Kauli ya Rais Samia iliwalenga wakina nani?

Ukijadili jambo huku unaongozwa na chuki huwezi kuuona ukweli. Hilo deni unalodai limeongezeka hadi trilli 70 kwani JPM alikuta deni likiwa zero? Awamu za Mwinyi, Mkapa na Kikwete madeni yao pamoja na riba umejumlisha na kutoa kabla ya kusema JPM amekopa ngapi? Umeoanisha na gharama za miradi aliyokopea hela ukaona hazitally?

Juzi hapa mmelalamika kutozwa kodi ya majengo kwa njia ya luku sh. 12,000 tu wakati hicho ni kiasi kidogo ambacho JPM ndiye aliyekishusha kutoka wastani wa elfu 30 kwa nyumba za mbavu za mbwa hadi laki tano na milioni zilizokuwa ndio kodi za majemgo kabla JPM hajaingia madarakani. Hata nafuu hiyo iliyoletwa na JPM huioni?

JPM ameacha marekebusho katika sekta ya madini ambapo sasa nchi inafaidika zaidi na mapato ya madini kuliko alivyokuta kutokana na mikataba mibovu aliyorithi.

Umeme wa Stiglers huko Rufiji aliamua kujenga baada ya kuona gesi sio yetu tena na ile mikataba kuipindua ni vigumu kwa jinsi ilivyosukwa hivyo badala ya kuendelea kuibiwa kwa kuuziwa gesi ya umeme kwa bei juu bora tuwe na chanzo chetu wenyewe cha bei nafuu na sasa wajanja wanataka kuturudisha huko wenye kutegemea umeme ghali wa gesi.

Kazi za JPM zitabakia classic katika nchi hii hata mfanyaje hamuwezi kupindua.
Uyo mwendazake hakuna tafuna maneno kalikoroga Taifa mpaka Basi,

Nakubali deni lingine kalikuta,ila aisee eti ndani ya miaka mitano tir 40, hivi pesa zote alikua anapeleka wapi maana hata miradi aliyoanzisha mikubwa ipo inamuumiza kichwa bi mkubwa, bora angemaliza reli tujue moja,au Bwawa na Nyerere tujue,
Ila tunashukuru katuachia uwanja wa chato,

Aliamin Tz anaweza kuifamya Dubei KWa wakati MMOJA, that miradi Mingi ipo nusu nusu,

Ila Bado naungana na Nape kukagua pesa izi na matumizi tir 40 nyingi sana
 
Hii kauli pana Sana , hata Wanaohusika kumbambikia KESI Mbowe wakae mguu pande, WENDA walimwingiza chaka ,Sasa anaukweli kwamba ni kamladi ka watu wachache serikalin ,

Jumba bovu lina maana nyingi Sana, ila alipo gusia ufisadi, hapa kwakweli anawalenga wote walio kuwa karibu na mwendazake, ni wapi, wanajijua na sisi tunawajua,

Maana hakuna kipindi Cha ufisadi mkubwa Kama Cha mwendazake, mpaka deni la taifa kaliacha na tir 70,

Wazee wa ma v8 mpooooo
Kiongozi mwenye busara anatakiwa kuongoza na kukubali mapungufu na kuyafanyia kazi bila kulalamika. Kama unakuta mapungufu au madudui basi yafanyie kazi bila kuingia jukwaani kuwa haya madudu ya leo yalikuwa ya fulani, hasa wakati ukijuwa huyo fulani hayupo duniani kujibu hayo. Hii tabia imeshamiri saana kwenye serekali ya SSH. Baada ya SSH kuanza kumlaumu Magufuli hadharani, imekuwa ni tabia na kawaida pia kwa mawaziri wake. Wakianza kushindwa kazi wanatoa lawama kwa Magufuli. Kama wanajuwa au walijuwa Magufuli aliharibu kwa nini wakubali kazi zilizokwisha haribika!

Watu wengi wanadai kuwa Magufuli alikuwa hampi nafasi SSH. Lakini itakuwa vizuri tukubaliane kuwa pamoja na makamu wa raisi kuwa namba mbili kwa uzito, lakini makamu wa raisi wote hawajawahi kuwa na umaarufu na nguvu yoyote. Siku zote hiki cheo kimekuwa cheo kisicho kazi maalumu, maana hata majukumu ya kila siku ya cheo hiki hayajulikani. Hata mawaziri walioyokuwa chini ya ofisi hii nao ni kama walikuwa hawana cha kufanya. Cheo cha waziri mkuu kinajulikana mna kazi zake zinajulikana.
 
