Kauli ya Rais Samia ‘Mimi na Magufuli ni kitu kimoja’ ni ya Kisiasa zaidi matendo yao yanatofautiana

Samia Hana ujanja Kwa magufuli huo ndo ukweli
Ni Sawa na magufuli Kwa kikwete,kikwete Kwa mkapa,mkapa Kwa mwinyi, mwinyi Kwa Nyerere
Kwani huyo magufuli yuko wapi mpaka Mheshimiwa Samia akose huo ujanja? Yaani Mtu akose ujanja kwa marehemu!! 🤔
 
Kwanini machadema mnahangaika sana kujaribu kujiaminisha kwamba Samia hampendi Magufuli na ccm?

Huu muda mngekuwa na akili mngeutumia kupigania zile taasisi mnazosemaga zinawanyima ushindi badala ya huu ujinga kutwa kuhangaika mara Samia vile, mara toa yule weka yule.

Yani machadema mnajikomba sana kwa mother ila sasa hana time na nyie kabisa.

Niwakumbushe tu kwamba yule ni ccm na yuko pale kwa mgongo wa ccm.
Ndio maana yakaitwa nyumbu Mkuu!
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.

Ndugai ameyasema hayo leo Jumatatu baada ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Lucy Mayenga kudai kuwa kuna kundi la wabunge wa chama hicho ambalo linamsifia Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kudhoofisha alama zilizoachwa na Hayati Rais John Magufuli.
 
Mama bado anajitahid apate kupendwa na kila MTU, which is impossible. Kuiongoza tz lazima uwe mbogo, wabongo tunahatari balaa kwa porojo na unafiki.
Well said,mimi namuangalia tu,mbaya atabezi kwa kundi la wachache
 
396DF980-3F66-4366-B04B-2244C30CF5E0.png
 
“Yeyote anayefikiria kuleta uhasama kwa Tanzania na kenya ujumbe kwake ni kuwa Tanzania na Kenya tulikuwepo, tupo na tutaendelea kuwepo," Rais @samia_suluhu_hassan.
 
Kwanini machadema mnahangaika sana kujaribu kujiaminisha kwamba Samia hampendi Magufuli na ccm?

Huu muda mngekuwa na akili mngeutumia kupigania zile taasisi mnazosemaga zinawanyima ushindi badala ya huu ujinga kutwa kuhangaika mara Samia vile, mara toa yule weka yule.

Yani machadema mnajikomba sana kwa mother ila sasa hana time na nyie kabisa.

Niwakumbushe tu kwamba yule ni ccm na yuko pale kwa mgongo wa ccm.
Huyu hajaelewa kabisa
 
Kisiasa Rais Samia Suluhu asingeweza kusema yupo kinyume na mtangulizi wake Magufuli, na hatutegemei aseme hivyo hadharani lkn inawezekana moyoni anawaza tofauti kabisa. Binafsi kinacho matter zaidi ni vitendo. Hivi ni baadhi ya viashiria vya tofauti zao kiutendaji.

————————
Magufuli: Tanzania hakuna corona ni hila za mabeberu tu ni vita ya kiuchumi.

Samia: Nitaunda tume kunishauri kuhusu Corona.
————————
Magufuli: Nchi inataka kodi kama hataki afunge biashara.

Samia: TRA msitumie mabavu kukusanya kodi TRA imewaumiza watu wengi na tunao ndugu wengi walifunga biashara zao.
————————
Magufuli: Bunge mnafanya kazi nzuri sana wabaneni huko wakija huku nje nitapambana nao.

Samia: Bunge mnachofanya hakina afya kwa taifa.
————————
Magufuli: Mahabusu waanze kufanya kazi wasikae tu na kula bure.

Samia: Angalieni kesi zisizo na maana mzifute.
————————
Magufuli: Tanzania ni tajiri kama hawezi kulipa kodi tunayoitaka waondoke tutachimba wenyewe.

Samia: Tunataka Wawekezaji wa-enjoy kuwekeza Tanzania.
————————
Magufuli: Sitasita kuzungushia ukuta sehemu yoyote yenye rasimali ambayo inaleta utata, hata ikiwa mlima Kilimanjaro nipo radhi kuulinda kwa kujenga ukuta.

Samia: Mirerani tumejenga ukuta tukaweka na Majeshi lakini Madini yanatoroshwa kama mwanzo.
————————
Magufuli: Nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari be careful, watch it, kama mnafikiri mna freedom ya namna hiyo not to that extent.

Samia: Serikali inaamini ktk Uhuru wa Vyombo vya Habari na TV zilizofungwa zifunguliwe ila zifuate Sheria.
—————————

Hizi ni baadhi ya kauli na viashiria vya utofauti wao.
Tayari watu washapewa kesi ya Uhaini
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom