Kauli ya Rais juu ya fao la kujitoa ilivyonifurahisha kisha ikanitesa, inanitesa na itaendelea kunitesa

Mshikawezi Mwizi

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
751
374
Utangulizi: Mkataba wangu wa kazi ulifikia ukomo tangu tarehe 31/12/2017. Sikuwa nimejiandaa sana juu ya ukomo wa kuendelea na kazi kwani kampuni niliyokuwa nikiifanyia kazi ilikuwa na utaratibu wa kutupatia mkataba wa muda wa mwaka mmoja na kila ulipoisha tulipewa mkataba mwingine, mwaka huo wa 2017 mambo yakawa kinyume na matarajio kwani kampuni ililazimika kupunguza wafanyakazi, mimi ni miongoni mwa wafanyakazi 16 ambao hatukupewa mkataba kwa mwaka 2018.

Niliamua kutumia pesa yangu kidogo iliyokuwa benki kuanzisha biashara ambayo haikufanya vizuri kulingana na matumizi ya kifamilia (ada za watoto shule,matibabu, chakula na kodi ya nyumba) kuwa juu kuliko faida iliyokuwa ikipatikana katika biashara husika.

Kipindi hicho chote maisha yangu na familia yangu yamekuwa magumu kuliko kawaida; nimetafuta kazi bila mafanikio; biashara imekwama kutokana na upungufu wa mtaji; chakula kimekuwa cha kubahatisha wakati mwingine watoto hulala bila kula; nimekwama kulipa kodi ya nyumba hivyo kulimbikiza madeni kwa mwenye nyumba; haya ni machache tu yanayonikabili, yapo mengi zaidi.

Kauli ya Rais ilivyonifurahisha: Mimi ni miongoni mwa makundi mbalimbali ya watu waliofurahishwa na kauli ya Rais aliyoitoa wakati akitatua mzozo wa kisimanzi uliokuwa umejitokeza katika jamii ya wafanyakazi juu ya kikotoo. Kauli ya Rais iliamuru mifuko ya kijamii ifanye kama ilivyokuwa ikifanya hapo mwanzo. Rais alienda mbele kidogo kwa kufafanua kuwa mtu hawezi kumaliza mkataba wake alafu ukamwambia eti unamtunzia pesa zake (alimaanisha kufanya hivyo ni kumnyanyasa na kumtesa mwenye pesa zake). Kauli hii ilinifurahisha sana, nikamsifu Rais wangu mpendwa, nikatafsiri neno mnyonge nikajiona kuwa mimi ni mmoja wao, nikatafsiri “Rais wa wanyonge” nikagundua ni Rais wetu, kwa ufupi niliamini nitapata FAO LA KUJITOA na hivyo kuendeleza biashara na kuyabadili maisha kuwa bora zaidi.

Kauli ya Rais ilivyonitesa: Kwa kuwa nilikuwa tayari nimetoka mkoa niliyokuwa nikifanyia kazi (Kagera) na kurudi nyumbani nilikozaliwa (Mbeya, Tukuyu, Ilima) niliamua kutoka Mbeya hadi Kagera-Bukoba kufungua fao la kujitoa. Kwa kuwa nilikuwa na nyaraka zote sikupata usumbufu wa kupokelewa japo kauli za kukatisha tamaa zilikuwepo. Nilipokamilisha taratibu nikaambiwa nisubiri kwa muda wa mwezi mmoja na nusu pesa yangu yote itakuwa imeingia (hiyo ilikuwa ni tarehe 22/1/2019). Hatua hii ya kufatilia fao la kujitoa kutoka Mbeya hadi Kagera ilinitesa sana kwani nilikopa pesa kwa ajili ya; safari;malazi;chakula; na kuiachia familia. Wote walionikopesha pesa hii wengi wao wakiwa ni rafiki zangu tulikuwa na kusoma pamoja niliwaahidi kuwalipa baada ya miezi miwili. Nilianza safari ya kurudi Mbeya nikiwa na matumaini ya kuipata pesa yangu halali ndani ya muda tajwa, japo niliteseka kwa kukopa pesa.

Kauli ya Rais inavyonitesa: Baada ya kutimia mwezi mmoja na nusu sikuona pesa katika akaunti yangu. Nikafanya mawasiliano nikaambiwa nitulie kwani jukumu langu nimemaliza niwaache wao pia wamalizie jukumu lao, nilipotaka kudadisi zaidi kuwa nitegemee lini kupata pesa hiyo simu ikakatwa. Nimekuwa nikiteseka kuwashawishi wanaonidai kuwa sijapata pesa, mmoja wao amekuwa mkali kiasi cha kunitamkia maneno makali akihitaji pesa yake na si ahadi. Kweli ninateseka; nawaza familia itakula nini; nawaza madeni ya watu; MUNGU NISAIDIE!.

