Kauli ya Rais Samia iliwalenga wakina nani?

Maza amebugi sana kuwarudisha wapigaji serikalini.
All in all ,yeye ndiye amir jeshi mkuu,she has power vested to her.afanye kila linalowezekana kuondoa hizo kasoro.na aache kulaumu wenzake
 
Huu mtifuano wa Sukuma Gang vs Msoga Gang umekaa vizuri sana hadi raha.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Sema ni mtifuano wa wezi na wazalendo,Tangu lini Msoga gang wakawa watu wasafi nchi hii?

Hivi hamkuona fungulia mafisadi TOKA sero ilofanyika nchi nzima!Tena KWA hoja nyepesi ,eti ulikosekana ushahidi.

Hivi mnajua wezi wa kalamu wanavyojidhatiti wasikamatwe ila reality ni wameiba hata KWA macho unaona tu.

Hii ni vita Kati ya MAFISADI(Msoga gang) vs SUKUMA GANG(wananchi)
Na ndo tafsiri iko hivyo
 
Bi Hangaya atasanda tu,urais si mchezo.

Heri ya akina Polepole wanaoongea leo kuliko hao waliokaa kimya ili waongee akitoka madarakani.

Tumeona waliokuwa wamekaa kimya enzi za Magufuli ndiyo wameibuka na tuhuma kibao baada ya kuondoka kwake kuliko hata waliokuwa wanapiga kelele enzi za uhai wake.
 
Mimi kila nikitafakari nakosa jibu ,kuwa huyu Pole pole mbona anajiamini Sana Ni akina Nani wamempa hiyo jeuri ya kuongea atakavyo? Maana kikawaida sidhan kama Ana nguvu hiyo ya kuongea kwa kujiamini kiasi hicho na asithibitiwe na kukemewa na yeyote yule.

Huyu mama amezungukwa na madui hapo ikulu yaan dizain wanamchora tu ,nadhan saiz kidogo akili imeanza kumkaa sawa kuwa hayuko na watu sahihi mwenye kuliongoza taifa zaidi tu wanamlia timing ili wapindue nanga.

Kuna watu Kama Katelephone ,mipango ya kazi ,na sabufa ya mjengo Nina waswas nao Sana kuwa ndio wanaomtafuna mama kimya kimya ,Hawa watu watatu naona Waz ndio mastermind wa kila kitu kwasasa ukijumrisha na mzee wa tozo ogopa Sana vile vichwa .

Muda utaongea Ila mama asipochukua hatua mapema na kujiimarisha mapema 2025 Hana chake watu wapo jikoni.
Kasimu majaliwa kasimu ataondolewa kuwa wazir mkuu. Ni suala la muda tuu
 
Sema ni mtifuano wa wezi na wazalendo,Tangu lini Msoga gang wakawa watu wasafi nchi hii?

Hivi hamkuona fungulia mafisadi TOKA sero ilofanyika nchi nzima!Tena KWA hoja nyepesi ,eti ulikosekana ushahidi.

Hivi mnajua wezi wa kalamu wanavyojidhatiti wasikamatwe ila reality ni wameiba hata KWA macho unaona tu.

Hii ni vita Kati ya MAFISADI(Msoga gang) vs SUKUMA GANG(wananchi)
Na ndo tafsiri iko hivyo
Walishawahi kuwepo wasafi lini na wapi?
Kuita mtengeza ndege ikulu na kujifungia nae ndani kuagiza ndege utakazo bila kufuata sheria ya manunuzi ya umma ni USAFI???
 
Polepole alisema ndani ya CCM kuna "Wahuni" ambao hawakumalizwa na Awamu ya Tano. Kuna watu walibeza akiwemo Nape. Sasa Mama SSH kaungana na Polepole. Mliokuwa mnambeza Polepole mnasemaje sasa!? Wahuni wapo hawapo?
watanzania ukiwa mtu wa hasira kama mwendazake unaweza ukawafyeka vichwa wote ukawamaliza.
 
Abuu Kauthar

View attachment 2033645

Mama kachefukwa kaamua atapike shombo. Nukuu yake imetembea mno mitandaoni kwa sababu moja tu: Inaashiria mambo si shwari huko serikalini na katika chama.

“Kuna makundi wanayajua wanayoyafanya ndani ya serikali ni makundi hayo hayo yanageuka kusema Serikali ya awamu ya sita ufisaidi umerudi, mambo yako hovyo, kumbe wao ndio wako hovyo.Na mambo yale hayakufanyika ndani ya awamu ya sita, yalifanyika huko nyuma gari bovu linaangushiwa awamu ya sita sitakubali. Niliapa kusimamia haki za wananchi, nitasimama nao,” alisema Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia alitoa kauli hiyo wakati wa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa gati katika Bandari ya Dar es Salaam Jumamosi Desemba 4, 2021 ambapo alilionya kundi la watu serikalini linalofanya mambo ya hovyo ya kifisadi kisha wamainyooshewa kidole Serikali hii ya awamu ya sita.

