Kauli ya Rais juu ya fao la kujitoa ilivyonifurahisha kisha ikanitesa, inanitesa na itaendelea kunitesa

Nateswa na kauli ya rais kwa sababu watendaji wa NSSF wanadai ilikuwa ni siasa tu za majukwaani wao hawatoi hela wala hawajaagizwa kutoa. Nadhani kuteswa na kauli ya rais ni sawasawa na kuteswa na rais, hivyo Rais ananitesa.
Kauli ya rais ilihusu kurefushwa muda wa kuanza matumizi ya kikokotoo kipya
 
Utangulizi: Mkataba wangu wa kazi ulifikia ukomo tangu tarehe 31/12/2017. Sikuwa nimejiandaa sana juu ya ukomo wa kuendelea na kazi kwani kampuni niliyokuwa nikiifanyia kazi ilikuwa na utaratibu wa kutupatia mkataba wa muda wa mwaka mmoja na kila ulipoisha tulipewa mkataba mwingine, mwaka huo wa 2017 mambo yakawa kinyume na matarajio kwani kampuni ililazimika kupunguza wafanyakazi, mimi ni miongoni mwa wafanyakazi 16 ambao hatukupewa mkataba kwa mwaka 2018.

Niliamua kutumia pesa yangu kidogo iliyokuwa benki kuanzisha biashara ambayo haikufanya vizuri kulingana na matumizi ya kifamilia (ada za watoto shule,matibabu, chakula na kodi ya nyumba) kuwa juu kuliko faida iliyokuwa ikipatikana katika biashara husika.

Kipindi hicho chote maisha yangu na familia yangu yamekuwa magumu kuliko kawaida; nimetafuta kazi bila mafanikio; biashara imekwama kutokana na upungufu wa mtaji; chakula kimekuwa cha kubahatisha wakati mwingine watoto hulala bila kula; nimekwama kulipa kodi ya nyumba hivyo kulimbikiza madeni kwa mwenye nyumba; haya ni machache tu yanayonikabili, yapo mengi zaidi.

Kauli ya Rais ilivyonifurahisha: Mimi ni miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu waliofurahishwa na kauli ya Rais aliyoitoa wakati akitatua mzozo wa kisimanzi uliokuwa umejitokeza katika jamii ya wafanyakazi juu ya kikotoo. Kauli ya Rais iliamuru mifuko ya kijamii ifanye kama ilivyokuwa ikifanya hapo mwanzo. Rais alienda mbele kidogo kwa kufafanua kuwa mtu hawezi kumaliza mkataba wake alafu ukamwambia eti unamtunzia pesa zake (alimaanisha kufanya hivyo ni kumnyanyasa na kumtesa mwenye pesa zake). Kauli hii ilinifurahisha sana, nikamsifu Rais wangu mpendwa, nikatafsiri neno mnyonge nikajiona kuwa mimi ni mmoja wao, nikatafsiri “Rais wa wanyonge” nikagundua ni Rais wetu, kwa ufupi niliamini nitapata FAO LA KUJITOA na hivyo kuendeleza biashara na kuyabadili maisha kuwa bora zaidi.

Kauli ya Rais ilivyonitesa: Kwa kuwa nilikuwa tayari nimetoka mkoa niliyokuwa nikifanyia kazi (Kagera) na kurudi nyumbani nilikozaliwa (Mbeya, Tukuyu, Ilima) niliamua kutoka Mbeya hadi Kagera-Bukoba kufungua fao la kujitoa. Kwa kuwa nilikuwa na nyaraka zote sikupata usumbufu wa kupokelewa japo kauli za kukatisha tamaa zilikuwepo. Nilipokamilisha taratibu nikaambiwa nisubiri kwa muda wa mwezi mmoja na nusu pesa yangu yote itakuwa imeingia (hiyo ilikuwa ni tarehe 22/1/2019). Hatua hii ya kufatilia fao la kujitoa kutoka Mbeya hadi Kagera ilinitesa sana kwani nilikopa pesa kwa ajili ya; safari;malazi;chakula; na kuiachia familia. Wote walionikopesha pesa hii wengi wao wakiwa ni rafiki zangu tulikuwa na kusoma pamoja niliwaahidi kuwalipa baada ya miezi miwili. Nilianza safari ya kurudi Mbeya nikiwa na matumaini ya kuipata pesa yangu halali ndani ya muda tajwa, japo niliteseka kwa kukopa pesa.

Kauli ya Rais inavyonitesa: Baada ya kutimia mwezi mmoja na nusu sikuona pesa katika akaunti yangu. Nikafanya mawasiliano nikaambiwa nitulie kwani jukumu langu nimemaliza niwaache wao pia wamalizie jukumu lao, nilipotaka kudadisi zaidi kuwa nitegemee lini kupata pesa hiyo simu ikakatwa. Nimekuwa nikiteseka kuwashawishi wanaonidai kuwa sijapata pesa, mmoja wao amekuwa mkali kiasi cha kunitamkia maneno makali akihitaji pesa yake na si ahadi. Kweli ninateseka; nawaza familia itakula nini; nawaza madeni ya watu; MUNGU NISAIDIE!.

Kauli ya Rais itaendelea kunitesa: Hivi sasa naelekea kukamilisha miezi mitatu tangu kukamilisha mchakato wa kupatiwa fao la kujitoa. Nimejitahidi kufanya mawasiliano huko Bukoba bado majibu ni yale yale ya kwamba niwaache watekeleze majukumu yao. Sizioni dalili za kuipata pesa yangu halali; wanaonidai wamepamba moto; maisha yamezidi kuwa magumu; najitazama, nawaza na kujisemea moyoni kuwa kama kauli ya Rais mpendwa isiposimamiwa vizuri, nikapata fao la kujitoa ITAENDELEA KUNITESA.