Kauli ya Rais itaendelea kunitesa: Hivi sasa naelekea kukamilisha miezi mitatu tangu kukamilisha mchakato wa kupatiwa fao la kujitoa. Nimejitahidi kufanya mawasiliano huko Bukoba bado majibu ni yale yale ya kwamba niwaache watekeleze majukumu yao. Sizioni dalili za kuipata pesa yangu halali; wanaonidai wamepamba moto; maisha yamezidi kuwa magumu; najitazama, nawaza na kujisemea moyoni kuwa kama kauli ya Rais mpendwa isiposimamiwa vizuri, nikapata fao la kujitoa ITAENDELEA KUNITESA.
 
POLE SANA MKUU HII NDIO TZ,KENYA NILISHUHUDIA HUWA WANALIPWA HARAKA SANA UKISHAKAMILISHA WEWE AFTER 3 WEEK OR 4 PESA INAKUWA TAYARI ILA HUKU KWETU SASA MMMMMH

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika barua ngapi za malalamiko katika ofisi husika au mamlaka inayosimamia hiyo ofisi ya mfuko uliokuwa ukichangia?? Walikujibuje?
Nakushauri kama haujafanya hivyo changamka uwasilishe kwa maandishi kwa kuambatisha vielelezo vyako ikibidi na waliokuwa wanakuhudumia uwataje kwa uharaka wa ufumbuzi.

Kumbuka Maofisi yanafanya kazi kwa maandishi. Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba muongozo kidogo mkuu. Barua za malalamiko nazawathirisha Bukoba au makao makuu ya NSSF? Nitumie njia gani? Ni lazima niandae tena safari ya kupeleka barua?. Natanguliza shukrani mkuu.
 
mkuu umeingia gharama bure, mafao unaomba kwenye mfuko wa jamii ulio karibu na wewe ili uweze kufuatilia, utakwenda Kagera tu kama umeamua kuhakiki michango yako na wakujazie form lakini unaibeba unaileta ofisi jirani na wewe (hii ilikuwa zamani hata hivyo). siku hizi ni digitally unafungua tu madai yako
 
Kifupi ni kuwa hao NSSF na mifuko mingine wamezuiliwa kutoa pesa kwani serikali imekopa sana kwenda kuwekeza kwenye viwanda na mikopo ya kuendeshea serikali. Hilo deni kwenye mifuko ya hifadhi kwa mujibu wa CAG ni matrilioni ya pesa ndo maana wote hawatoi pesa kuna wengi wanadai huko NSSF na PPF (sasa inaitwa PSSSF). Ni ahadi tu . Tunatakiwa tuone nini tutafanya yale maneno na kumtumbua Irene Isaka ilikuwa ni kujitafutia mileage ya kisiasa yaani tunaumwa na kupulizwa.
 
Naomba muongozo kidogo mkuu. Barua za malalamiko nazawathirisha Bukoba au makao makuu ya NSSF? Nitumie njia gani? Ni lazima niandae tena safari ya kupeleka barua?. Natanguliza shukrani mkuu.
Mkuu Haina haja ya kwenda bukoba we fatilia ofisi ya nssf iliyo karibu na wewe, ulijisumbua tu kwenda bukoba kufungua madai ungefungulia ofisi iliyo karibu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kifupi ni kuwa hao NSSF na mifuko mingine wamezuiliwa kutoa pesa kwani serikali imekopa sana kwenda kuwekeza kwenye viwanda na mikopo ya kuendeshea serikali. Hilo deni kwenye mifuko ya hifadhi kwa mujibu wa CAG ni matrioni ya pesa ndo maana wote hawatoi pesa kuna wengi wanadai huko NSSF na PPF (sasa inaitwa PSSSF). Ni ahadi tu . Tunatakiwa tuone nini tutafanya yale maneno na kumtumbua Irene Isaka ilikuwa ni kujitafutia mileage ya kisiasa yaani tunaumwa na kupulizwa.
Inauma aisee....
 
Hata mimi nimehisi hicho kitu.....Kauli ya Rais wa wanyonge juu ya fao la kujitoa itaendelea kuninyonga daima, japo hata mimi ni mnyonge.
 
Back
Top Bottom