli Channel Ten, Mwaka.....

Baada ya kuziweka kumbukumbu vizuri tujiulize, hivi kauli zao hao wahusika zinawaeleza vipi?. Kwa maoni yangu kauli 1 na 2 zinawaeleza mawaziri wa fedha kama watu wasiokuwa na huruma. Kauli zingine zinawaelezaje wengine?

Kauli namba 3 inamaanisha kuwa Mkapa hawaheshimu wanawake hata mkewe...Mfumo dume umemharibu.
 
Majasho

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
374
250
sijui kama kuna mtu ameshaandika hii, lakini i think iliyo waudhi wengi ikiwemo mimi ni Mh,CHENGE

kwenye tuhuma ya RADA ya MABILLION...alisema

'HIVYO NI VIJISENTI TU'
 
Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
0
[I said:
''Mimi sijawahi kuwashambulia mafisadi lakini inashangaza nimekuta jimboni mwangu wamesambaza mamilioni" - Victor Mwambalaswa (Mb-Lupa CCM), December, 2009.[/I]
Kati ya wabunge waliochoka au tuseme walioingia kwenye siasa kwa njaa zao na sio kwa maslahi ya uwakilishi wa wananchi wa jimbo lake ni huyu aliyetoa kauli hii.
Kwa tafsiri rahisi ni kwamba kwa kuogopa nguvu za mafisadi hawezi kusema chochote kwa maslahi ya wananchi kwa kuwa ataharibu future ya ubunge wake, kiasi anatia kinyaa. Nadhani huyu kesha jihukumu tayari wananchi watakuwa wana hitimisha tu mwezi wa kumi.
Mungu wajalie hekima na upendo kwa nchi yao wananchi wa Lupa.....Ameen!!
 
Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
0
"Nimepokea maombi ya wapiga kura wengi kutoka ktk majimbo ya uchaguzi ya Kinondoni,Kigoma Mjini,Kigoma kaskazini,Geita na Kahama wakiniomba nikagombee"-Mbunge Zitto Zubeir Kabwe!

Hii nadhani inachekesha, aliitoa akiwa wapi na lini? watanzania walikasirika?
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,193
2,000
Hii nadhani inachekesha, aliitoa akiwa wapi na lini? watanzania walikasirika?

Kauli hii kaitoa wiki iliyopita na kanukuriwa na vyombo vingi sana vya habari bila Mbunge Zitto kukanusha,na akaongeza zaidi kuwa kaituma timu yake ya wataalam wamletee habari ni wapi akagombee kati ya majimbo hayo 5!

Ni habari iliyotukera wengi maana ina leta maswali mengi zaidi ya majibu na kwa kweli ingekuwa nchi zilizoendelea matamshi haya ya Mbunge Zitto ndiyo ingekua kabuli lake kisiasa!

Kwanza,Je ina maana Zitto kamaliza kero zote za wana Kigoma kama mwakilishi wao na sasa anasukumwa zaidi kupeleka maendeleo kama aliyoyaleta Kigoma kwenye majimbo mengine aliyoyatambua yeye kuwa wana wawakilishi hafifu bungeni?

Pili,wapiga kura wa watz wapo tayari kumchagua Mbunge kwa sababu tu mgombea Ubunge huyo ana ujuzi zaidi wa raslimali zilizopo kwenye jimbo hilo kama Zitto aliposema kwa nini anaombwa kugombea Ubunge Kahama na Geita?

Tatu,je ni kweli anakabwa na msongo wa sifa za"Mbunge wa Taifa"hata akawa ana hisia kuwa anaweza kuwa Mbunge wa Jimbo lolote lile nchini TZ bila hata ya kujali kama kachangia nini kwenye jimbo hilo kabla ya kuomba nafasi ya Ubunge?

