Kauli ya Rais Magufuli mjini Mwanza, "walionipa kura msiwabomoleshe!" Je ukimya wa CCM unatupa picha gani Watanzania?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757

Chama tawala CCM kimehusishwa katika uamuzi wa Rais John Pombe Magufuli wa kusitisha bomoa bomoa mjini Mwanza.

Sababu ya kwanza iliyotolewa ni kwamba wahusika pamoja na kukiuka sheria walimpa kura na kumpa Urais hivyo wasibomoleshwe!

Sababu ya pili ni kwamba serikali ya Magufuli ina huruma hivyo isichukue maamuzi yatakayowaumiza hao wananchi.

Sababu ya tatu ni kwamba chama cha CCM ina "human face" na kwamba CCM ndicho chama pekee chenye human face.

Maswali: Kama Wananchi, tuutafsirije huu ukimya wa CCM? Je uamuzi huu wa serikali una baraka za CCM? Je hii huruma ni kwa watu waliompa Urais peke yao? Je hiyo human face haipo kwa walimnyima kura?
 
Ni aibu kwa kweli, ina maana waliobomolewa Maeneo ya Kimara, Mbezi, Kibamba wote walimnyima kura?, hivi kweli unaweza kuendesha nchi kwa kuwagawa watu kiasi hichi?
Makonda kugushi vyeti ni sawa, wengine wanafutwa kazi
Mwanza kujenga kwenye reserve ya barbara sawa, Kwingine Bomoa

Sipati picha Lukuvi alivyovimba, maana nyumba yake aliivunja mwenyewe kwa mkono wake
 
sasa wewe utampendaje mtu asiekupenda?......Arusha na Moshi wanajulikana kwa kuichukia CCM huwezi peleka maendeleo sehemu usiyotakiwa....CHARITY BEGINS AT HOME...........Mpende akupendae
 
Ndio maana wachaga kila

Kimara mbunge wao ni Kubenea ina maana walichagua CHADEMA
 
Hivi anaposema sijui wao ndo wana human face, wengine wana monkey face au?

Halafu anaposema ccm kina human face, ana maanisha kitu gani? Kwamba ndo chama chenye ubinadamu? If so aache utani kabisa!

Ama alipozungumzia human face, kwamba wao ccm ndo wanayo na vyama vingine havina, je ni kuhusu uongozi? Anajaribu kusema viongozi wa vyama vingine hawana ubinadamu bali wa ccm?

Au alikuwa na maana nyingine kabisa lakini akakosa maneno ya kuwakilisha? Dah!
 
LAKI si pesa, hebu tumia akili kidogo...Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50, Magufuli alipata kura milioni 8 sawa na asilimia 16% ya Watanzania kwa ujumla wao. Hilo moja lakini la pili ni je wanaolipa kodi ni wale waliompigia kura peke yao?

Kwa nini kodi zao akusanye lakini asiwajibike kwao, Urais hauendi hivyo. Kwa kauli yake hiyo ya hovyo na ya kijinga nilitegemea chama chake kitoe kauli ya kumkemea, kumuonya na kumpa somo kuhusu uendeshaji wa nchi.
 
huwezi kumpa chakula mtoto wa jirani wakatinaa mwanao ana njaa,,,,,,utaanza kwanza na mtoto wako.........waacheni.wana mwanza wakishashiba atakuja huko kwingine
a
 
Kama unasema hizo ndizo akili za Rais Magufuli, yawezekana unaamini unamtetea kumbe ndio unambomoa kwa sababu ni kama vile unasema hatuna Rais tunaye punguani.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
LAKI si pesa, hebu tumia akili kidogo...Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50, Magufuli alipata kura milioni 8 sawa na asilimia 16% ya Watanzania kwa ujumla wao. Hilo moja lakini la pili ni je wanaolipa kodi ni wale waliompigia kura peke yao?

Kwa nini kodi zao akusanye lakini asiwajibike kwao, Urais hauendi hivyo. Kwa kauli yake hiyo ya hovyo na ya kijinga nilitegemea chama chake kitoe kauli ya kumkemea, kumuonya na kumpa somo kuhusu uendeshaji wa nchi.
Ha ha ha mkuu nani wa kumkemea na kumuonya wakati yeye ndio Top? watu wanazipenda ajira zao mtu mwenyewe ndio kama hivyo akiamua Dar tusilale na umeme basi na umeme utazimwa.
 
sasa wewe utampendaje mtu asiekupenda?......Arusha na Moshi wanajulikana kwa kuichukia CCM huwezi peleka maendeleo sehemu usiyotakiwa....CHARITY BEGINS AT HOME...........Mpende akupendae
Kwanini mnachukua kodi kwenye mikoa ya watu wasiowapenda?

Chukueni kodi ya huko wanakowapenda muendeshee nchi tuone kama mna ubavu huo.
 
Hivi anaposema sijui wao ndo wana human face, wengine wana monkey face au?

Halafu anaposema ccm kina human face, ana maanisha kitu gani? Kwamba ndo chama chenye ubinadamu? If so aache utani kabisa!

Ama alipozungumzia human face, kwamba wao ccm ndo wanayo na vyama vingine havina, je ni kuhusu uongozi? Anajaribu kusema viongozi wa vyama vingine hawana ubinadamu bali wa ccm?

Au alikuwa na maana nyingine kabisa lakini akakosa maneno ya kuwakilisha? Dah!
Human face=Sura ya kibinadamu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom