Kauli ya Rais Magufuli ya 'Watu Kuishi kama mashetani' inahalalisha maovu

"Kuna watu nchi hii wanaishi kama malaika nawaahidi nitawashusha wote waishi kama mashetani"

Nimenukuu tu msiniite mchochezi na huko ndipo tunaelekea tutaanza kupata mlo mmoja kwa siku na maji safi na huduma bora itakuwa anasa
Alikuwa anatania tu
 
Umamuuliza nani ili swali.. Maswali ya kijinga jinga kwanini hasipende watu waishi vizuri na ndio maana anahakikisha amani iwepo ili watu waishi vizuri zaidi..

Alishasema wapiga dili, wezi, wauza madawa.. Mafisadi hatokua na HURUMA nao.. Ila wafanya biashara wazalendo wataishi vizuri na Biashara zao zitakua mzuri.. Naomba ujaribu kua unampa ushauri Mbowe..
www.povu@lumumba.org
 
Umamuuliza nani ili swali.. Maswali ya kijinga jinga kwanini hasipende watu waishi vizuri na ndio maana anahakikisha amani iwepo ili watu waishi vizuri zaidi..

Alishasema wapiga dili, wezi, wauza madawa.. Mafisadi hatokua na HURUMA nao.. Ila wafanya biashara wazalendo wataishi vizuri na Biashara zao zitakua mzuri.. Naomba ujaribu kua unampa ushauri Mbowe..
Mbowe bana yaani Chadema watajuta sana.
Hashauriki popote
 
Muishi kama mashetani hiyo ni furaha yake kuu yaani akiona hivyo mpaka moyo wake unacheza kwasakwasa.
Nimeyakomeshaga !!!

No vision.
Primitivity.
Malezi mabaya ya utotoni.
.
.
.
.
Wewe unajpenda kweli? Hayo maneno shauri yako
 
Umamuuliza nani ili swali.. Maswali ya kijinga jinga kwanini hasipende watu waishi vizuri na ndio maana anahakikisha amani iwepo ili watu waishi vizuri zaidi..

Alishasema wapiga dili, wezi, wauza madawa.. Mafisadi hatokua na HURUMA nao.. Ila wafanya biashara wazalendo wataishi vizuri na Biashara zao zitakua mzuri.. Naomba ujaribu kua unampa ushauri Mbowe..
Mbowe katokea wapi tena?
 
Hivi mheshimiwa fulani anapenda kweli kuona watu kwa kutumia vipata vyao halali wamailiki nyumba nzuri na za kisasa, watu wanamiliki magari mazuri, anapenda kuona vitega uchumi vya watu vikistawi na anapenda kuona watu wanalipwa mishahara mizuri?

Hivi akikuona unamiliki kigari chako kimoja na kajumba kako alafu unadai nyongeza ya mshahara kweli anakuelewa?

Hivi akikuona unapanda ndege badala ya basi kwenda likizo kijijini kwako kujipumzisha moyoni mwake atakuwa anakufurahia au anakuona tu mpenda anasa?

Alafu ukiwa masikini sana anakuelewa?Hakuoni kama hujishughulishi kwa kutofanya kazi bali umekaa tu?Hatamani kukutolea uvivu kwa hasira maana haamini umeshindwa kujikwaamua?Hatamani hata kukufukuza machoni pake?

Je,si kweli haamini katika utajiri(kila tajiri kwake si mtu muadilifu) na je, si pia haamini katika umasikini (anaamini umasikini ni matokeo ya kutofanya kazi tu)?

Mtu wa aina hii unaweza kweli kum-define?

Nimewaza sana mpaka nikajikuta najiuliza haya maswali maana hivi ndivyo navyoweza kumtamfsiri mh huyu katika jimbo langu.
Fasihi yako imeeleweka
Kama umepata kwa jasho lako,hakuna atakaekugusa
Fanya kazi ule kivulini
 
kwanza kabisa natengua kauli ya kuishi kama Mashetani na natengua kauli ya kuishi kimasikini kwa dam ya YESU. Amen. Nimeona nitengue kauli hii kwakuwa imeanza kuleta matokeo yanayoendana kwa watu wengi. Wote wasio taka kuwa affected na kauli hii njooni hapa tuivunje kwa taifa zima na tulikabidhi taifa kwa Mungu Wa Israel.
 
shindwa roho ya kuishi kama mashetani nakataa roho ya umaskini sijazaliwa ili niwe maskini na kuishi kama shetani, nimezaliwa niwe tajiri na niishi kama malaika huo ndo mpango wa Mungu kunileta hapa duniani. Kwa hiyo natamka ww pepo uchwara shindwa kwa jina la Yesu. Amen
 
"Kuna watu wanaishi kama malaika, ni lazima tuwashushe waishi kama shetani" Rais John Pombe Joseph Magufuli, Machi 2016.

Wote tunajua kuwa kuishi kama malaika ni kuishi maisha mazuri, tulivu yenye amani, furaha, raha na bila dhambi yaani utakatifu wa kimungu. Na kuishi kama shetani ni kuishi ndani ya shida, maovu na dhambi za kila aina kama uongo, wizi, uzinzi, tamaa, utapeli, ufisadi, rushwa, dhiki, magonjwa, mabalaa na kila aina ya mabaya.

