Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,641
- 218,085
Nchi yenye wasomi wengi kama Tanzania haiwezi kunyamazia kauli ya Mh Majaliwa ya ku ignore barakoa zilizotumiwa na madaktari wetu miaka nenda rudi kuwalinda na maambukizi ya magonjwa wanapowahudumia Watanzania kwenye hospitali za umma na nyinginezo.
Hii ni kwa sababu wenye mamlaka ya kuhakiki ubora wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ni serikali yenyewe , leo Waziri Mkuu anapoanza kutilia shaka bidhaa ambazo zinapitishwa na mamlaka anazozisimamia na kulipiwa kodi, tena zilizotengenezwa kwa viwango vya WHO na wakati huo huo akaanza ku promote barakoa za "Dengrizi" zisizo na viwango vyovyote, zilizoshonwa na fundi cherehani wa Buza kwa Mpalange ambaye hata VETA hakupita , inahitajika Maombi mazito sana kwa ajili ya nchi hii .
Nawaomba wasomi na wataalam (hasa wa afya) mtuthibitishie bila uoga kama kweli barakoa za " Climplin au chilimeni ama dengrizi " zinaweza kuwa na ubora kuliko barakoa zinazotengenezwa kwa viwango vinavyoelekezwa na WHO.
Naomba kuwasilisha.