Mwisho,je ina maana kuwa na elimu kuhusu mikataba ya madini ndiyo sifa kubwa ya mtu husika aupate Ubunge?Je kuwepo kwake Bungeni Mheshimiwa Zitto kaisha wahi ishawishi serikali iweke mazingira mazuri ili pesa zipatikanazo kwenye madini ziwanufaishe watu wa Kahama/Geita?Au anasubiri awe Mbunge ndiyo aanze ushawishi?

Kule Kigoma wana mali asili zao,kama Chumvi,mawese na uvuvi,wakazi wengi wa kule wanafaidika lolote na malia asili hizo?Iweje asiwafanye wana Kigoma wafaidike na mali asili yao alipokuwa mbunge wa huko lkn akawafanye wana Kahama wafaidikie akiwa Mbunge wao?Mbona zipo Wilaya nyingi sana zenye madini ambazo hafikirii kwenda kugombea?Kyela wana makaa ya mawe,Arusa kuna Tanzanite,mbona haendi huko?

Kama sifa ya kuchaguliwa Kahama/Geita ni elimu ya mikataba ya madini,je ni sifa gani itakayomfanya achaguliwe kule Kinondoni kusikokuwa na madini?au ndiyo hii sifa ya kuwa"Mbunge wa Taifa"?

Nashauri akagombee kwenye jimbo walilomchagua kuwa Mbunge,maana kazi yake ya ushawishi huko itakuwa ni rahisi sana;watapima tu alichofanya kwa miaka hii 5 alipopewa Ubunge.
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,862
2,000
- Mkuu heshima yako sana, wewe unakubaliana na Kichuguu na mimi ninasimamia hoja yangu kwamba hii kauli originally ilidaiwa kwamba aliisema kwenye TRC Club iliyoko karibu na Central Police, ambako ni kweli siku hiyo Malecela alikuwepo ilikuwa Jumamosi kwenye tafrija ya Relwe, na bado ninakataa kwamba hakuisema hiyo kauli, isipokuwa ilitengenezwa na maadui zake kisiasa waliomtumia msaidizi wake wa karibu sana Marehemu Gisley Mapunda.

- Huu mchezo wa kumkosesha raha kisiasa Malecela haukuishia hapo, infact after that kuna "watu" walitumwa kwenda kupitia kila kona kijijini alikozaliwa kuona kama kuna anything negative inayoweza kutumiwa kumkandamiza zaidi wananchi wengi pale kijijini walimfahamisha mwenyewe juu ya watu hawa wageni pale kijijini, na baadaye walihamia mjini Dodoma, kwa vile hakukuwepo anything serious ndio zakiaanza kazi za njama za kumng'oa ubunge kwa kumtumia Marehemu Mazengo.

- Sasa ninaomba nikufahamishe hivi kwamba ninachosimamia hapa ni a principle na sio Malecela as a human, kwa sababu najua kwamba ana mapungufu mengi sana kama mimi na wewe, lakini siku zote nina mkataba na ukweli regardless unamhusu nani ninasimamia ukweli ninaoujua, na mkuu haya maswali niliwahi kumuuuliza mwenyewe Malecela, licha ya wasaidizi wake hasa Mzee Misano, aliyekuwa Manager wake wa uchaguzi na wengineo kama ndugu yake Mzee Lusinde, haiwezekani kwmba Malecela ana nguvu za ajabu kiasi cha kuwafanya hawa watu wote wazima waseme uongo on his behalf.

- Katika maisha yake ya siasa Malecela siku zote alikuwa na haters tena wa ajabu sana, ambao wako willing kusema anything ku-support the big conspiracy ambayo hawakuijua kuwa ilikuwa inaongozwa na mtu mmoja tu kwa makusudi yake binafsi, sasa ndio maana siwezi kushangazwa na ushuhuuda wako kwamba Malecela alisema, siku inayodaiwa kwamba alisema, wakati wote wa chakula alikuwa karibu sana na Marehemu Mama Kirunda, aliyekuwa Manager wa Cattering wa TRC, Tom Mmari aliyekuwa big Administrator wa TRC, Marehemu Mzee Kitenge another TRC big then, na Marehemu Mzee Kibwana another TRC big then, pia alikuwepo karibu naye alikuwa Marehemu Gisley Mapunda aliyekua personal Assistsant wake, na Waandishi wengi wa habari akiwemo Bwana Balinagwe. Na ninaomba nikuhakikishie kwamba it is a matter of time kabla vitabu vya majibu kuhusu all accusations against Malecela havijaanza kuchapishwa na ndipo wananchi wa taifa hili watakapoamua ukweli na uongo ulipo. na hivi vitabu vitawaelezea kwa urefu wale waandishi wote wa habari waliotumika na hizo conspiracy kwa kuweka wazi record zao za uandishi ili kuonyesha with evidence kwamba kwa nini kwenye Malecela walikua wanaandika bila kujali taratibu za uandishi.

- Kwenye hizi conspiracy against Malecela mkuu ninaongea na utafiiti wala sio majungu kwa hiyo, rest assured kwamba ninaheshimu sana Demokrasia na hasa Dual Process, ambapo kila upande unapewa nafasi ku-represent it case na wananchi kuamua conclusion.

Respect.

FMEs!

FMES; nadhani uachane najitihada zako za kuandika upya history kwa kudai kuwa jambo hili halikutokea. Nadhani la maana ni kutambua kuwa ni jambo lililotokea zamani sana ambalo haliwasaidii watanzania kupata ugali wao leo, kwa hiyo halina haja kuendelea kuongelewa; badala yake watu waangalie mambo yenye umuhimu zaidi katika kipindi hiki tulicho nacho.

Unakosea sana kutoa madai ya kuwa maneno hayo yalitungwa na maadui wa kisiasa dhidi ya Waziri Malecelea aliyekuwa kwenye serikali ya Nyerere tena chini ya mfumo wa Chama kimoja. Utakuwa unawapotosha sana watoto waliozaliwa baada ya mwaka 1985 ukiwaambia kuwa wakati ule maadui wa kisiasa walikuwa wanaweza kumpakazia jambo mwanasiasa na kiongozi wa serikali, halafu eti jambo hilo la kupakaziwa likatangazwa katika vyombo vya habari ambavyo vilijkuwa vinamilikiwa na CHAMA na serikali. Naona unaleta masihara wewe, kuna watu wa heshima leo hii walijikolea kwenye suruali mbele ya Nyerere halafu etu kuwa na mkurugenzi wa RTD au Mhariri wa gaezti aeendike upuuzi aendelee kubaki madarakani. Unless unataka kusema kuwa Nyerere naye alikuwa ni mmoja wa hao conspirators; jambo ambalo litakuwa gumu zaidi kuthibitisha kwa sababu hakuwa na haja ya kufanya hivyo kama kweli alikuwa ni adui wake wa kisiasa basi asiengempa uwaziri na labda angemweka kizuizini tu.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,858

Kichuguu umesema kweli,
Kauli ile kwa sasa haina madhara yeyote kwa mzee Malecela hivyo si hoja tena. Maana baada ya pale ameendelea kufanya mambo mengi makubwa makubwa na kati ya hayo yapo aliyofanya kwa mafanikio na yapo aliyokosea na ndio maana jina lake bado lina heshima kitaifa na kimataifa.
Tusipoteze muda mwingi kutaka kufuta kuwa hakutamka kauli ile au alipakaziwa na maadui zake (anbao kama walikuwepo hawakuwa na ubavu wa kuzusha jambo kama hilo)
 
Jayfour_King

JF-Expert Member
Nov 15, 2009
1,135
0
Kauli hii kaitoa wiki iliyopita na kanukuriwa na vyombo vingi sana vya habari bila Mbunge Zitto kukanusha,na akaongeza zaidi kuwa kaituma timu yake ya wataalam wamletee habari ni wapi akagombee kati ya majimbo hayo 5!

