Kauli ya Rais juu ya fao la kujitoa ilivyonifurahisha kisha ikanitesa, inanitesa na itaendelea kunitesa

Utangulizi: Mkataba wangu wa kazi ulifikia ukomo tangu tarehe 31/12/2017. Sikuwa nimejiandaa sana juu ya ukomo wa kuendelea na kazi kwani kampuni niliyokuwa nikiifanyia kazi ilikuwa na utaratibu wa kutupatia mkataba wa muda wa mwaka mmoja na kila ulipoisha tulipewa mkataba mwingine, mwaka huo wa 2017 mambo yakawa kinyume na matarajio kwani kampuni ililazimika kupunguza wafanyakazi, mimi ni miongoni mwa wafanyakazi 16 ambao hatukupewa mkataba kwa mwaka 2018.
Niliamua kutumia pesa yangu kidogo iliyokuwa benki kuanzisha biashara ambayo haikufanya vizuri kulingana na matumizi ya kifamilia (ada za watoto shule,matibabu, chakula na kodi ya nyumba) kuwa juu kuliko faida iliyokuwa ikipatikana katika biashara husika.
Kipindi hicho chote maisha yangu na familia yangu yamekuwa magumu kuliko kawaida; nimetafuta kazi bila mafanikio; biashara imekwama kutokana na upungufu wa mtaji; chakula kimekuwa cha kubahatisha wakati mwingine watoto hulala bila kula; nimekwama kulipa kodi ya nyumba hivyo kulimbikiza madeni kwa mwenye nyumba; haya ni machache tu yanayonikabili, yapo mengi zaidi.
Kauli ya Rais ilivyonifurahisha: Mimi ni miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu waliofurahishwa na kauli ya Rais aliyoitoa wakati akitatua mzozo wa kisimanzi uliokuwa umejitokeza katika jamii ya wafanyakazi juu ya kikotoo. Kauli ya Rais iliamuru mifuko ya kijamii ifanye kama ilivyokuwa ikifanya hapo mwanzo. Rais alienda mbele kidogo kwa kufafanua kuwa mtu hawezi kumaliza mkataba wake alafu ukamwambia eti unamtunzia pesa zake (alimaanisha kufanya hivyo ni kumnyanyasa na kumtesa mwenye pesa zake). Kauli hii ilinifurahisha sana, nikamsifu Rais wangu mpendwa, nikatafsiri neno mnyonge nikajiona kuwa mimi ni mmoja wao, nikatafsiri “Rais wa wanyonge” nikagundua ni Rais wetu, kwa ufupi niliamini nitapata FAO LA KUJITOA na hivyo kuendeleza biashara na kuyabadili maisha kuwa bora zaidi.
Kauli ya Rais ilivyonitesa: Kwa kuwa nilikuwa tayari nimetoka mkoa niliyokuwa nikifanyia kazi (Kagera) na kurudi nyumbani nilikozaliwa (Mbeya, Tukuyu, Ilima) niliamua kutoka Mbeya hadi Kagera-Bukoba kufungua fao la kujitoa. Kwa kuwa nilikuwa na nyaraka zote sikupata usumbufu wa kupokelewa japo kauli za kukatisha tamaa zilikuwepo. Nilipokamilisha taratibu nikaambiwa nisubiri kwa muda wa mwezi mmoja na nusu pesa yangu yote itakuwa imeingia (hiyo ilikuwa ni tarehe 22/1/2019). Hatua hii ya kufatilia fao la kujitoa kutoka Mbeya hadi Kagera ilinitesa sana kwani nilikopa pesa kwa ajili ya; safari;malazi;chakula; na kuiachia familia. Wote walionikopesha pesa hii wengi wao wakiwa ni rafiki zangu tulikuwa na kusoma pamoja niliwaahidi kuwalipa baada ya miezi miwili. Nilianza safari ya kurudi Mbeya nikiwa na matumaini ya kuipata pesa yangu halali ndani ya muda tajwa, japo niliteseka kwa kukopa pesa.
Kauli ya Rais inavyonitesa: Baada ya kutimia mwezi mmoja na nusu sikuona pesa katika akaunti yangu. Nikafanya mawasiliano nikaambiwa nitulie kwani jukumu langu nimemaliza niwaache wao pia wamalizie jukumu lao, nilipotaka kudadisi zaidi kuwa nitegemee lini kupata pesa hiyo simu ikakatwa. Nimekuwa nikiteseka kuwashawishi wanaonidai kuwa sijapata pesa, mmoja wao amekuwa mkali kiasi cha kunitamkia maneno makali akihitaji pesa yake na si ahadi. Kweli ninateseka; nawaza familia itakula nini; nawaza madeni ya watu; MUNGU NISAIDIE!.
Kauli ya Rais itaendelea kunitesa: Hivi sasa naelekea kukamilisha miezi mitatu tangu kukamilisha mchakato wa kupatiwa fao la kujitoa. Nimejitahidi kufanya mawasiliano huko Bukoba bado majibu ni yale yale ya kwamba niwaache watekeleze majukumu yao. Sizioni dalili za kuipata pesa yangu halali; wanaonidai wamepamba moto; maisha yamezidi kuwa magumu; najitazama, nawaza na kujisemea moyoni kuwa kama kauli ya Rais mpendwa isiposimamiwa vizuri, nikapata fao la kujitoa ITAENDELEA KUNITESA.
 
Hali si shwari,Mtu ukikosa kazi na familia inakutazama utahisi kufa,hizi porojo za mzee huyu mi nahisi anaelekea kuwa bashir na yeye.

Anawatesa sana wananchi wa kipato cha chini.Hii mifuko haina pesa kwani hata watumishi wanakili wazi kuwa bado hawajapewa waraka wa kulipa mafao ya watu,ila ukifungua madai wanapokea na wanayaweka kabatini kungojea waraka wa ulipaji,sa sijui itakuwa baada ya jiwe kutoka madarakani 2025?

Huu wakati kuna watu wanakula neema ya nchi ila kuna wengine wanaishi kama mashetani.Tulikosea sana kupata mtu wa namna hii,inahitajika nguvu ya ziada kulekebisha hii hali la sivyo hii miaka kumi ikiisha na sisi tutakuwa tumeisha
Ni balaa mkuu.
 
Unateswa na agizo la rais au na watendaji wa nssf
Nateswa na kauli ya rais kwa sababu watendaji wa NSSF wanadai ilikuwa ni siasa tu za majukwaani wao hawatoi hela wala hawajaagizwa kutoa. Nadhani kuteswa na kauli ya rais ni sawasawa na kuteswa na rais, hivyo Rais ananitesa.
 
Ila ukumbukwe kuwa "wanyonge hawataurithi ufalme wa mbinguni" hivyo kwa vile yule ni raisi wako "wa wanyonge" unapaswa usipewe kabisa hizo pesa kwa vile ni "mnyonge".
Mimi sio mnyonge hivyo huyo ni raisi wenu nyie wanyonge.
Kumbuka pia ile methali isemayo
"Mnyonge mnyongeni,.......ila haki yake mpeni"
Kwa hiyo wewe mnyonge unastahiki kunyongwa then ukifa haki yako utapata.
Pole mnyonge wa John.
Asante kwa kunikosoa mimi na rais anayependa kusema "yeye ni rais wa wanyonge". Yote kwa yote kauli ya rais inanitesa.
 
POLE SANA MKUU HII NDIO TZ,KENYA NILISHUHUDIA HUWA WANALIPWA HARAKA SANA UKISHAKAMILISHA WEWE AFTER 3 WEEK OR 4 PESA INAKUWA TAYARI ILA HUKU KWETU SASA MMMMMH

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka 2015 Nilipata mafao yangu ndani ya siku kumi tu...

sasa hivi nasikia hii mifuko ina hali mbaya sana kifedha....muheshimiwa anaikopa sana
 
Back
Top Bottom