Kauli ya Spika Ndugai kuhusu Makonda imetupa siri tatu muhimu

Beem

JF-Expert Member
May 18, 2018
1,630
2,425
Habari Wakuu, kutokana na kauli ile ya Mhe Spika Bungeni akimzungumzia kijana yule, kuna siri 3 ambazo zimekuwa wazi

1. Kijana ana nguvu, kama mwenyewe alivyotamka ndivyo inavyoonekana kuwa hivyo. Cheo cha Uspika ni cheo kikubwa sana kikatiba na ana nguvu kubwa kwa sababu ya kuongoza mhimili wa Bunge . Pamoja na ukubwa wa cheo chake lakini anakiri tena kwa unyonge kuwa kijana ana nguvu tena kuliko yeye tofuati na uhalisia wa vyeo

2. Kijana ana kikosi kazi kwa ajili ya propaganda na 'information warfare' ambacho anakitumia yeye kwa maslahi yake na kikundi chake. Bila shaka na JF hakikosekani. Na amekiri kimekuwa kikitumika kuwachafua viongozi wengine

3. Viongozi wengi wakubwa hawampendi, ndio maana ya maneno kuwa "hajitambui na hajielewi". Maneno haya makali yanaashiria kuwa yalikuwepo moyoni kwa muda mrefu sasa ndio amepata nafasi ya kuyatoa. Na kitendo cha wabunge wa Chama chake kushangilia ni ishara tosha kuwa kijana hata ndani ya chama chake hapendwi na wanaompenda wanampenda kinafki kwa hofu ya Mzee

Baada ya Katibu Mkuu wa Chama kusema,ikaja kauli ya mstaafu kwenye Harambee ya Yanga na leo ni Spika. Ni dhahiri kijana 'is not popular' kwa wazee
 
Pipa na mfuniko tu wote hao, ila dogo Makonda amejisahau sana,na anguko lake haliko mbali sana,maana kama ni mbereko itachanika tu,JPM kama hajui kuna asilimia kubwa anachukiwa kutokana na huyo dogo.

Spika kwa unyonge kabisa kama kamwagiwa maji analala kifo cha mende kabla dogo Zitto haja update ubongo wa Spika na ghafla naye akajikaza kaza kiaina ila tayari alikuwa ameshaonyesha "UDHAIFU" nikamkumbuka hadi sieiji
 
Mbeleko hiyo sidhani kama itachanika kama mpaka sasa haijachanika. Acha ale raha miaka mitano iliyobakia
 
Back
Top Bottom