Ni habari iliyotukera wengi maana ina leta maswali mengi zaidi ya majibu na kwa kweli ingekuwa nchi zilizoendelea matamshi haya ya Mbunge Zitto ndiyo ingekua kabuli lake kisiasa!

Kwanza,Je ina maana Zitto kamaliza kero zote za wana Kigoma kama mwakilishi wao na sasa anasukumwa zaidi kupeleka maendeleo kama aliyoyaleta Kigoma kwenye majimbo mengine aliyoyatambua yeye kuwa wana wawakilishi hafifu bungeni?

Pili,wapiga kura wa watz wapo tayari kumchagua Mbunge kwa sababu tu mgombea Ubunge huyo ana ujuzi zaidi wa raslimali zilizopo kwenye jimbo hilo kama Zitto aliposema kwa nini anaombwa kugombea Ubunge Kahama na Geita?

Tatu,je ni kweli anakabwa na msongo wa sifa za"Mbunge wa Taifa"hata akawa ana hisia kuwa anaweza kuwa Mbunge wa Jimbo lolote lile nchini TZ bila hata ya kujali kama kachangia nini kwenye jimbo hilo kabla ya kuomba nafasi ya Ubunge?

Mwisho,je ina maana kuwa na elimu kuhusu mikataba ya madini ndiyo sifa kubwa ya mtu husika aupate Ubunge?Je kuwepo kwake Bungeni Mheshimiwa Zitto kaisha wahi ishawishi serikali iweke mazingira mazuri ili pesa zipatikanazo kwenye madini ziwanufaishe watu wa Kahama/Geita?Au anasubiri awe Mbunge ndiyo aanze ushawishi?

Kule Kigoma wana mali asili zao,kama Chumvi,mawese na uvuvi,wakazi wengi wa kule wanafaidika lolote na malia asili hizo?Iweje asiwafanye wana Kigoma wafaidike na mali asili yao alipokuwa mbunge wa huko lkn akawafanye wana Kahama wafaidikie akiwa Mbunge wao?Mbona zipo Wilaya nyingi sana zenye madini ambazo hafikirii kwenda kugombea?Kyela wana makaa ya mawe,Arusa kuna Tanzanite,mbona haendi huko?

Kama sifa ya kuchaguliwa Kahama/Geita ni elimu ya mikataba ya madini,je ni sifa gani itakayomfanya achaguliwe kule Kinondoni kusikokuwa na madini?au ndiyo hii sifa ya kuwa"Mbunge wa Taifa"?

Nashauri akagombee kwenye jimbo walilomchagua kuwa Mbunge,maana kazi yake ya ushawishi huko itakuwa ni rahisi sana;watapima tu alichofanya kwa miaka hii 5 alipopewa Ubunge.
Mawazo ni mazuri sana mkuu, lakini kama siasa zetu zingekuwa na nidhamu hiyo hapo nilipo mark red kwa mawazo yako wabunge wapya wangekuwa wanapatikana vipi? Binafsi sioni kama kauli ya Zitto kama ina ubaya wowote achilia mbali madhara hivyo napendekeza tuwe fair. Ni nchi hii hii tunakumbuka kwa umaarufu aliokuwa nao Mrema wakati huo aliweza kugombea jimbo la uchaguzi la TMK na kumshinda Cisco Mtiro pamoja na kufanyiwa kampeni na Mr Clean wa wakati huo akiwa rais wa nji na bado Mrema alishinda.

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, sioni ubaya wa kauli aliyotoa Kabwe hata kama ana matatizo mengine kwenye fani hii ya siasa lakini kwa hili naomba umsamehe bure!!
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0
FMES; nadhani uachane najitihada zako za kuandika upya history kwa kudai kuwa jambo hili halikutokea. Nadhani la maana ni kutambua kuwa ni jambo lililotokea zamani sana ambalo haliwasaidii watanzania kupata ugali wao leo, kwa hiyo halina haja kuendelea kuongelewa; badala yake watu waangalie mambo yenye umuhimu zaidi katika kipindi hiki tulicho nacho.

