Kauli ya Tibaijukwa ya kutangaza viwanja yawa kiinimacho-Kigoma Manispaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya Tibaijukwa ya kutangaza viwanja yawa kiinimacho-Kigoma Manispaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul J, Sep 7, 2012.

 1. P

  Paul J Senior Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nikiwa Kigoma lilipita gari likitangaza kuwa manispaa imekamilisha upimaji wa viwanja katika maeneo ya Kibirizi na Bushabani kwa ajiri ya makazi na biashara hivyo kuwataka wananchi wachukue form kwa ajiri ya kuomba kupatiwa viwanja katika maeneo husika. Mwisho wa kuchukua form ilikuwa iwe tarehe 11/9/2012 na gari lilianza kutangaza 4/9/2012, bei ni Tsh 2500/sqm na form ni Tsh10,000/=. Huwezi amini gari limetangaza jioni mida ya saa mbili kasorobo lakini asubuhi yake unaambiwa viwanja kwishenea na hawatoei tena form. Baada ya kuuliza kulikoni nikagundua kumbe viwanja viliisha uzwa muda mrefu watu wana lease tayari na wengine walishajenga misingi ila tangazo lilikuwa ni kiini macho kumfurahisha Tibaijuka na kuadaha umma wa wadanganyika! Mheshimiwa Tibaijuka naomba uwaulize manispaa ya Kigoma lini walitangaza viwanja na kwa muda gani wananchi walichukua form? Kuna arufu ya ufisadi mkubwa hapa! Time will tell
   
Loading...