Tumepata bahati nyingine ya kuwa na Rais mpole ,msikivu ,mvumilivu na mwenye utu kupitiliza......

Pamoja na yote hayo ,baadhi yetu watanzania(walioko chamani na serikalini) tuna tabia ya UNAFIKI NA UKOSEFU WA UTIIFU WA DHATI KWA VIONGOZI WETU WAKUBWA.....

Sambamba na hilo ,wako wasiompenda mh.Rais kwa ukosefu wa fikra pana za MUSTAKABALI WA TAIFA LETU PENDWA......

Miongoni mwao wamo humu:-

1)Waliokuwa na matarajio kuwa utawala wa awamu ya 5 usingehitimika vile....
2)Waliokosa teuzi mbalimbali

Kwa kuwa mh.Rais SSH ana kofia 3 kubwa;-
1)Amiri Jeshi wa Majeshi ya ulinzi na usalama
2)Chifu Mkuu wa machifu wote nchini
3)Mwenyekiti wa CCM taifa

Mh.Rais SSH asicheke na wanaotaka kumwangusha.....
Ebu rudia
Amesema HATOKUBALI HATOKUBALI HATOKUBALI....ashikilie hapohapo💪

Nchi ngumu hii
Nchi ngumu hii
Nchi ngumu hii
Nchi ngumu hii

Masalaam🙏

SIEMPRE JMT🙏
Ebu rudia tena! Maana ulichoandika ni utopolo mtupu!
 
Abuu Kauthar

View attachment 2033645

Mama kachefukwa kaamua atapike shombo. Nukuu yake imetembea mno mitandaoni kwa sababu moja tu: Inaashiria mambo si shwari huko serikalini na katika chama.

“Kuna makundi wanayajua wanayoyafanya ndani ya serikali ni makundi hayo hayo yanageuka kusema Serikali ya awamu ya sita ufisaidi umerudi, mambo yako hovyo, kumbe wao ndio wako hovyo.Na mambo yale hayakufanyika ndani ya awamu ya sita, yalifanyika huko nyuma gari bovu linaangushiwa awamu ya sita sitakubali. Niliapa kusimamia haki za wananchi, nitasimama nao,” alisema Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia alitoa kauli hiyo wakati wa hotuba yake katika hafla ya uzinduzi wa gati katika Bandari ya Dar es Salaam Jumamosi Desemba 4, 2021 ambapo alilionya kundi la watu serikalini linalofanya mambo ya hovyo ya kifisadi kisha wamainyooshewa kidole Serikali hii ya awamu ya sita.

Gazeti la Mwananchi liliandika katika habari yao ya tukio hili: Samia alionya genge linalotaka kuchafua Serikali yake.”

Hii maana yake nini?

Jambo moja lipo dhahiri. Hali si shwari ndani ya CCM. Mama ameanza kung’amua maadui zake na amechoka kuwa mpole, akijua wazi kuwa ukimchekea nyani, utayavuna mabua.

Wengi bila shaka watakuwa wanajiuliza genge analolizungumza Rais Samia ni lipi? Kauli yake inajifafanua yenyewe hasa pale aliposema: “Mambo yale (ya hovyo, ya kifisadi) hayakufanyika ndani ya awamu ya sita, (bali) yalifanyika huko nyuma (ila) gari bovu linaangushiwa awamu ya sita.”

Je huko nyuma maana yake ni nini? Ni kipindi cha Rais wa kwanza Julius Nyerere au waliomfuatia Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete? Bila shaka walengwa wa kauli ni watu waliong’ara kipindi cha mtangulizi wake, John Magufuli.

Wote tunajua kuwa Magufuli alikuwa na ushawishi wa ajabu. Tunajua pia kuwa waliomuamini na kumpenda waliumia mno alipofariki. Lakini maumivu yameendelea zaidi baada ya kuingia Rais Samia madarakani kwa mujibu wa katiba, na kuanza kufanya mabadiliko makubwa, akigeuza karibu misingi yote ya mtangulizi.

Mmoja wa watu walioonekana kuidindia serikali ya Rais Samia kutoka chama tawala ni Humphrey Polepole, ambaye hivi karibuni amekuwa akitoa kauli nyingi tata zinazoashiria kuitukuza serikali iliyopita na kuiponda iliyopo.

Ukiichunguza vizuri kauli ya Rais Samia ni kama amejiweka mbali na hayo yaliyofanyika katika awamu iliyopita, akijua wazi kuwa alikuwa ni Makamu wa Rais. Tafsiri yangu ya kitendo hiki ni kuwa anakiri wazi, bila kusema moja kwa moja, kuwa kumbe kipindi chake cha umakamu alipuuzwa, hakushirikishwa na hivyo anakataa kubeba lawama ya yaliyotokea kipindi hicho.

Sio siri kuwa, hata kwa asili tu ya mwanadamu, wapenzi wa Magufuli hawawezi kumpenda Rais Samia, lakini mama naye kachoka kuwa mpole. Rais Samia kaamua kurejesha mashambulizi. Naamini hii movi haijaisha kabisa. Tutaona mengi zaidi huko mbele ya safari.

Je Rais ataweza kuwadhibiti maadui zake? Au wao ndio watamdhibiti, ikijulikana wazi kuwa sio watu dhaifudhaifu bali walikijenga na kujiimarisha kipindi hicho cha awamu ya tano.

Yetu macho!View attachment 2033644
Kwani ni uongo, watu wake wanamdanganya wanawatoa waadilifu na kuweka wezi kwenye nafasi
 
Ukijadili jambo huku unaongozwa na chuki huwezi kuuona ukweli. Hilo deni unalodai limeongezeka hadi trilli 70 kwani JPM alikuta deni likiwa zero? Awamu za Mwinyi, Mkapa na Kikwete madeni yao pamoja na riba umejumlisha na kutoa kabla ya kusema JPM amekopa ngapi? Umeoanisha na gharama za miradi aliyokopea hela ukaona hazitally?

Juzi hapa mmelalamika kutozwa kodi ya majengo kwa njia ya luku sh. 12,000 tu wakati hicho ni kiasi kidogo ambacho JPM ndiye aliyekishusha kutoka wastani wa elfu 30 kwa nyumba za mbavu za mbwa hadi laki tano na milioni zilizokuwa ndio kodi za majemgo kabla JPM hajaingia madarakani. Hata nafuu hiyo iliyoletwa na JPM huioni?

JPM ameacha marekebusho katika sekta ya madini ambapo sasa nchi inafaidika zaidi na mapato ya madini kuliko alivyokuta kutokana na mikataba mibovu aliyorithi.

Umeme wa Stiglers huko Rufiji aliamua kujenga baada ya kuona gesi sio yetu tena na ile mikataba kuipindua ni vigumu kwa jinsi ilivyosukwa hivyo badala ya kuendelea kuibiwa kwa kuuziwa gesi ya umeme kwa bei juu bora tuwe na chanzo chetu wenyewe cha bei nafuu na sasa wajanja wanataka kuturudisha huko wenye kutegemea umeme ghali wa gesi.

Kazi za JPM zitabakia classic katika nchi hii hata mfanyaje hamuwezi kupindua.
Umewachambulia vizuri sana!
 
Mimi kila nikitafakari nakosa jibu ,kuwa huyu Pole pole mbona anajiamini Sana Ni akina Nani wamempa hiyo jeuri ya kuongea atakavyo? Maana kikawaida sidhan kama Ana nguvu hiyo ya kuongea kwa kujiamini kiasi hicho na asithibitiwe na kukemewa na yeyote yule.
Huyu mama amezungukwa na madui hapo ikulu yaan dizain wanamchora tu ,nadhan saiz kidogo akili imeanza kumkaa sawa kuwa hayuko na watu sahihi mwenye kuliongoza taifa zaidi tu wanamlia timing ili wapindue nanga.
Kuna watu Kama Katelephone ,mipango ya kazi ,na sabufa ya mjengo Nina waswas nao Sana kuwa ndio wanaomtafuna mama kimya kimya ,Hawa watu watatu naona Waz ndio mastermind wa kila kitu kwasasa ukijumrisha na mzee wa tozo ogopa Sana vile vichwa .
Muda utaongea Ila mama asipochukua hatua mapema na kujiimarisha mapema 2025 Hana chake watu wapo jikoni.
Nimechekeshwa kwa jinsi ulivyopangilia tuneno! Eti katerephone ahahahaha
 
Mimi namkumbusha moja tu; kwa kuwa yeye hakukubaliana na JPM japo alikaa kimya huku akimsigina kimyakimya ajue na yeye kuna watu wamemzunguka japo wanamsigina kama alivyofanya kwa JPM.

