Kauli ya Rais ni sheria, kwanini hadi sasa wizara ya Afya haijatenga kalantini yenye wataalamu wa tiba asili?

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
622
1,000
Wote tumemsikia Rais akishauri na kusisitiza wizara ya afya iwasisitize watu zaidi matumizi ya tiba asili kama kujifukiza kwa wagonjwa wa corona. Taasisi ya Rais haiwezi kuongea bila kuwa na taarifa sahihi kutoka vyanzo vyake. Si hilo tu, kuna shirikisho au tuite umoja wa waganga wa tiba asili wanaotambulika na mamlaka hapa nchini.

Kwa vile kirusi cha korona hakina dawa na inasemekana kujifukiza na baadhi ya dawa asili zipo zinazoongeza kinga mwili kwa ajili ya kupambana na magonjwa ikiwemo corona, kwanini wizara ya Afya isitenge karantini maalumu ambayo hawa wataalamu wa tiba asili waliokwisha thibitishwa na mamlaka husika waende nao kuonyesha utaalamu wao kwa kuwasaidia waliopata changamoto ya korona

Imethibitika kwamba wagonjwa wakorona hospitali au kwenye vituo maalumu hakuna dawa mahususi wanayopewa ya kutibu corona zaidi ni kuwaangalia tu na kuwapa dawa za kutibu magonjwa nyemelezi mengine.

Wizara husika hawaoni kwamba hawa wataalamu wa tiba asili wanaweza kuwa msaada zaidi kwenye hizo kalantini na hawa madaktari ambao kimsingi hata hawatoshi wabaki kutibu wagonjwa wengine?

Nashauri hawa waliokwisha thibitishwa ambao sio janja janja wapelekwe kwenye hizo kalantini wakatoe huduma hata kama serikali haitawalipa wagonjwa wenyewe watajilipia maana tunajua namna serikali ya sasa inavyotolea macho kukusanya zaidi kuliko kutumia hata pale ambapo ni muhimu. Serikali nyingine dunia zinasamehe kodi na kutoa unafuu kwa watu wao ila hapa kwetu ndo kwanza TRA wanapita mtaani kusisitiza watu walipe kodi kwa wakati badala ya magari hayo kupita kuhimiza watu wajilinde dhidi ya korona

Madagascar wameshaanza, nasisi tufuate. Tamko la Rais kwamba watu waruhusiwe kujitibu kiasili tena akasema wizara isisitize zaidi hili linaweza kuleta madhara kwa watu wengi kama halitawekewa miongozo. Tunawafahamu watanzania wanavyojua kutumia fursa, kwa hili kuna makanjanja wengi wanaweza kuibuka na kughalimu maisha ya watu.
 
Robidinyo

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
2,117
2,000
Aliegharimu Maisha ya Watu ni Yule aliye hutubia Juzi Maana kaaribu kila kitu na Kavuruga Kila mtu.
 
Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
622
1,000
Aliegharimu Maisha ya Watu ni Yule aliye hutubia Juzi Maana kaaribu kila kitu na Kavuruga Kila mtu.
Yeye ametoa maelekezo kwa wizara husika wafanyie kazi. Wewe huamini kama tiba asili ipo inayoweza kusaidia katika hili janga?
 
Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,074
2,000
Yeye ametoa maelekezo kwa wizara husika wafanyie kazi. Wewe huamini kama tiba asili ipo inayoweza kusaidia katika hili janga?
Kipindi waganga wa tiba asilia wanatafuta dawa, vp wagonjwa watakuwa wanapata huduma gani?
 
Robidinyo

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
2,117
2,000
Yeye ametoa maelekezo kwa wizara husika wafanyie kazi. Wewe huamini kama tiba asili ipo inayoweza kusaidia katika hili janga?
Hajatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya bali kawaambia wananchi Wajifukize ili kuchoma futa, Mtaalam wa Afya ambae ni Naibu waziri alisema hiyo njia siyo sahii, ni Juu yako kumsikiliza Dr ambae na mtaalam wa Afya au kumsikiliza Mwana siasa aliyejificha kwao Kijijini
 
Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
622
1,000
Hajatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya bali kawaambia wananchi Wajifukize ili kuchoma futa, Mtaalam wa Afya ambae ni Naibu waziri alisema hiyo njia siyo sahii, ni Juu yako kumsikiliza Dr ambae na mtaalam wa Afya au kumsikiliza Mwana siasa aliyejificha kwao Kijijini
Naibu waziri yuko sahihi kwa Taaluma yake ya ki magharibi. Mwanasiasa anajua ameongea kwa malengo gani maana mwanasiasa yeye kitu kikubwa anasoma upepo.

Tuwaache hao wote tuongelee hawa wataalamu wa tiba asili waliosajiliwa. Wamepewa nafasi wakasema kwa tiba zao hawawezi kufanya lolote katika hili la korona?
 
Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
622
1,000
Kipindi waganga wa tiba asilia wanatafuta dawa, vp wagonjwa watakuwa wanapata huduma gani?
Kwani wanapopelekwa huko hospitali wanapata huduma gani? Naamini hawa wataalamu wa tiba asili wanaouwezo wa kutoa hizo huduma za kutibu dalili vizuri kuliko hata huduma wanazopata hospitali.
 
Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,074
2,000
Unaamini ila huna uhakika
Kwani wanapopelekwa huko hospitali wanapata huduma gani? Naamini hawa wataalamu wa tiba asili wanaouwezo wa kutoa hizo huduma za kutibu dalili vizuri kuliko hata huduma wanazopata hospitali.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom