Kauli ya Rais Magufuli kuhusu ugunduzi mpya wa gesi aina ya Helium nchini

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Habari wanaJF,

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameandika kupitia ukurasa wa wake wa Twitter kuhusu ugunduzi wa gesi ya Helium (He) na kutoa wito kwa wanasheria, wachumi na wataanzania wote.

Nukuu za Rais Magufuli hizi hapa;


Tunamshukuru Mungu Tanzania tumegundua gesi aina ya Helium(He),wito wangu kwa wachumi,wanasheria na watanzania wote kwa ujumla tujipange.
fgfgdh.png


Ugunduzi huu utuelekeze kujipanga hasa ktk eneo la mikataba yetu ili rasilimali hii adimu isaidie kuujenga uchumi wetu.

Screenshot from 2016-06-29 15:26:07.png

 
Hakika Mungu ameikumbuka Tanzania.....tupo na kwa jinsi yeyote ile hakuna wakutuzulumu tena. The old is gone tazama tumetengenezewa mwanzo mpya.....Mungu akiwa upande wetu nani atakuwa kinyume chetu? Kwa hakika Tanzania njema is a must project
 
Hivi UDSM mbona wanatuaibisha sana atoke mzungu Ulaya huko anagundua gesi maproffesor wetu wa UDSM wapo wapo tu kazi yao kubwa ni kudesa tu na kukariri vitabu vilivyopitwa na wakati...Ugunduzi.Utafiti ni Zero kabisa..SHAME ON THEM UDSM
 
Tanzania tumegundua gesi ya Helium au gesi ya Helium imegunduliwa Tanzania?

Either case, nadhani ni muhimu wahusika wote kuhakikisha hizi raslimali ambazo kila uchao tunasikia zimegunduliwa nchini kwetu kama mafuta, gesi asilia na sasa gesi hii adimu na adhimu sana; pamoja na raslimali nyinginezo asilia kama madini, mbuga za wanyama, misitu, nk zitumike kuliondoa taifa hili katika umaskini uliotopea. Imetosha sasa sisi kuwa chanzo cha utajiri kwa mataifa mengine huku wenyewe tukisalia kuwa maskini ombaomba.
 
Inabidi serikali itafute consultant kutoka nchi ya nje ambaye amebobea kwenye kuandika mikataba ya aina hii. Wanasheria wetu wengi wametuangusha sana kwenye mikataba waliyo andika miaka ya nyuma na sithani watabadilika sasa.
 
Hivi UDSM mbona wanatuaibisha sana atoke mzungu Ulaya huko anagundua gesi maproffesor wetu wa UDSM wapo wapo tu kazi yao kubwa ni kudesa tu na kukariri vitabu vilivyopitwa na wakati...Ugunduzi.Utafiti ni Zero kabisa..SHAME ON THEM UDSM

Hivi unafikiri hiyo gesi inapatikana kama mchanga ambao kila mtu anaweza kuiona? Inahitaji kuwekeza tena wakati mwingine bila kuwa na mategemeo ya muda mfupi. Prof. wa udsm hawezi kugundua hiyo gesi:

1) bila kuwa na research fund on a specific project (national research priorities).

2) Kuwa na research fund pekee haitoshi lazima kuwepo na mazingira rafiki (vifaa na watu wakukusaidia unapofanya hizo kazi) sasa wabongo wengi walizoea short-cuts huwezi kumpeleka porini kwa TZS 50k per day.

3) Lazima kuwepo na watu ambao ni motivated na hakuna kumuingilia with politics when excuting his/her duties. Inapotokea mwizi anaonekana wa maana na anashingiliwa kwenye jamii kama shujaa ujue sustainability ya hiyo jamii ni negative na ndiyo tulipokuwa tumefikia.

But trust me, tunaelekea kwenyewe kule ambapo bila kuwa na akili za kipekee...utatamani ardhi ikumeze.
 
Wachumi, wanasheria wanatakiwa kujipanga kwa elimu kwny sector hii na wa kuwezesha hili ni serikali yenyewe. Kama kweli mheshimiwa rais anamaanisha kwa vitendo hiyo kauli yake basi serikali kuanzia mwaka ujao wa fedha watoe ufadhili wa kozi fupi na ndefu nje ya nchi kwny mataifa yenye utaalamu wa gesi. Kozi hizo ziwe za upande wa kitaalamu wa masuala hayo ya gesi na upande mwingine ujasiriamali na fursa zitokanazo na malighafi hizo. Kwa kufanya hayo basi walau itakuwa ni hatua kwa vitendo katika kujiandaa kuvuna utajiri huu sisi wenyewe kushirikiana na wataalamu wa kigeni. Ahsante.
 
