Kauli za Jussa juu ya uchaguzi wa Uzini ni hatari kwa umoja wa kitaifa!

Binafsi siwezi kutoa tamko kwani sijamsikia wala kupata maelezo yeyote kuhusiana na hili. Lakini hata kama ni kweli Jussa katamka hili, litakua si tukio la mwanzo kwa wanasiasa wa Tanzania. Tumeshuhudia uchaguzi mkuu wa 2010 Viongozi wa CHADEMA wakitamka matamshi mengi tu yanayoashiria UDINI! Lakini mimi naamini 'issue' hii ni ule msemo; "give dog a bad name and kill it". Na pia ni miongoni mwa mambo munayoyazua na kuyakuza nyinyi Watanganyika (CHADEMA) ili mutugawanye Wazanzibari na badala yake tusahau mapambano yetu ya kutaka kuileta Zanzibar iliyo HURU. Hamutupati tenaaaaaa. Zanzibar Daima, Am proud with happiest to be Zanzibari!
 
tutaangalia kwenye mtandao wao wa mzalendo kama hizi pumba aliongea, halafu mimi nashangaa wananchi wa ZNZ wanajaza wahindi tu kwenye serikali haahhaaaa yaani......

Si ndio hayo kwa hayo. Kwako muhindi ni binaadamu mwengine
 
Hakika huyu Jussa ni mtu mbaya sana.Sijui anapata faida gani kuwagawa watu kwa misingi ya udini.Hii ni laana na dhambi mbaya sana.Na naapa kwa maneno yake haya hii dhambi itamtafuna mpaka immalize.Huyu ni kaburu wa hali ya juu
 
Imetolewa na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa – Zanzibar.

TUMEJIFUNGIA na WAZEE na tumekaa tukanong'ona ! Kwanza Serikali ya Tanganyika walituletea sakata la Hamad Rashid, na watu wakalivamia. Ikawa mwezi na nusu Wazanzibari hatujadili tena kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Baadae likaja suala la kuongezwa kwa mipaka ya bahari kuu la Tibaijuka na Shamhuna. Akina Bilali, Samia Suluhu na wenziwao tutajuwana nao.

BAADA ya kuiweka mezani Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Pia kwa makusudi, wamelizusha suala la kufutwa kwa mitihani ya kidato cha nne. Tunalopaswa kufanya ni kuhakikisha Waziri wa Elimu wa Zanzibar, anatoa ripoti juu ya kufutwa kwa mitihani ya kidato cha nne, pamoja na kutueleza kwa kina mfumo wa mzima wa elimu duni uliopo Zanzibar.

Hivi sasa limezuka suala la uchaguzi mdogo wa Uzini na Chadema kuchukua nafasi ya pili baada ya kuwanunua wapiga kura mamluki.

Tujue kwamba, Tanganyika iliyojificha ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano, haitosita na haitolala mpaka tuifuate MILA yao ya kuijadili Katiba ya Muungano.

KWANZA bila ya kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Tukiyafuata waliyoyakusudia na wanayoyapanga, tutakuwa tumetoka nje ya kuidai HAKI yetu ya kimsingi ya kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. Hamad Rashid, Bilali, kufutwa kwa mitihani na uchaguzi wa Uzini, zote hizi ni mbinu, ujanja na fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Kamwe hatutaicheza ngoma yao!

Zamani ilikuwa ni UHAINI kujadili Muungano. Juzi tu, wajanja hawa hawa kwa kutaka kuiendeleza falsafa hiyo ya Unyerere, wamepitisha sheria Bungeni ya kumchukulia hatua yo yote atakaejadili lo lote ambalo liko nje ya hadudi rejea za rasimu ya Katiba. Kwa mantiki hiyo, yo yote atakaetoa NGUVU ya HOJA ya kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

KWANZA na/au Muungano wa Mkataba na kuukataa Muungano wa Katiba wakati wa mchakato wa Katiba utakapokuja, atachukuliwa hatua za kisheria kwa kufikishwa Mahakamani, ili wengine waogope kuendelea kuidai Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, na badala yake iendelezwe HOJA ya NGUVU na ya udikteta inayotakiwa ya kujadili Katiba iliyosimama juu ya misingi ya KIKOLONI inayopinga uwepo wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambayo ndio mbia mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hizo zinazodaiwa kuwa ni hati za Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zilijengwa juu ya taswira ya Muungano baina ya Uingereza na Ireland ya Kaskazini ya wakati ule, pale Ireland ya Kaskazini ilipokuwa
ni koloni la Uingereza.

Kudhihirisha njama za wajanja hawa, juzi tarehe 12 Februari 2012, Halmashauri Kuu ya CCM kwa makusudi, imeifanyia marekebisho Katiba ya CCM yenye lengo la kuwaangusha na kuwadhibiti – MASHUJAA wa MARIDHIANO yetu yaliyo HALALI Kikatiba, na badala yake, kuwabeba VIBARAKA ambao wameonesha wako tayari kuiuza Zanzibar na Wazanzibari kwa UTASHI wa UBINAFSI unaoongozwa na uroho na ulafi wa madaraka.

WAZANZIBARI po pote tulipo duniani TUMESHAAMKA na KUSIMAMA KIDETE kwa kuelewa kuwa, yote haya ni katika mbinu
chafu, hadaa, ghilba na fitina za kutuondoa kwenye lengo KUU la kuipigania na kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Tusikubali, na kwa hakika HATUTAKUBALI kuondolewa kwenye njia na lengo letu hilo HALALI la kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye hadhi yake kitaifa na kimataifa; maana sisi wananchi wa Zanzibar, tuna mamlaka na haki ya Kikatiba katika kuendesha nchi yetu kama Katiba ya Zanzibar ya 1984, Toleo la 2010, inavyoeleza kwenye Sura ya Pili: (a) "Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa
wananchi wenyewe".

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar KWANZA!
 
Mkuu propaganda zingine si nzuri na hazitatufikisha pazuri. we endelea tu utaona matokeo yake.

Hapa ni mahali pa hoja kama huna hoja kaa kimia siyo kutishana na ninahaki ya kusema na kutoa maoni yangu bila hofu huku nikisimamia ukweli sina ugomvi na jussa tena namuheshimu sana lakini kwa hili amekosea lazima tuseme kweli.
 
Wadau niliwaahidi kuleta clip ya maneno ya jussa. bahati mbaya nimeshindwa kuiupload bt bado najaribu
 
Jamani tarifa sahihi ni kuwa jusa amedanganya,ukweli ni kuwa raza ni rais wa jamatini ambako walikubaliana jamatini sehemu ya ibada ya washia walikubaliana kuwa lazima rais wa jamatini ashinde ili nao waungane ,moja mbili jusa naibu katibu
mkuu amesaliti a cuf kwa maslahi ya tasisi ya dini yake ya shia na sasa anapotosha uma rejeni makubaliano yake na rostam wote shia
 
Wadau niliwaahidi kuleta clip ya maneno ya jussa. bahati mbaya nimeshindwa kuiupload bt bado najaribu
kwani hiyo clip bado haijabandikwa mzalendo.net ? au wameona aibu kuubandika huu u.p.upu kama walivyoubandika fasta ule u.p.upu wa kumtukana samuel sita
 
Haya wadau evidence hii hapo chini - maneno ya jussa mwenyewe!!

[video=youtube_share;agep7E2bafk]http://youtu.be/agep7E2bafk[/video]
 
Jamani tarifa sahihi ni kuwa jusa amedanganya,ukweli ni kuwa raza ni rais wa jamatini ambako walikubaliana jamatini sehemu ya ibada ya washia walikubaliana kuwa lazima rais wa jamatini ashinde ili nao waungane ,moja mbili jusa naibu katibu
mkuu amesaliti a cuf kwa maslahi ya tasisi ya dini yake ya shia na sasa anapotosha uma rejeni makubaliano yake na rostam wote shia
 
..sasa mbona aliyeshinda siyo Mkristo au mwenye asili ya Tanganyika?

..I dont think Jussa can be that shallow. Ningefurahi sana kama ungetuletea hayo mahojiano na sisi tupate kumsikia.

Ni kweli alisema ndugu yangu. Inatia aibu sana! alisema maneno ya kibaguzi mno!
 
Uzini wamejaa makafiri ndo wamechagua ccm A
Jussa mwingine huyo wakati kwa mungu hakuna kafiri wala nani,kwani wote ni waja wake,na ndio maana kuna usemi wa Mungu si athmani ,watu wa sampuli kama yenu kama mgepewa uwezo wa kimungu kwa kuwa na roho zenu chafu dunia hii ingekuwa mawe,wewe ni nani hadi uwaite watu makafiri?si ajabu hao unawaita wewe makafiri ndio wanakufanya uishi kwa njia moja au nyingine ,hivi unajua hiyo kompyuta unayotumia kaitengeneza nani?ama kwa hakika baniani mbaya kiatu chake dawa
 
jamani mwacheni huyu mwarabu jussa na nadhani tuache kumjadili kabisa kwani si mtanzania kwa sasa baba zake wadogo wote wameshakimbilia oman sasa nayeye anatafuta sababu ya kufukuzwa aende huko
Kwa nyongeza tu navilaumu vyombo vya habari kwa kumpa nafasi huyo Jussa,je wahariri wa habari kazi yao nini ,nafikiri kazi yao pia ni kuangalia habari ipi itangazwe na ipi iwekwe kapuni,naona tumesahau ya Rwanda na huko Kenya ,sote tunajua radio na tv zilivyochochocea vita ,ndio maana watu kama akina Sang wa KASS redio wansubiri mashtaka huko Hague.Hivi kweli haya maneno angesema mtu kama Lema au Lissu ,kweli Mwema angekaa kimya,umefika muda vyombo vya habari vimuweke kwa carpet huyo Jussa,sio bure hicho kiburi cha Jussa kina kitu nyuma ya pazia ,hapo nyuma hakuwa na hiyo jeuri,WATU WATASHINDWA KUTEMBEA NA MIKASI YA KUKATIA UTEPE kama hakutakuwa na amani
 
Jamani tarifa sahihi ni kuwa jusa amedanganya,ukweli ni kuwa raza ni rais wa jamatini ambako walikubaliana jamatini sehemu ya ibada ya washia walikubaliana kuwa lazima rais wa jamatini ashinde ili nao waungane ,moja mbili jusa naibu katibu
mkuu amesaliti a cuf kwa maslahi ya tasisi ya dini yake ya shia na sasa anapotosha uma rejeni makubaliano yake na rostam wote shia
Na wewe pia unaongea lugha ya Jussa lakini kwa kutumia maneno mengine!!
 
Hiyo link niliyoweka hapo ya youtube iweke kwenye original post yako pls
 
Back
Top Bottom