Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,502
- 4,408
Imenibidi kwa mara nyingine nijiridhishe kwa kurejelea kusikilizwa hotuba ya Mhe.Rais iliyokuwa inazungumzia kupanda bei kwa vitu kunakosababishwa na vita vya Ukraine na Russia na mapokeo ya kauli hiyo.
Sio kwamba nimetumia muda kusikilizwa tena sikusikia vizuri ila nilifanya hivyo kuongeza uelewa binafsi na kujiridhisha nia ya kutolewa kauli ile. Je, haikupaswa kutolewa au ingetolewaje?
Alichifanya Mhe. Rais ni kuweka kumbukumbu sawa kwa wanaoelewa na wataamua kupotosha na wasiolewa kabisa. Watanzania tuna tabia ya kusahau, kesho Mbowe au Lissu akipanda jukwaani na kudai Serikali imeamua kwa makusudi kupandisha bei ya vitu si wote watakaokumbuka kulikuwa na vita na moja ya madhara ya vita ile ilisababisha vitu kupanda. Watu watakuwa wamesahau na hiyo itakuwa ni agenda na wengi wanaolalamika wanalalamika agenda hiyo kuzimwa.
Ukweli ulio mchungu ambao wanaoujua hawataki watu waujue kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kisiasa ni kwamba Tanzania ni 'importer' na bidhaa nyingi tumeagiza kutoka nje ambako ni watumiaji wakubwa wa mafuta na gesi ya Urusi katika uzalishaji na kwa sababu ya vita inayoendelea upatikanaji wa mafuta na gesi umekuwa wa kusuasua kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo:
i) vikwazo
ii) usalama
iii) malipo kutokubalika kwa mfumo uliozoelewa, n.k.
Tutajadili siku nyingine juu ya mambo mpaka kupelekea kuadimika kwa mafuta na gesi.
Hivyo, hata kama mafuta na gesi tunayotumia hayotoki Urusi lakini kwa sababu tunategemea bidhaa zinazozalishwa kwa gesi na mafuta ya Urusi basi kuathirika kwa doko kwao kutaathiri soko zima la nchi tegemezi.
Mfumo wa soko( market system) bei inategemea hali ya uhitaji na upatikanaji wa malighafi na vingine vingi. Tukitumia kanuni ya 'demand na supply' kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa nyingine zinazotegemea au kutumia mafuta kwa nchi yetu pia haiepukiki.
Ni ukweli usiopingika vitu vitapanda bei kutokana na kupanda bei katika soko la dunia sehemu ambayo Rais Samia hawezi kuzuia zaidi ya kuacha kanuni ya soko kufanya kazi.
Katika mazingira haya Serikali inatakiwa kudhibiti upandaji wa bei kiholela upandaji usiozingatia misingi ya kanuni ya soko lakini kusema itaweza kuzuia vitu kupanda bei ni kudanganywa wenyewe. Wanaoratibu bei ya soko ndio wameathiriwa na mfumuko wa bei ,kwa hiyo tutegemee bei Tanzania ibaki ileile?
Nampongeza Mhe.Rais kuwa muwazi na zaidi katuweka tayari kufunga mikanda dunia inapoelekea janga jingine la kiuchumi baada ya Corona kuonekana sio tishio tena.
Tumsaidieni Mhe.Rais kuusema ukweli huu, kwenye vita ya uchumi hatakiwi kupambana mwenyewe. Mwisho napenda kunukuu maneno ya Biblia yanayosema"Watu wataijua kweli nayo kweli itawaweka huru kwelikweli" na ninukuu pia msema wa kiswahili unaosema "mficha maradhi kifo humuumbua"