Kauli ya Rais Kikwete juu ya milipuko ya Mabomu Gongo la Mboto

mi nilitaka na yeye alipukiwe ana bomu wakati akiwa Gongo la Mboto ili ayaonje machungu. waathirika wa mabomu Mbagala wapo amabo hawajalipwa mpaka leo, wa Gongo la mboto nao wajue tu kuwa wameshapigwa siasa hakuna cha fidia wala kifuta machozi kama mimi Muongo si tutaona.
 
Msemaji mmoja wa Jeshi jana alisema kwanini mnayaona mabaya ya Jeshi tu hamuangalii na mazuri? hamkumbuki wanajeshi wetu walivyo jenga daraja kule kilombero kwa muda mfupu mpaka wananchi waka wachinjia mbuzi? nilitamani nipate simu nimpigie yule jamaa.... yani yeye kaweza kulinganisha ujenzi wa daraja na majanga haya ya mbagala na gongo la mboto na ujenzi wa daraja??? embu wasinge jenga daraja kama kigezo ndo hicho cha wao kuacha tuuuu mabomu yalipuke kila kukicha, mi kwanza sidhani kama hawa watu wetu ni thaaaaaat much compitent mtanisamehee, hivi hapa Dar es salaam mnajua kuna makambi mangapi???? kila kona kambi, upanga kambi, mwenge kambi, mbagala, masaki karibu na sea cliff, lugalo, temeke, AH!!! mengine mtamalizia wenyewe na si hajabu kote huko mabomu yamesha expire nayo yanasubiri joto liongozeke yalipuke!!! hapo sasa watanzania wenzangu uhsusani wale ambao nao wakisikia milio kama hiyo wanakimbilia kuona, kama ulivyo lipuka ubalozi wa USA.....!!!!!!!!! weweeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!
 
Jambo moja kubwa ambalo mi linaniumiza kichwa ni kutokuwajibika kwa kiongozi yoyote yule!!! na ndo mana mimi mpaka leo pamoja na Mabaya yake Hayati Mwl, J. K. Nyerere alikiri kukosea ingawa sikuwahi kusikia akisema mnisamehe nafsini mwangu nilimsamehe, kwani alikiri kukosea katika uongozi wake na alisema hakuwa na experience yoyote katika uongozi ule, Abaki salama huko aliko, sasa hawa wakwetu, hivi unajua ukiachia Lowasa ambaye leo hii hata ukienda kumu uliza je unafikiri uliachia ngazi kwa haki au la??? anaweza kusema HAPANA???? kama Rais Kikwete ni muungwana mi naona angeachia ngazi tu kwa niaba ya wale wooooote chini yake wanao kosea kwani hakuwahi kumuwajibisha mtu katika uongozi wake.
 
Colleagues,

Nilitegemea azimio No. 15 kuwa hili hapa:

Kwa kuwa tukio hili la mlipuko wa Mabomu Gongo La Mboto limetokea si muda mlefu na lile la Mbagala; Baraza la Usalama la Taifa limeazimia kuchukua hatua kali za uwajibikaji kwa Viongozi wafuatao (1) Waziri wa ulinzi (2) Mkuu wa majeshi....ilikupisha uchunguzi huru wa matukio hayo.


Na kwakuwa hakuna tamko hilo hapo juu, maoni yangu nikuwa hakuna dhamira ya dhati ya kuhakikisha tukio kama hilo linakuwa la mwisho hapa Tanzania. Pili, Viongozi serikalini wameamua sasa kufanya watakavyo na hakuna wakumwajibisha mwenzake. Hii ni hatari sana kwa sana kwa amani na maendeleo ya Taifa. Bunge (kwa spika) mambo hayaendi kama tunavyotaka; Serilikalini (Kwa kikwete) mambo ndo hivyo na Mahakamani (Kwa Othman) Mpaka mamilion ya fedha ku-file kesi za uchaguzi!
 
Kilicho muhimu kwake ni kikosi cha jeshi na si waathirika wa mabomu...... OK..... we shall see...

Ni kweli Mkuu kwani kwenye kauli ya Baraza la Usalama la Taifa aliyoitoa ameipongeza JWTZ mara mbili - kwa kuondoa mabomu yalipodondokea na kuzima moto - Yote hayo ni mambo waliyopaswa kufanya baada ya uzembe wao wa kutochukua tahadhari ili watu wasio na hatia wasife kwa mlipuko wa mabomu. Inasikitisha kuwa hakuna kauli ya kusema kuwa uchunguzi wa kina utafanywa na hatua zitachukuliwa kwa watakaogundulika kusababisha nchi ipate msiba huu mkubwa kwa kutochukua tahadhari mlipuko usitokee. Ilichofanya kamati hiyo ya hatari (siyo ya usalama) ni kama kumpongeza aliyekojoa chumbani kwa kupiga deki chumba hicho baada ya mkojo wake kusababisha mtu mwingine ateleze, aangukie kisogo na kufa. Pongezi za nini kwa kikojozi huyo aliyedeki mkojo wake baada ya mkojo huo kusababisha kifo cha mwingine asiye na hatia? Ingekuwa busara kama kusingekuwa na kauli zozote za pongezi kwenye msiba huu mkubwa hasa ikizingatiwa hao wanaopongezwa ndiyo chanzo cha msiba huo na hawakusaidia chochote kwa walioathirika licha ya kuwa na hospitali kubwa ya Lugalo yenye wataalam wa hali ya juu,magari ya kuwasaidia waathirika yakiwemo ambulance,chakula cha msaada na kadhalika.Wapo baridiiiii kama hawahusiki huku wakipokea pongezi kwa baya walilofanya!
 
Back
Top Bottom