Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,303
- 12,962
Wakati ambapo rais amemteua Dr. Asha Rose Migiro kuwa mbunge na hatimaye pengine akateuliwa kuwa waziri, kuna fununu kuwa huenda anaandaliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015.
UVCCM Bagamoyo waliwahi kutoa tamko kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 hatatoka kanda ya kaskazini.
Sasa najiuliza Migoro anatoka kaskazini. Lakini pia kuna wanaCCM wengine kutoka kaskazini wapo katika kampeni kubwa ya kuwania urais 2015. Hawa ni Edward Lowassa, Fredrick Sumaye na hata Steven Wassira naye nasikia yumo.
Kauli ile haijawahi kutenguliwa au kukemewa na kiongozi yeyote wa CCM sawa na kauli ya "..wapigwe tu, maana tumechoka sasa..." ya Bwana Mizengo Pinda.
Wakati huu wagombea wa CCM kutoka kaskazini wanapozidi kujiimarisha na kuimarishwa katika CCM hali itakuwaje. Maana kaskazini ndiko Nape amekuwa akikipiga vita CHADEMA kuwa kimeegemea kanda hiyo na ukabila kwa kanda hiyo akisahau kuwa hata rais wa kwanza na mwasisi wa CCM marehemu Mwl J. K. Nyerere anatokea kaskazini.
Sasa inakuwaje wakati huu harakati za wagombea kupitia CCM zikionekana wazi kuwa kaskazini ina wengi kuliko kanda nyingine na wakati jumuiya imeweka msimamo na Nape akipigilia msumari wa mwisho?
Haya yakifanyika kwa CHADEMA wataita ukanda, kwa CCM naona mhubiri mkuu wa udini, ukanda na ukabila Nape yupo kimya.