Unakosea sana kutoa madai ya kuwa maneno hayo yalitungwa na maadui wa kisiasa dhidi ya Waziri Malecelea aliyekuwa kwenye serikali ya Nyerere tena chini ya mfumo wa Chama kimoja. Utakuwa unawapotosha sana watoto waliozaliwa baada ya mwaka 1985 ukiwaambia kuwa wakati ule maadui wa kisiasa walikuwa wanaweza kumpakazia jambo mwanasiasa na kiongozi wa serikali, halafu eti jambo hilo la kupakaziwa likatangazwa katika vyombo vya habari ambavyo vilijkuwa vinamilikiwa na CHAMA na serikali. Naona unaleta masihara wewe, kuna watu wa heshima leo hii walijikolea kwenye suruali mbele ya Nyerere halafu etu kuwa na mkurugenzi wa RTD au Mhariri wa gaezti aeendike upuuzi aendelee kubaki madarakani. Unless unataka kusema kuwa Nyerere naye alikuwa ni mmoja wa hao conspirators; jambo ambalo litakuwa gumu zaidi kuthibitisha kwa sababu hakuwa na haja ya kufanya hivyo kama kweli alikuwa ni adui wake wa kisiasa basi asiengempa uwaziri na labda angemweka kizuizini tu.

- Mwalimu Kichuguu, sina muda wa kujadili logic utakapopata facts lete hapa tujadili, lakini otherwise sina muda wa kujadili hizi nonsense! umeleta uongo, sasa kubali badala ya kubadili badili the subject, kubali kwamba umeleta uongo!

- Sina muda wa kujadili uzuushi na majungu, pamoja na uongo wewe simply ni muongo huna facts za kuthibitisha kwamba Malecela alisema hayo maneno na alipoyasemea na aliyemsikia huwajui sasa nyamaza maana:-

!no facts, no research no right to accuse no right to speak!
, history ya kuandikwa na magazeti ya CCM my foot!

Kamanda FMES, hivi Mheshimiwa alikanusha wakati ule kuwa hakusema hayo maneno?
 
Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,665
0
Kamanda FMES, hivi Mheshimiwa alikanusha wakati ule kuwa hakusema hayo maneno?

- Chakaza Malecela sio mjinga, he knew who was behind the attacks, na aliwahi kuniambia hivi anaishukuru sana amani ya Tanzania, yeye alipokuwa balozi UN in the 60s alikuwa na wenziwe wengi kutoka Africa ambao waliporudi kwao wakawa ma-political stars, wakaishia kuwekwa jela na kufia huko, infact anasema siku moja aliwahi kutembela Guinea na kumkuta balozi mwenzake wa zamani akiwa jela ambako alienda kumuona, anasemaa to this day hasahau hali aliyomkuta nayo yule rafiki yake mpenzi sana walipokuwa UN, anasema ni yeye tu na Vernon Mwaaanga, aliyekwua balozi wa Zambia, ambaye mpaka sasa waziri huko ndio walioopona, I hope nimekusaidia sana kwamba kwa nini Malecela hakukanusha wala kupiga kelele, sasa mind you hakukanusha mengi sana sio hayo tu pekeyake.

- By the way na wewe vipi unazo facts za wapi alisema hayo maneno, na alimwambia nani? Je unao ukweli au na wewe unataka tujadili logic na facts za magazeti yaliyokuwa yakiongozwa na Mkurugezi wa propaganda wa chama bwana Sozigwa, yaani Daily News, Sunday News na Mzalendo?

- Eti na wewe unasema CCM wanayo magazeti ambayo once upon a time yalikuwa yakiandika ukweli tu, unatka na mimi niapnde hii treni ya 70%? Au na wewe unafikiri bado tuko zile enzi za kuhesabu visoda vya bia wanazokunywa wannchi kwenye mabar? na kutoruhusiwa kusema wala kuuliza?

Respect.

FMEs!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom