Kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwalipa wastaafu kila mwezi imetekelezwa kwa kiasi gani, Msemaji wa Serikali ashindwa kujibu

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Mhe shimiwa Rais alisimama mwezi baada ya kuapishwa na kuahidi kuwa Serikali yake itaanza kuwalipa wastaafu wa PSSF kila mwezi ili kupunguza uwingi wa wastaafu hao na hii ndio dhamira yake, leo Msemaji wa Serikali akitoa taarifa na ufafanuzi kuhusu maswala mbali mbali Msigwa kaja na mpya anasema ni baada ya miezi 6 ndio watakuwa wanalipwa, suala la utekelezwaji wa Kauli ya Rais haujafanyiwa kazi, Swali ni je zipo kauli anazozitoa Rais zenye uzito na zingine zisizo na uzito hadi wasemaje wa serikali wanakuwa wanashindwa kufafanua.

Tutaona na tutasikia mengi muhimu na yasiyo ya muhimu.
 
Mhe shimiwa Rais alisimama mwezi baada ya kuapishwa na kuahidi kuwa Serikali yake itaanza kuwalipa wastaafu wa PSSF kila mwezi ili kupnguza uwingi wa wastaafu hao na hii ndio dhamira yake, leo Msemaji wa Serikali akitoa taarifa na ufafanuzi kuhusu maswala mbali mbali Msigwa kaja na mpya anasema ni baada ya miezi 6 ndio watakuwa wanalipwa, swala la utekelezwaji wa Kauli ya Rais haujafanyiwa kazi, Swali ni je zipo kauli anazozitoa Rais zenye uzito na zingine zisizo na uzito hadi wasemaje wa serikali wanakuwa wanashindwa kufafanua. Tutaona na tutasikia mengi muhimu na yasiyo ya muhimu.
Anayeongoza nchi sio yeye by polepole
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanataka wastaafu wapukutike kwa msongo wa mawazo ili watie hizo hela kibindoni. Mungu epusha hilo
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yule Rais mwanamke anayetaka kutumia uanamke wake kuwaongoza wanaume kwa mdomo wake kagonga mwamba kwenye hili.
Msigwa kadhihirisha hilo leo.
Huu ni mwanzo tuu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Utasikia mara oh tumetoa bilioni 50 mara oh tumetoa bilioni 100 kwenye miradi sijui yapi wakati wastaafu wenye pesa zao ambazo serikali iliwakata kama mafao hawataki kuwalipa. hizi pesa walizokuwa wanawakata huwaga hazina account maalumu ili kama zinazungushwa kuzalisha zingine na kutumika kwingine ziwe zinarudishwa kila mwezi na kuhifadhiwa kwenye akaunti hizo hizo. si ajabu labda watu walizila maana kama ziliazimwa si lazima zirudishwe ili mtu akistaafu tu mwezi huu na mwezi ujao anapewa chake. aibu sana
 
Waziri wa fedha aone aibu awalipe wastaafu pesa zao si amejigamba wanapata fedha nyingi kwenye tozo awalipe hawa wastaafu watawaombea laana
 
Wakije utasikia tumewalipa pensheni wastaafu tar 22 mwezi wa 9 wanakwepa ktaja MAFAO maana wanajua hawajalipa mafao na hao wanao subiria mafao wangelipwa basi pensheni
 
Back
Top Bottom