Kauli ya waziri wa viwanda: damira na matendo ya serikali vinakinzana

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
1,163
1,125
Nalisalim jukwaa la JF,
Ukisikiliza hotuba na kauli mbalimbali za Rais wetu JPM zinaonyesha wazi kuwa dhamira yake ni njema na ni kuwasaidia watanzania wanyonge ili waondokane na umaskini walio nao. Lakini kinachonisononesha pia ni kauli mbalimbali za viongozi waandamizi wa serikali wanazotoa na maaamuzi yao hayajielekezi kwenye damira kuu inayohubiriwa.
Niweke mfano mmoja tu mbele yenu kudhihirisha na kukazia hoja yangu.
Hivi majuzi waziri wa viwanda na biashara alisikika akiwaambia wafanyabiashara ya usafirishaji/wamiliki wa malori kuwa wapaki magari yao na watafute kazi nyingine ya kufanya. Jambo hili lilinisangaza kwa sabababu ya hasara za kiuchumi kwa serikali na haswa kwa jamii ya wafanyabiashara wadogo wanaonufaika na kuwepo kwa biashara hii ya usafirishaji kwa njia ya malori.
1. Kiwango cha matumizi ya mafuta na vilainishi kitashuka hivyo kodi zote kwenye mafuta makusanyo yake yatashuka. mfuko wa barabara ujiandae kwa ukata na matengenezo ya barabara za vijijini yatapungua.
2. Biashara kwenye vituo vya mafuta itashuka hivyo vingine vutafungwa na wafanyakazi wake kupunguzwa.
3. madereva na wasaidizi wao watapoteza kazi. angalia ni familia ngapi zitaathirika.
4. Gereji za utengenezaji wa magari makubwa zitaathirika kwa kiasi kikubwa. ziangalie familia zitakazoathirika.
5. Maduka ya spea na waagizaji wake watakaokosa biashara na hivyo kuwaachisha kazi wafanyakazi wao.
6. Wanyabiashara wa hoteli, nyumba za kulala wageni na mama ntilie wote wanaoudumia malori kwenye mnyororo wote wa njia utaathirika kwa kiasi gani.
7. wenye nyumba wote wanaowapangisha wote wanaofanya hizi biashara wataathirika kwa kiasi gani?

orodha ni ndefu ukitafakari kauli za viongozi kama hawa na dhamira halisi.

najiuliza na nakuuliza wewe mwana JF tufanyeje viongozi wetu wafahamu kuwa dhamira zao zinaweza kuwa nzuri ila maamuzi yao yanatunagamiza !!!!

Nawasilisha tujadili na tuwashauri
 
ukitoa ushauri wewe ni mchochezi.

kwa ujumla hii serikali imekula jezi.
 
Back
Top Bottom