Pole sana mkuu, ila kwa maneno ya watu mitaani husema itakupasa usubiri kwa muda wa MIEZI SITA.

Kwa nini MIEZI SITA?
Kwa kuwa mkataba wako ulimalizika na hukuwa na kazi nyingine ndio maana uliamua kufungua Madai, lakini vipi kama ikitokea ukapata kazi sehemu nyingine ndani ya miezi miwili baada ya ule mkataba wako wa kwanza kuisha?
Namaanisha hivi;
Wao watakuacha miezi sita ukae nyumbani kwanza ili kama utapata Kibarua ndani ya muda huo basi hawatokulipa pesa yoyote bali wataunganisha akaunti yako ya zamani na hiyo mpya kuendelea kutunisha mfuko/acc

Ila kama ikifika miezi sita watakupa tu mzigo wako hivyo umeshaianza safari, jaribu kuwa mvumilivu itamalizika tu ila jiandae kisaikolojia
 
Dah! Kauli ya Rais yaniua najitazama. Mungu akubaliki Rais kwa kunitesa.
 
Nzee muongo sana ana mtindo wa kuonesha kuwa hausiki na tatizo ila ukichunguza utagundua yeye ndie yupo nyuma ya tatizo.
SASA HAPA MAGUFULI ANAHUSIKA VIPI??? Yeye alishasema mlipwe, sasa kama kuna watu wanaendelea kuwazungusha lawama hapa zinamjiaje kwa mfano.. Anakujua kusema kwamba KASIKIA HUJALIPWA CHAKO AFU KAKAA KIMYA AU??? Hivi mna nini na huyu mzee ndugu zng Mfano baba ako akitoa kauli mama akupe hela ya madaftari afu mama ako asipokupa hapo baba ako anahusika vipi..??? Yaani kila siku mnaamka na mbinu mpya ya kumchafua huyu mzee Ukipata muda soma tena kwa umakini essay yako uliyotuandikia afu ujiulize wee mwenyewe, JE NINA HAKI YA KUENDELEA KUMCHAFUA HUYU MZEE NAMNA HII, Jibu utakalopata baki nalo mwenyewe
 
Pole sana mkuu, ila kwa maneno ya watu mitaani husema itakupasa usubiri kwa muda wa MIEZI SITA.

Kwa nini MIEZI SITA?
Kwa kuwa mkataba wako ulimalizika na hukuwa na kazi nyingine ndio maana uliamua kufungua Madai, lakini vipi kama ikitokea ukapata kazi sehemu nyingine ndani ya miezi miwili baada ya ule mkataba wako wa kwanza kuisha?
Namaanisha hivi;
Wao watakuacha miezi sita ukae nyumbani kwanza ili kama utapata Kibarua ndani ya muda huo basi hawatokulipa pesa yoyote bali wataunganisha akaunti yako ya zamani na hiyo mpya kuendelea kutunisha mfuko/acc

Ila kama ikifika miezi sita watakupa tu mzigo wako hivyo umeshaianza safari, jaribu kuwa mvumilivu itamalizika tu ila jiandae kisaikolojia
mkuu hata ukae miezi tisa huna kazi hawa mabwana wakubwa hawatoi hela yoyote
 
SASA HAPA MAGUFULI ANAHUSIKA VIPI??? Yeye alishasema mlipwe, sasa kama kuna watu wanaendelea kuwazungusha lawama hapa zinamjiaje kwa mfano.. Anakujua kusema kwamba KASIKIA HUJALIPWA CHAKO AFU KAKAA KIMYA AU??? Hivi mna nini na huyu mzee ndugu zng Mfano baba ako akitoa kauli mama akupe hela ya madaftari afu mama ako asipokupa hapo baba ako anahusika vipi..??? Yaani kila siku mnaamka na mbinu mpya ya kumchafua huyu mzee Ukipata muda soma tena kwa umakini essay yako uliyotuandikia afu ujiulize wee mwenyewe, JE NINA HAKI YA KUENDELEA KUMCHAFUA HUYU MZEE NAMNA HII, Jibu utakalopata baki nalo mwenyewe
Katika huu upumbavu, nimeshangaa tu kumuona mtu ninaemuheshimu kama Khantwe ame-like
 
SASA HAPA MAGUFULI ANAHUSIKA VIPI??? Yeye alishasema mlipwe, sasa kama kuna watu wanaendelea kuwazungusha lawama hapa zinamjiaje kwa mfano.. Anakujua kusema kwamba KASIKIA HUJALIPWA CHAKO AFU KAKAA KIMYA AU??? Hivi mna nini na huyu mzee ndugu zng Mfano baba ako akitoa kauli mama akupe hela ya madaftari afu mama ako asipokupa hapo baba ako anahusika vipi..??? Yaani kila siku mnaamka na mbinu mpya ya kumchafua huyu mzee Ukipata muda soma tena kwa umakini essay yako uliyotuandikia afu ujiulize wee mwenyewe, JE NINA HAKI YA KUENDELEA KUMCHAFUA HUYU MZEE NAMNA HII, Jibu utakalopata baki nalo mwenyewe
Mm niliambiwa na kuoneshwa barua kabisa na meneja yenye maelezo tofauti na kauli yawalipwe
Kifupi jiwe anacheza na akili za watz anatoa tamko hadharani aonekane mwa hali ya kua ni mtu hatari akirudi ofisini anasema tofauti kwa watendaj
 
Back
Top Bottom