Kauli ya Rais wa Turkey, Kuna somo la kujifunza hapa

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
2,000
Nimetazama taarifa za matukio ya jaribio la kutaka kumpindua Rais wa Turkey....Kwa waliotazama speech yake ni kuwa amewaomba wananchi wafanye maandamano kuelekea kwenye uwanja Taksim square.

Swali nililojiuliza ni kuwa;
Kwa nini Rais Erdogan hakuomba vyombo vya ulizi na usalama kama polisi, magereza, FFU, Usalama wa taifa, na majeshi na private companies kuzuia jaribio! isipokuwa aliwaomba wananchi kuandamana kuzuia kupinduliwa kwake?
Nilichojifunza ni kuwa hata watawala wanatambua kuwa nguvu kubwa kabisa ni nguvu ya umma "wananchi", wala sio mabomu ya machozi, vifaru n.k

Erdogan ametoa somo kubwa sana kwa watawala....

Ni hayo tu

Tume ya katiba

Mod tafadhari msiunganishe huu uzi...kuna kaujumbe hapa
 
HEKIMA KWANZA

JF-Expert Member
Mar 31, 2015
2,882
2,000
Kwa nini Rais Erdogan hakuomba vyombo vya ulizi na usalama kama polisi, magereza, FFU, Usalama wa taifa, na majeshi na private companies kuzuia jaribio! isipokuwa aliwaomba wananchi kuandamana kuzuia kupinduliwa kwake?
Nilichojifunza ni kuwa hata watawala wanatambua kuwa nguvu kubwa kabisa ni nguvu ya umma "wananchi", wala sio mabomu ya machozi, vifaru n.k

Erdogan ametoa somo kubwa sana kwa watawala....

Ni hayo tu

Tume ya Katiba hebu na wewe jiongeze kidogo. Erdogan ataomba vipi msaada kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakati mageuzi yamefanywa na hivyo vyombo? Yaani mtu aombe msaada kwa watu wale wale wanaompindua?
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,795
2,000
Tume ya Katiba hebu na wewe jiongeze kidogo. Erdogan ataomba vipi msaada kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakati mageuzi yamefanywa na hivyo vyombo? Yaani mtu aombe msaada kwa watu wale wale wanaompindua?
sina cha kuongeza...mod funga huu uzi tafadhali
 
Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
2,000
Akili ya mleta maada haina akili...km wananchi wa Turkey wangekua wameandamana kumpinga angeamuru jeshi kumlinda..ila kwa sasa Jeshi limemuasi sasa anaomba wananchi kumlinda
Mkuu ni ka portion tu ka wanajeshi, lakini idadi kubwa ya jeshi lilikuwa nyuma yake sambamba na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.....kwa nini aombe msaada kwa wananchi? ni kwa kuwa anatambua nguvu ya umma dhidi ya hayo mavifaru..
 
  • Thanks
Reactions: cmp

zionale

Member
Oct 13, 2012
25
75
Tume ya katiba hebu tafakar kwa kina kabla hujapost.
Ni hivi, Raisi anahitaji maandamano ya wananchi ili kuionesha dunia kuwa ile 52% iliyomuingiza madarakani kwa kura bado inamhitaji. Wakiandamana wengi inamhalalishia yeye kutumia wanajeshi watiifu kuendeleaza mapambano. kumbuka hadi sasa wanajeshi zaidi ya 1500 wametiwa nguvuni, zaidi ya 1100 wamejeruhiwa, watu zaidi ya 190 wamekufa wakiwemo police zaidi ya 40. Hivyo mgogoro ni mkubwa kwani nusu ya wanajeshi wa vikosi vya anga na ardhini wameasi na hawataki kusalimu amri. Duru zinaonesha kuwa wanajeshi wanaoasi wanaongezeka na pia wananchi wanaopinga Arabic migration hawaitaki serikali. aidha, msimamo wa raisi kuhusu jimbo la kurd hauwafurahisi wananchi.
 
Return2roots

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
874
500
Mkuu ni ka portion tu ka wanajeshi, lakini idadi kubwa ya jeshi lilikuwa nyuma yake sambamba na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.....kwa nini aombe msaada kwa wananchi? ni kwa kuwa anatambua nguvu ya umma dhidi ya hayo mavifaru..
...we utakuja waingiza mkenge wenzio kwa mapungufu ya matukio yakihistoria...kamilisha na kuuliza kilichojiri ktk tianmen square, uchina...!
 
MNYAMAKAZI

JF-Expert Member
Oct 7, 2014
2,123
2,000
Unafikiri wananchi wangeandamana dhidi ya serikalu asingetumia hivyo vyombo kuwatia discipline? Unaongea vitu kinyume & hakuna la kujifunza, watawala wote wa nchi zenye demokrasia changa wana tabia moja.
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,890
2,000
Tume ya Katiba hebu na wewe jiongeze kidogo. Erdogan ataomba vipi msaada kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakati mageuzi yamefanywa na hivyo vyombo? Yaani mtu aombe msaada kwa watu wale wale wanaompindua?
Kwani anashindwa vipi kushawishi wanajeshi/askari watiifu kwake kuzuia mapinduzi?Sema anajua kabisa umma ndo solution ya kutokupinduliwa kwake.
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,890
2,000
Akili ya mleta maada haina akili...km wananchi wa Turkey wangekua wameandamana kumpinga angeamuru jeshi kumlinda..ila kwa sasa Jeshi limemuasi sasa anaomba wananchi kumlinda
Jeshi halijamuasi bali ni kundi dogo sana la askari walioasi ndo maana waliweza kuzingirwa na polisi na kujisalimisha wenyewe.
 
cmp

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,890
2,000
Mkuu ni ka portion tu ka wanajeshi, lakini idadi kubwa ya jeshi lilikuwa nyuma yake sambamba na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.....kwa nini aombe msaada kwa wananchi? ni kwa kuwa anatambua nguvu ya umma dhidi ya hayo mavifaru..
Huu ndo ukweli ila watu wataleta hoja zisizo na mashiko.Huwezi kupambana na nguvu ya umma hata utumie vifaru vipi.
 
master09

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
788
1,000
Tume ya Katiba hebu na wewe jiongeze kidogo. Erdogan ataomba vipi msaada kutoka vyombo vya ulinzi na usalama wakati mageuzi yamefanywa na hivyo vyombo? Yaani mtu aombe msaada kwa watu wale wale wanaompindua?
Hiyo sawa.... Lakini alikuwa na jeshi linalo mkubari siyo wote walitakakumsalit tho katika hari km hyo kumwamini mtu wakati shughur isha anza yataka moyo ndo maana his last resort ilikuwa wananchi.... (nb: hilo hilo jeshi ndo lilimrudisha kwenye kitu baada ya wasaliti kuuwawa au kukamatwa)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom