Kauli ya Waziri wa Maji iende mbali zaidi kwani miji mingi tunauziwa Maji kwa bei kubwa

T2020CDM

Senior Member
Oct 17, 2020
134
212
Maji ni uhai wa vitu vyote vinavyopumua Dunia, nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri kwa kushugulikia tatizo hili ambalo limekuwa sugu hasa kwa wauza Maji ya ku pump kutumia pump za dezel au uneme.

Imekuwa kawaida kwa wasambazaji wa huduma hii kujiongezea kiwango Cha pesa pasipo washirikisha wateje.

Napenda kuuliza huku mpiji Magoe wilaya ya Ubungo mbona tunauziwa Maji Tena ya chumvi kwa Tzs 2,000/= kwa unit je mamlaka husika zinajua? Na tunaambiwa nafasi za kuunganishiwa Maji hazipo badala yake unapewa utaratibu mwingine kuwa toa kiasi kadhaa cha pesa unapewa risiti ya kuandikwa kwa mkono kisha unaandikiwa vifaa vya kununua mpaka mita ya maji ambayo ni Mali ya shirika.

Kiukweli wananchi hawajui wafanye nini na walalamike wapi.

Tunomba mamlaka zinazohusika zitoe majibu.
 
Mbona huko Mpiji Magoe mnanafuu?

Nenda Msakuzi hapo jirani tu. Msumi pale. Tegeta n.k ni 4000 hadi 6000 kwa unit na watu wanaishi.
 
Mbona huko Mpiji Magoe mnanafuu?

Nenda Msakuzi hapo jirani tu. Msumi pale. Tegeta n.k ni 4000 hadi 6000 kwa unit na watu wanaishi.
Waziri amepwaya, mimi namshauri afungue platform ya kupokelea malalamiko moja kwa moja kutoka kwa wananchi kuhusu kero za maji
 
Back
Top Bottom