What goes around comes around! Kuanzia na namba mbili ajue kuwa hawako pamoja, namba tatu hawako naye, mawaziri kibao na wabunge wanamchora tu, ukiingia kwenye vyombo ndokabisaaa wana hasira naye balaa!

Namshauri aachane na ba moko akae na wapinzani aachane na kufyatuafyatua hovyo na kuinanga serikali iliyopita.

JPM sjui aliwaroga watu maana watu wengi wanaamini yule hakuwa MTU wa kawaida kumbe alikuwa mjanja tu!

Hata viongozi wa dini takribani zote nahisi kama hawako happy naye kabisa maana bwana yule aliwapa nafasi sana mpaka wakamlinganisha na Mungu ahahs
 
Na nilishangaa sana juzi anasema mtu yeyote atakaye thubutu kuhujumu mradi wa J.Nyerere awe makini sana na asithubutu kabisa maana hatutakubali..ahahahahah duh!
 
Hakutusikia tulimwambia mwanzoni aunde serikali yake aweke watu wake akutuelewa, nadhani sasa ameelewa.
Kuwa kiongozi hakumaanishi kujua KILA kitu.Mtazamaji mpira anauona mpira zaidi kuliko mchezaji uwanjani.
 
Si achukue hatua badala ya kulialia kama mtu asiye na authority na power mwenzake alikuja na safu yake ambayo alijua iko royal kwake yeye anashindwa nini ? Tatizo anataka kufanya mambo bila kumkera mtu kitu ambacho hakipo
 
Mimi namkumbusha moja tu; kwa kuwa yeye hakukubaliana na JPM japo alikaa kimya huku akimsigina kimyakimya ajue na yeye kuna watu wamemzunguka japo wanamsigina kama alivyofanya kwa JPM.

What goes around comes around! Kuanzia na namba mbili ajue kuwa hawako pamoja, namba tatu hawako naye, mawaziri kibao na wabunge wanamchora tu, ukiingia kwenye vyombo ndokabisaaa wana hasira naye balaa!

Namshauri aachane na ba moko akae na wapinzani aachane na kufyatuafyatua hovyo na kuinanga serikali iliyopita.

JPM sjui aliwaroga watu maana watu wengi wanaamini yule hakuwa MTU wa kawaida kumbe alikuwa mjanja tu!

Hata viongozi wa dini takribani zote nahisi kama hawako happy naye kabisa maana bwana yule aliwapa nafasi sana mpaka wakamlinganisha na Mungu ahahs
JPM hakuwaroga watu aliishi nao! Kitendo cha kuzunguka nchini asimama popote anawasikiliza, ni mbinu nzuri ya kuwasogeza watu karibu! Unawasikiliza shida zao, unawateka kisaikolojia,
Sasa wewe hata bango hutaki, unazunguka na ndege, angani utakutana na nani?
 
Ukijadili jambo huku unaongozwa na chuki huwezi kuuona ukweli. Hilo deni unalodai limeongezeka hadi trilli 70 kwani JPM alikuta deni likiwa zero? Awamu za Mwinyi, Mkapa na Kikwete madeni yao pamoja na riba umejumlisha na kutoa kabla ya kusema JPM amekopa ngapi? Umeoanisha na gharama za miradi aliyokopea hela ukaona hazitally?

Juzi hapa mmelalamika kutozwa kodi ya majengo kwa njia ya luku sh. 12,000 tu wakati hicho ni kiasi kidogo ambacho JPM ndiye aliyekishusha kutoka wastani wa elfu 30 kwa nyumba za mbavu za mbwa hadi laki tano na milioni zilizokuwa ndio kodi za majemgo kabla JPM hajaingia madarakani. Hata nafuu hiyo iliyoletwa na JPM huioni?

JPM ameacha marekebusho katika sekta ya madini ambapo sasa nchi inafaidika zaidi na mapato ya madini kuliko alivyokuta kutokana na mikataba mibovu aliyorithi.

Umeme wa Stiglers huko Rufiji aliamua kujenga baada ya kuona gesi sio yetu tena na ile mikataba kuipindua ni vigumu kwa jinsi ilivyosukwa hivyo badala ya kuendelea kuibiwa kwa kuuziwa gesi ya umeme kwa bei juu bora tuwe na chanzo chetu wenyewe cha bei nafuu na sasa wajanja wanataka kuturudisha huko wenye kutegemea umeme ghali wa gesi.