Unapokuwa kiongozi, hasa kiongozi mkuu wa nchi inakubidi uchunge sana kauli zako, kwani zinaweza kupoteza maana halisi na kuleta mkanganyiko.
biblia inasema kimtokacho MTU ndo kiujazacho moyo wake, na maneno huumba, kwa kauli hizi za mtukufu ni rahisi sana kwa wanatheologia kumjua ni MTU wa aina gani
 
biblia inasema kimtokacho MTU ndo kiujazacho moyo wake, na maneno huumba, kwa kauli hizi za mtukufu ni rahisi sana kwa wanatheologia kumjua ni MTU wa aina gani
Hapendi kuona mtu akifanikiwa na kumzidi. Ana leverage behaviour, yaani tabia ya kutaka kulinganisha watu, hata kama uwezo wao ni tofauti.
 
Shetani ni kiumbe kilicholaaniwa na Mwenyezi Mungu Je nasisi watanzania tulaaniwe?
 
Uruga ruga utamponza,tatizo la watu wengi walio zaliwa na kukulia bara na kuishi uko muda mrefu ni kushindwa kujua na kuimudu kazi nzima ya kucheza na maneno!jk alikuwa ******,ila alijua kucheza na maneno!magufuli anaitaji trimming ya hali ya juu,na sipati picha hapo ameenda kuhutubia U.N,na ile lafudhi yake,halafu autoe mfano kama huo...dah,sijui watz tuta ziweka wapi sura zetu
duh! eti "trimming"
 
Wanafunzi wataishi kama mashetani ndio maana yake baba asante
Kati ya Wanafunzi 60,000+ walioomba Mikopo ya Elimu ya Juu, ni wanafunzi wasiozidi 12,000 ndio waliofanikiwa kupata Mikopo hiyo. Hii ni aibu hasa ukizingatia ni moja ya Ahadi za Urais, kuhakikisha wanafunzi wanapata Mikopo.
 
NATAFUTA SABABU ZA KWANINI JPM ANATAKA MATAJIRI WAISHI KAMA MASHETANI.
Raisi wetu mpendwa Mh John Pombe Magufuli anatamani sana kuona maskini walio wengi wanaishi kama matajiri na wale Matajiri waishi kama maskini. Hii ina maana hata wale waliowekeza juhudi,Nguvu na hata maarifa yao kujiajiri ni lazima wajengewe mazingira ya kufirisika wawe wanataka au hawataki ili tu waweze kuishi maisha wanayoishi watanzania wengine. Hali kama anayoitaka ilikuwepo kipindi cha zama za mawe za kati hata kabla moto haujagunduliwa, Naona kuna kila jitihada za zama hizo kujirudia kwenye kizazi cha teknolojia ya habari na mawasiliano. Kwanini matajiri wakosolewe kiasi hicho? Kuna kosa gani matajiri wamelifanyia taifa mpaka waundiwe zengwe la kufirisika? Kama watafirisika mpaka sumuni ya mwisho Tanzania itafaidika na nini? Hivi mheshimiwa raisi anajua ni kwa kiasi gani hawa matajiri au Mabepari wanaendesha uchumi wa nchi?. Unapozungumzia matajiri wakubwa (Capitalists) unazungumzia watu ambao wanatumia vipaji vya watu na hata muda wa watu ili kutengeneza ukwasi wa kutosha. Na siku zote hawa ndio wenye uwezo wa kutikisa uchumi wa Tanzania na hata uchumi wa nchi zinazotuzunguka unaweza kuathirika pia. Ni hawa hawa matajiri ambao wanatoa financial facilities zinazotengeza ajira za kutosha, Zinazozalisha biashara za watu na hata wawekezaji wengine hua wanatokana na hawa matajiri. Watu wengi wanakua impacted na uchumi wa mabepari na hivyo kupelekea uchumi wa mtu mmoja mmoja (Microeconomics) na hata uchumi mkubwa wa taifa(Macroeconomics) kuinuka.JPM hawataki Matajiri pasi na kujua kwamba hawa ndio wanaosababisha kutengenezwa kwa idadi kubwa ya matajiri na hata kuinua ustawi wa watu. Umaskini sio sifa wala sio cheo cha kusema utasimama hadharani na kujisifia. Miongoni mwa maadui ambao Baba wa Taifa Mwl Julius K Nyerere aliwakemea kwa nguvu zote ni huu Umaskini lakini miaka zaidi ya 50 bado kuna mtu anasimama hadharani na kutaka watu waishi kimaskini. Mheshiwa atambue kwamba ulimwengu mzima tunaishi na uchumi unaotegemeana (Interdependent economy). Tafsiri yake ni kwamba ili yule mtu maskini aondokane na umaskini wake ni lazima watu wenye kipato kikubwa zaidi yake wawepo ili kumuinua nae aishi kama wao. Sasa kama Mheshimiwa anatamani matajiri waishi kimaskini ni nani atawainua hawa maskini ambao yeye anataka waishi kitajiri? . Bado natafuta sababu za kwanini Mheshimiwa anachukizwa na uwepo wa matajiri.
 
Maskini kwa kawaida huchukia wanapowaona watu wenye ukwasi.Na huwa wanatamani matajiri wafirisike ili wawe sawa.Hii fikra haina tofauti na uchawi.Kwa bahati mbaya wanasiasa uchwara hupenda kuwaaminisha maskini kwamba umaskini wao unatokana na kunyonywa na matajiri, ambao hupewa majina tofauti kwa nyakati tofauti.Kwenye azimio la Arusha waliitwa makabaila,wanyonyaji,Kupe nk.Kwa hiyo maskini hujisikia faraja ya Kisaikolojia kwamba mambo yatakuwa mazuri,pindi matajiri wakiwa mfirisi.Njia sahihi ingekuwa kuwapa mbinu maskini jinsi ya Kufanya kazi kwa bidii na weredi,ili waondokane na umaskini!!
 
Back
Top Bottom