Kauli ya werema bungeni, mtazamo wangu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya werema bungeni, mtazamo wangu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nsami, Jul 21, 2012.

 1. n

  nsami Senior Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana jamvi habari?

  Jana bungeni mwanasheria mkuu wa serikali mhe. Werema alitoa kauli yenye utata ya kuwa "....kazi ya kichwa si kuotesha nywele tu, ni pamoja na kufikiri...." kauli hii inakuja mda mfupi baada mhe. Lisu, mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni kuomba idhini kwa spika kutoa hoja ya kuahirisha shughuli zilizopangwa ktk order paper ili kujadili ajali ya Mv Skagit.

  Kuna swali la kujiuliza! Werema analenga kufikisha ujumbe wake wapi na kwa nani na kwa lengo gani?

  Majibu ya swali hili ni mengi.
  1. Yawezekana anamlenga mhe. Lisu, na wapinzani wote kuwa mbunge huyu (na wenzie) hawezi kufikiri ingawa ana kichwa na nywele, kuwa anatumia kichwa chake vibaya hakitumii kufikiri bali kufugia nywele!

  2. Yawezekana alimlenga mnadhimu mkuu wa serikali mhe. Lukuvi (na wabunge wote wa chama tawala) kuwa hawatumii vichwa vyao kufikiri na kuona ni hoja gani iletwe bungeni badala yake wanatumia vichwa vyao kufugia nywele na kuwaachia wapinzani wanaleta hoja nzito kama hizo bungeni na kujiongezea umaarufu, pengine....

  3. Yawezekana alimlenga N/spika, na viongozi wenzake ndani ya bunge kuwa anaongoza kiti kinachohitaji mtu anaejua kufikiri na sio kufuga nywele! na kwa udhaifu huo huo N/S anashindwa kuona ni tusi na dharau kwake badala yake anamshabikia na kusema kauli yake haina tatizo!

  4. Na pengine bwana mkubwa huyu alikuwa anajizungumzia yeye mwenyewe akilenga kumfikishia ujumbe boss wake aliyemteua kuwa nafasi yake inahitaji mtu anayetumia kichwa chake kufikiri sio kufuga nywele kama afanyavyo yeye.

  Kwa kuwa hakupata muda wa kulifafanua hili nje au ndani ya bunge, sisi tusiokuwa na nywele ambao kazi ya vichwa vyetu ni moja tu kufikiri! tunaendelea kufikiri!

  Unaweza kuongezea majibu yako hapa!
   
 2. Bolizozo

  Bolizozo Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :A S 465::A S 465:Ni dhahri kuwa Kauli ya Werema ilimlenga moja kwa moja Tundu Liso kwani ndiye aliyekuwa akijibiwa hoja yake kwa wakati huo. Matusi au maneno ya kejeli na dharau si kitendo cha kiungwana kwa mtu yeyote mwenye akili timamu. Aidha kuunga mkono Tabia mbaya kama alivyofanya Naibu Spika, mtu ambaye kikanuni anatakiwa kuwa neutral, kuna lidharilisha Bunge na ni chanzo cha uhasama ambao usipodhibitiwa unaweza kuleta Mazda ndani ya Bunge na mafioso yake yanaweza kusambaa Hadi kwa wananchi. Madhala haya yanapasa kudhibitiwa na Mkuu wa Kaya kwani ndiye mwenye dhamana ya kuliendesha Taifa hili njia iliyo sahihi.
   
 3. i

  iseesa JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu siyo siri kuwa Werema anamuogopa Tundu Na hamuwezi kwa hoja. Hivyo basi amebaki kutoa mipasho. Kwa wataalamu wa Saikolojia hii inaashiria despair, frustrations na inferiority complex. Werema ni "Mtu mzima Hovyooo!"
   
 4. m

  maingu z Senior Member

  #4
  Jul 21, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mkuu wa kaya gani wa kudhibiti hali hii ikiwa yeye mwenyewe dhaifu bin hoi taabani yupo yupo tuuuu!
  Yaani ni ujinga kuendelea kumtegemea huyo mkuu wa kaya. Kwani nadhani hata maarifa yamemwishia amebaki......kuchekacheka tu
   
Loading...