Kazi za JPM zitabakia classic katika nchi hii hata mfanyaje hamuwezi kupindua.

cash ya kununua ndege tunayo ,ila kulipa deni ni ziro
 
Katika uchumi huwezi kufanya vitu vyote ndio maana kuna mipango. Pili deni lina life span yake ya kulipa, tatizo ni pake tu unapodefault kulipa.
 
Uyo mwendazake hakuna tafuna maneno kalikoroga Taifa mpaka Basi,

Nakubali deni lingine kalikuta,ila aisee eti ndani ya miaka mitano tir 40, hivi pesa zote alikua anapeleka wapi maana hata miradi aliyoanzisha mikubwa ipo inamuumiza kichwa bi mkubwa, bora angemaliza reli tujue moja,au Bwawa na Nyerere tujue,
Ila tunashukuru katuachia uwanja wa chato,

Aliamin Tz anaweza kuifamya Dubei KWa wakati MMOJA, that miradi Mingi ipo nusu nusu,

Ila Bado naungana na Nape kukagua pesa izi na matumizi tir 40 nyingi sana
JPM hakukopa trilioni 40 huo ni uzushi. Kokotoa kwanza deni la Mwinyi, Mkapa na Kikwete pamoja na riba zake kisha jumlisha kabla hujasema JPM alikopa kiasi gani.
 
Katika uchumi huwezi kufanya vitu vyote ndio maana kuna mipango. Pili deni lina life span yake ya kulipa, tatizo ni pake tu unapodefault kulipa.

nenda kakope china !.naona utapata akili na kushindwa kutetea hayo
 
Mimi kila nikitafakari nakosa jibu ,kuwa huyu Pole pole mbona anajiamini Sana Ni akina Nani wamempa hiyo jeuri ya kuongea atakavyo? Maana kikawaida sidhan kama Ana nguvu hiyo ya kuongea kwa kujiamini kiasi hicho na asithibitiwe na kukemewa na yeyote yule.
Huyu mama amezungukwa na madui hapo ikulu yaan dizain wanamchora tu ,nadhan saiz kidogo akili imeanza kumkaa sawa kuwa hayuko na watu sahihi mwenye kuliongoza taifa zaidi tu wanamlia timing ili wapindue nanga.
Kuna watu Kama Katelephone ,mipango ya kazi ,na sabufa ya mjengo Nina waswas nao Sana kuwa ndio wanaomtafuna mama kimya kimya ,Hawa watu watatu naona Waz ndio mastermind wa kila kitu kwasasa ukijumrisha na mzee wa tozo ogopa Sana vile vichwa .
Muda utaongea Ila mama asipochukua hatua mapema na kujiimarisha mapema 2025 Hana chake watu wapo jikoni.
Nyie ni wapumbavu mbona kipindi kile tunalalamikia usalama wa magufuli ikulu adi kufika atua mbaya habari nyeti za ikulu zinavujishwa na kigogo mkawa mnachekelea na kumuona ni shujaa mpaka jpm umahuti unamkuta.wacha nayeye aisome number tunawasiwasi ukute ni huyu huyu mama ndo aliusika na kuumpa taarifa kigogo maana sasa tenga limekuwa ndoo mpya halivuji tena maji.
 
Hakutusikia tulimwambia mwanzoni aunde serikali yake aweke watu wake akutuelewa, nadhani sasa ameelewa.
Kuwa kiongozi hakumaanishi kujua KILA kitu.Mtazamaji mpira anauona mpira zaidi kuliko mchezaji uwanjani.
Unajua karma wewe? Ata kama angetengeneza serikali yaka akaweka ndugu zake wote Karma ingemrudia ,yeye alikaa na magufuli kinafiki na ata hao wangefanya the same.
 
Tanzania haijaanza na Kikwete ,wala Magufuli.....

Mbona mnapenda kujidanganya kiasi hicho na "kumtukuza" kiongozi mmoja tu ilihali taifa letu limebarikiwa VIONGOZI 6 hadi sasa?!!!

Kwa hiyo mh.Rais SSH akirekebisha pahala basi anakuwa alikaa kinafiki na hayati JPM?!!!😳😳

Kwa hiyo JPM naye alikaa kinafiki na mh.Kikwete ?!!!😳😳
 
Huu mzimu hautamuacha salama na bado atasema hadi msiyotarajia, time is the good teacher.
 
Back
Top Bottom