Kauli ya Prof. Elifas Bisanda juu ya tahadhari ya Corona kwa wafanyakazi na wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria Tanzania inatoa picha gani kwa wasomi?

Wasomi wetu watia aibu sana. Prof. Bisanda, Makamu wa Chuo Kikuu Huria (OUT) anahojiwa na BBC ni kwa nini ameamua kuwataka wanafunzi wake wabakie nyumbani kusoma kwa mtandao?

"Hilo haliwahusu, mimi nimetoa taarifa hiyo kwa wanafunzi wangu tu na wafanyakazi wa Chuo kuhusiana na Corona, haliwahusu si lenu!"

Mashaka! Tujikinge!

Kuhusu waraka, soma > Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21

Kama hii ndiyo Sura yake wala sishangai kwa Maelezo ( Majibu ) yake ya Kipuuzi aliyoyatoa. Nawaonea mno Huruma Wanafunzi waliofundishwa nae.
 
Profesa Bisanda (Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania) umesimama katika zamu yako lakini Itifaki imekuponza! Ungana na Askofu Mwamakula atakapokuja katika eneo lako kuongoza "Matembezi ya Hiyari" yenye lengo la kuhamasisha umma kuhusu umuhimu na uhitaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya!

Ndiyo! Wasomi wa ngazi yako wanapaswa kuwa mstari wa mbele kutetea haki, ukweli na ustawi katika jamii! Ndiyo! Tunataka kuandika Katiba Mpya itakayorudisha uhuru wa fikra na mamlaka stahiki kwa Vyuo Vikuu pia. Tunataka Tume Huru ya Uchaguzi itakayoheshimu maamuzi ya wananchi kuhusu nani wawe viongozi wao!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
 
Back
Top Bottom