Kauli ya UVCCM dhidi ya Dr. Slaa ni ya uchochezi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya UVCCM dhidi ya Dr. Slaa ni ya uchochezi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MANAMBA, Jan 24, 2011.

 1. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #1
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umoja wa vijana wa ccm hivi karibuni ulitoa kauli ya kuitaka serikali imkamate kwa nguvu dr. Slaa na kwenda kumpima akili. Ingawa kauli hiyo imejibiwa kistaarabu na dr. Slaa mwenyewe kwa maoni yangu nadhani kauli ile ya vijana wa ccm ni ya kihuni, ya kukosa adabu kwa mtu mzima na ya kichochezi ambayo ingeweza kuvunja amani na utulivu. Nilitarajia kusikia wapenda amani wakiilaani vikali kauli kama zile kwani endapo vijana wa chama cha dr. slaa au chama kingine chochote cha upinzani kingetoa kauli ile kwa viongozi wa juu wa ccm hivi kweli wasingekamatwa kwa uchochezi?

  Katika hali ya kawaida katika nchi yetu hatukuzoea kuona vijana wadogo wakiwatukana watu wazima, hiyo siyo heshima au ndiyo kielelezo cha mmomonyoko wa maadili? hata kama hiyo ni sissa kauli hiyo ilipaswa kutolewa na kiongozi wa ccm aliye wa kaliba ya dr. Slaa siyo vijana wale. Haya ndiyo mambo ambayo hata ccm wenyewe walitakiwa kuyakemea kwani yanakiongezea lawama na kupoteza umaarufu bure.

  Endapo uvccm wanaamini kuwa dr. Slaa anamatatizo ya akili kama walivyodai eti kwa sababu ya kuitisha maandamano ya Arusha basi siyo tusi kwa dr. Slaa peke yake bali ni kwa maefu ya wote walioitikia mwito ule. Je vijana hao wanataka kutulazimisha tuamini kuwa wana Arusha wale kwa maelfu hawana akili ila wenye akili ni uvccm?

  Ingawa mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini nadhani lipo tatizo katika nchi yetu kwa baadhi ya watu kutotambua maana ya kuwepo kwa vyama vingi vya siasa. Inapotokea mpinzani akipinga jambo lolote inatafsiriwa kuwa ni uchochezi! Endapo wapinzani wasipopinga mambo ambayo kwao wanayaona kuwa ni kinyume cha taratibu na maslahi ya taifa badala yake wakakubaliana na kila kinachofanywa na chama tawala, maana ya upinzani itakuwa nini?

  Fanyeni siasa zenu na chungeni ndimi zenu ila mtuachie amani yetu.
   
 2. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  asante kwa hili mkuu,naamini chama makini kingelitolea ufafanuzi suala lile na kikalisemea katika lugha ya kistaarabu ili kisionekane ku-set precedent.Kama vyamaa vingine vikianza siasa za majitaka, uwanja wa siasa za kistarabu hautakuwepo tena. u
   
Loading...