Gazeti la Mwananchi liliandika katika habari yao ya tukio hili: Samia alionya genge linalotaka kuchafua Serikali yake.”

Hii maana yake nini?

Wengi bila shaka watakuwa wanajiuliza genge analolizungumza Rais Samia ni lipi? Kauli yake inajifafanua yenyewe hasa pale aliposema: “Mambo yale (ya hovyo, ya kifisadi) hayakufanyika ndani ya awamu ya sita, (bali) yalifanyika huko nyuma (ila) gari bovu linaangushiwa awamu ya sita.”

Yetu macho!View attachment 2033644
Kuna makundi yanajua yanayofanya ndani ya serikali (makundi hayo yapo serikalini hawamu ya tano na sita) makundi hayo yanageuka na kusema mambo ya ovyo, kumbe wao ndio wa ovyo, mambo hayo yamefanyika nyuma wanakusudia gari bovu kuangushia hawamu ya sita, (huko nyuma ni hawamu ya tano, ambao sehemu yote ya serikali imeendelea hadi hawamu ya sita)
 
Jambo moja lipo dhahiri. Hali si shwari ndani ya CCM. Mama ameanza kung’amua maadui zake na amechoka kuwa mpole, akijua wazi kuwa ukimchekea nyani, utayavuna mabua.

Wengi bila shaka watakuwa wanajiuliza genge analolizungumza Rais Samia ni lipi? Kauli yake inajifafanua yenyewe hasa pale aliposema: “Mambo yale (ya hovyo, ya kifisadi) hayakufanyika ndani ya awamu ya sita, (bali) yalifanyika huko nyuma (ila) gari bovu linaangushiwa awamu ya sita.”

Je huko nyuma maana yake ni nini? Ni kipindi cha Rais wa kwanza Julius Nyerere au waliomfuatia Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete? Bila shaka walengwa wa kauli ni watu waliong’ara kipindi cha mtangulizi wake, John Magufuli.

Wote tunajua kuwa Magufuli alikuwa na ushawishi wa ajabu. Tunajua pia kuwa waliomuamini na kumpenda waliumia mno alipofariki. Lakini maumivu yameendelea zaidi baada ya kuingia Rais Samia madarakani kwa mujibu wa katiba, na kuanza kufanya mabadiliko makubwa, akigeuza karibu misingi yote ya mtangulizi.

Mmoja wa watu walioonekana kuidindia serikali ya Rais Samia kutoka chama tawala ni Humphrey Polepole, ambaye hivi karibuni amekuwa akitoa kauli nyingi tata zinazoashiria kuitukuza serikali iliyopita na kuiponda iliyopo.

Ukiichunguza vizuri kauli ya Rais Samia ni kama amejiweka mbali na hayo yaliyofanyika katika awamu iliyopita, akijua wazi kuwa alikuwa ni Makamu wa Rais. Tafsiri yangu ya kitendo hiki ni kuwa anakiri wazi, bila kusema moja kwa moja, kuwa kumbe kipindi chake cha umakamu alipuuzwa, hakushirikishwa na hivyo anakataa kubeba lawama ya yaliyotokea kipindi hicho.

Sio siri kuwa, hata kwa asili tu ya mwanadamu, wapenzi wa Magufuli hawawezi kumpenda Rais Samia, lakini mama naye kachoka kuwa mpole. Rais Samia kaamua kurejesha mashambulizi. Naamini hii movi haijaisha kabisa. Tutaona mengi zaidi huko mbele ya safari.

Je Rais ataweza kuwadhibiti maadui zake? Au wao ndio watamdhibiti, ikijulikana wazi kuwa sio watu dhaifudhaifu bali walikijenga na kujiimarisha kipindi hicho cha awamu ya tano.

Yetu macho!View attachment 2033644
Dawa dhidi ya wanaompinga ni kutekeleza haki na kweli.Hawatanfanya kitu huku watanzania tukiwatazama tu.Ila mama anaweza kuchafuliwa na swala la Mbw endepo alidanganywa.
 
JPM hakukopa trilioni 40 huo ni uzushi. Kokotoa kwanza deni la Mwinyi, Mkapa na Kikwete pamoja na riba zake kisha jumlisha kabla hujasema JPM alikopa kiasi gani.
Mpaka Mwalimu Julius K. Nyerere anang'atuka madarakani deni lilikuwa kiasi gani? tuanzie hapo.
 
Kuna makundi yanajua yanayofanya ndani ya serikali (makundi hayo yapo serikalini hawamu ya tano na sita) makundi hayo yanageuka na kusema mambo ya ovyo, kumbe wao ndio wa ovyo, mambo hayo yamefanyika nyuma wanakusudia gari bovu kuangushia hawamu ya sita, (huko nyuma ni hawamu ya tano, ambao sehemu yote ya serikali imeendelea hadi hawamu ya sita)
Mkuu ukiandika hakikisha unahariri (edit). Ni awamu sio hawamu.
 
Back
Top Bottom