Huge Helium Gas Field Found in Africa Is a ‘Game Changer’

June 28, 2016
62e0e97b0df64e210d248b44db8c43f0

There is currently a global shortage of helium
(JOHANNESBURG) — The discovery of a huge helium gas field in East Africa is a “game changer for the future security of society’s helium needs” amid a global shortage, researchers in Britain said Tuesday.

The discovery in Tanzania is the result of a new exploration approach for the precious gas that is essential to spacecraft, MRI scanners, nuclear energy, according to the Oxford University statement. Helium also fills party balloons.

This is the first time helium has been found intentionally, said the statement. Until now, the gas has been found in small amounts accidentally during oil and gas drilling.

Independent experts have estimated the helium discovery is about 54 billion cubic feet, Oxford professor Chris Ballentine said.

“To put this discovery into perspective, global consumption of helium is about 8 BCf per year,” he said in the statement. “This is a game changer for the future security of society’s helium needs, and similar finds in the future may not be far away.”

Researchers found that the intense volcanic heat in Tanzania’s East African Rift Valley has released helium from ancient rocks and trapped it in shallow gas fields, the statement said. The researchers worked with Norway-based exploration company Helium One.

The new approach can be used to find helium resources in other parts of the world with similar geological history, Oxford researcher Pete Barry said in the statement.

“This is badly needed given the current demand for helium,” he said.

Oxford tweeted a photo of some of the low-tech components used in the exploration, including a roll of duct tape and plastic piping propped on a stick in what looks like a shallow pond.

“It may not look like much, but it helped find enough helium for 1.2 million medical MRI scanners,” the tweet said.
 
Hakika Mungu ameikumbuka Tanzania.....tupo na kwa jinsi yeyote ile hakuna wakutuzulumu tena. The old is gone tazama tumetengenezewa mwanzo mpya.....Mungu akiwa upande wetu nani atakuwa kinyume chetu? Kwa hakika Tanzania njema is a must project
kutegemea Tanzania njema kwa gesi hii ni ndoto maana lundo la rasilimali ambazo tunazo tayari linatosha kutufanya tuwe Uswizi au hata USA. Kabla ya kusubiri mikataba mipya ni kwa nini tusifanya amendment kwa hii mibovu!?
Kikubwa hapa ni akili na sio asilimali, mbali na hapo tutakuwa na rasilimali nyingi lakini zitavumbuliwa na wenye akili kama hii na mwisho ndio watanufaika wao, kwa nini hujiulizi tulikuwa wapi mpaka tusijue uwepo wa hii gesi!
 
Hizi natural resources siku hizi zingagunduliwa kila kukicha duniani kote. Huwa kuna kipindi kitafika wa kumuuzia itakuwa kazi.
Mfano wakati Israel wamegundua Gesi na Mafuta wakifikilia soko litakuwa Egypy, Egypt wakagundua katika mediteranian sea gesi nyingi ya kihistoria. HIvi vinavyowezekana kwa sasa tuvifanye kwa nguvu zote.
 
Hivi UDSM mbona wanatuaibisha sana atoke mzungu Ulaya huko anagundua gesi maproffesor wetu wa UDSM wapo wapo tu kazi yao kubwa ni kudesa tu na kukariri vitabu vilivyopitwa na wakati...Ugunduzi.Utafiti ni Zero kabisa..SHAME ON THEM UDSM
Ndugu yangu hata mlima kilimanjaro,tunaambiwa
uligunduliwa na mzungu wakati wachagga wapo pale toka
kuumbwa kwa ulimwengu.
Nadhani uliowataja watajitetea kuwa hawana mtaji.
kama wamachinga wanavyojieleza kukosa mtaji.
 
Hivi UDSM mbona wanatuaibisha sana atoke mzungu Ulaya huko anagundua gesi maproffesor wetu wa UDSM wapo wapo tu kazi yao kubwa ni kudesa tu na kukariri vitabu vilivyopitwa na wakati...Ugunduzi.Utafiti ni Zero kabisa..SHAME ON THEM UDSM
Madini mengi yanayo gunduliwa tanzania mfano haya ya Vito wanayoyagundua ni Samara mbao misituni Na wafugaji wakati mwingine wakulimaaaaa.....
Hawo wanaojifanyaga wataalam wa madini wao kazi Yako kushinda maofisini ya matumboo Yao makubwaaa tu
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom