Kauli ya Rais Samia 'Nendeni mkabuni vyanzo vipya vya mapato' kumgombanisha na Watanzania?

Siri ya sifuri

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
2,014
1,498
Salaam wakuu.
"Nendeni mkabuni vyanzo vipya vya mapato"hiyo ndio amri ya bi mkubwa aliyoitoa kwa wasaidizi wake ambayo sasa inaelekea kumgombanisha na wananchi wake.

Binafsi nashindwa kuelewa ubaya wa hii kauli ya Mama ulipo. Mama ni mswahili na ninahakika anakifahamu vyema kiswahili na alichoagiza alimaanisha.

Aliwaagiza wasaidizi wake waje wabuni vyanzo vipya vya mapato lakini badala yake wao wamekuja kubuni kodi mpya kwenye vyanzo vya zamani. Je, hivyo ndivyo mama alivyoagiza!?

Ni dhahiri kwamba mama alijua vyanzo vyote vya mapato vya zamani tayari vinautaratibu wake wa kuchangia maendeleo ya taifa ndio maana ya kuwaagiza waje wabuni vyanzo vingine vya mapato ya Serikali katika maeneo ambayo bado hayachangii pato la taifa moja kwa moja.

Kwa mfano mafundi,madereva na maeneo mengine ambayo hayaja rasimishwa ndio waliotakiwa waje wayapangie utaratibu utakaowezesha kulipa kodi na sio kwenye vyanzo vile vya zamani ambavyo tayari kuna kodi chungu tele mpaka wao wenyewe wanakosa majina ya kuzipa na sasa wanaziita kodi za kujitolea. Kujitolea gani huku kwa lazima!?

Sitoona ajabu hata leo hii Mama akiamrisha kufutwa kwa tozo mpya zilizoanzishwa kwenye miamala ya simu kwasababu sicho alichoamrisha. Ni aibu kuona hadi leo hii kuna viongozi wakubwa serikalini hawakielewi Kiswahili mpaka wafafanuliwe.
 
Hizo stori zenu tulishazizoea enzi za jk maneno yalikuwa haya haya ooh wateule wake wanamwangusha kumbe jamaa yeye ndio alikuwa anawaangusha kwa ufisadi big big. Huyu nae mmeanza maneno yale yale ya kipumbuvu ooh anaangushwa mpk anaangushwa yeye ni kipofu au ni nini hasa ?!

Toka mwanzo tuliwaambia huyu hana uwezo huo wa kuhimili nchi hii ....mh jiwe ndie alikuwa mtu sahihi kuiendesha hii nchi

Hizi ni mvua za rasha rasha tu mpk 2025 mtaota mvi kwa kipigo kikali
 
hizo stori zenu tulishazizoea enzi za jk maneno yalikuwa haya haya ooh wateule wake wanamwangusha kumbe jamaa yeye ndio alikuwa anawaangusha kwa ufisadi big big....huyu nae mmeanza maneno yale yale ya kipumbuvu ooh anaangushwa mpk anaangushwa yeye ni kipofu au ni nini hasa ?!

toka mwanzo tuliwaambia huyu hana uwezo huo wa kuhimili nchi hii ....mh jiwe ndie alikuwa mtu sahihi kuiendesha hii nchi

hizi ni mvua za rasha rasha tu mpk 2025 mtaota mvi kwa kipigo kikali
tuombe uhai.
 
Na wewe unafaili milembe?
 
mi kwa Sasa sisemi,naendelea kumcheki tu ,ni mapema Sana kutoa tadhimini !2023yr nitakuwa nimepata picha kamili.
 
Back
Top Bottom