Kauli ya UVCCM Bagamoyo kuwa rais hatatoka kaskazini vipi kwa Lowassa, Migiro na Sumaye?

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,303
12,962
Wakati ambapo rais amemteua Dr. Asha Rose Migiro kuwa mbunge na hatimaye pengine akateuliwa kuwa waziri, kuna fununu kuwa huenda anaandaliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015.

UVCCM Bagamoyo waliwahi kutoa tamko kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM 2015 hatatoka kanda ya kaskazini.

Sasa najiuliza Migoro anatoka kaskazini. Lakini pia kuna wanaCCM wengine kutoka kaskazini wapo katika kampeni kubwa ya kuwania urais 2015. Hawa ni Edward Lowassa, Fredrick Sumaye na hata Steven Wassira naye nasikia yumo.

Kauli ile haijawahi kutenguliwa au kukemewa na kiongozi yeyote wa CCM sawa na kauli ya "..wapigwe tu, maana tumechoka sasa..." ya Bwana Mizengo Pinda.

Wakati huu wagombea wa CCM kutoka kaskazini wanapozidi kujiimarisha na kuimarishwa katika CCM hali itakuwaje. Maana kaskazini ndiko Nape amekuwa akikipiga vita CHADEMA kuwa kimeegemea kanda hiyo na ukabila kwa kanda hiyo akisahau kuwa hata rais wa kwanza na mwasisi wa CCM marehemu Mwl J. K. Nyerere anatokea kaskazini.

Sasa inakuwaje wakati huu harakati za wagombea kupitia CCM zikionekana wazi kuwa kaskazini ina wengi kuliko kanda nyingine na wakati jumuiya imeweka msimamo na Nape akipigilia msumari wa mwisho?

Haya yakifanyika kwa CHADEMA wataita ukanda, kwa CCM naona mhubiri mkuu wa udini, ukanda na ukabila Nape yupo kimya.
 
Tulimumu, Nyerere na Wasira ni wa kaskazini kweli? Makubwa haya! geografia yako haipo sawa au historia ya watu hawa kwakao haijakaa sawa! Au una maana gani? nakubalina Lowassa, Sumaye na huyu mpare Mama Migiro wanatoka kaskazini.
 
kama hapo kuna shida, basi inatuhusu wengi, kaskazini kwangu mimi nikiiangalia ramani naona yuko sawa!
 
Nadhani hizi ni kauli zilizokuwa zikitolewa kisiasa zaidi na hazipo kiuhalisia. Sidhani kauli ya Nape inaweza kuchukuliwa kiuzito zaidi kuwa ni kauli ya chama.
 
but ninavyojua migiro mtu wa ruvuma hebu tembeleeni biography yake
 
jina lake halisi ni ASHA ROSE MTENGETI ni mpare kaskazini ahahahha
 
huu mnakasha naona bado unamatege.mara ruvuma,mara upareni.mwe! mwe!.
 
Jiografia inasumbua hapa Tulimumu
sahihisha basi. Pipoooozi.....Pawaa.
Sumaye anatoka Arusha, Asha Rose Migiro anatoka Kilimanjaro, Edward Lowassa anatoka Arusha, Steven Wassira na Nyerere wanatoka Mara kote huko ni kaskazini mwa Tanganyika. Angalia ramani labda unababaika na Mara iko kaskazini ingawa huwa wanaiweka kaskazini magharibi
 
Asha rose migiro ni mpare anatoka wlaya ya mwanga tarafa ya usangi kata ya chomvu kijiji cha mshewa mtaa wa mchali karibu na kanisa la kkkt mchali

Afadhali mkuu umenisaidia kumbe watu hawajui asili za viongozi wengi. Ungemalizia kwa kuwapa na mkoa ambao ni kilimanjaro. Mimi nimewahi kuishi mpaka kwenye nyumba yake hapo Usangi!
 
Tulimumu, Nyerere na Wasira ni wa kaskazini kweli? Makubwa haya! geografia yako haipo sawa au historia ya watu hawa kwakao haijakaa sawa! Au una maana gani? nakubalina Lowassa, Sumaye na huyu mpare Mama Migiro wanatoka kaskazini.
Wanatoka mkoa wa Mara ambao uko kaskazini mwa Tanganyika ingawa huwa wanasema uko kaskazini magharibi. Kama ilivyo Kilimanjaro na Arusha nao unapakana na Kenya. Sasa kama Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha iko kaskazini na inapakana na Kenya na wakati huo huo Mara nayo inapakana na kenya, huko kutakuwa wapi kama sio kaskazini? Au itakuwa ni Karibu na Mtwara?

Kwa upande wa kaskazini mwa Tanganyika mikoa inayopakana na Kenya ni Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Mara. Hapo unaweza hata kumuongeza January makamba kama mgombea mwingine wa CCM mtarajiwa kutoka kaskazini ingaw Tanga nyo huwa inawekwa kaskazini mashariki.

Sasa, iwe kaskazini mashariki au magharibi zote hizo ni kwa umoja zinaitwa kasakazini. Tofauti ya hiyo kaskazini ni kuwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro uko katikati yamikoa ya Mara na Tanga lakini yote ipo kaskazini na yote inapakana na Kenya!
 
Mama Migiro anatokea mkoa wa Ruvuma ila bwanake ndio mtu wa Kilimanjaro.
Umechemsha yeye ni mpare anatokea mkoa wa Kilimanjaro wilaya ya Mwanga tarafa ya Usangi. Labda huyo mumewe ndio atakuwa anatokea huko Ruvuma!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom