Kauli ya Paul Makonda ni taa nyekundu kwa Dr Ryoba?

Huyo anamponda Dr. Ryoba kwa sababu aliteuliwa na nape

TBC haipo Huru hata wakileta mkurugenzi Mzungu hawezi kufanya chochote labda kuwa na mipaka ya kumzuia Naibu Rais ndugu Daud Maliyamungu Bashite kuwaingilia kienyeji
 
Kuna tofauti kati ya Katibu wa itikadi na uenezi na Msemaji wa chama.

Kwa sasa msemaji wa chama ni jukumu linalofanywa ama na Katibu mkuu au na Katibu wa itikadi na uenezi hivyo ingekuwa vema kama Tido angeziba hilo ombwe.

Jumatatu njema
Maendeleo hayana vyama!
 
Tumesikia mkuu wa mkoa wa Dar mtukufu Paul Makonda akimwaga sifa kwa mkurugenzi wa Azam TV ambaye pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa TBC ndugu Tido Mhando.

Kauli ya mtukufu Paul Makonda ilionesha kutoridhika kwake kuona mtu mwenye ubunifu kamaTido Mhando anawafaidisha Azam.

Maswali:
1. Dr Ryoba anawashiwa taa nyekundu?

2. Mtukufu Paul Makonda havutiwi na ubunifu wa mtaalamu na gwiji wa fani ya habari Dr Ryoba?

3. Ubunifu wa Dr Ryoba pale TBC wa kuanzisha vipindi vya Tunatekeleza, Safari ya Dodoma, live coverage ya matukio ya CCM, wasanii kutembelea ujenzi wa reli, hotuba za Mh sana nk yeye (Mtukufu Paul Makonda ) hajavutiwa hadi avutiwe na TV za nje?

4. Anapata wapi muda wa kuangalia Azam TV na kuacha kuangalia TV ya kizalendo (TBC1)

Asante
Baadhi ya maswali yako yana majibu ya wazi sana. Mfano hilo swali la 4; WanaCCM wengi hawaangalii hiyo TV na hata madazeti yao Uhuru na Mzalendo yanaishi kwa fedha za kodi zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niwafahamishe tu chama kikongwe sasa kinamiliki channel ten, dtv, na vituo vyote vya redio vyenye undugu na hizo tv kwa hiyo inawezekana anahitajika mtu mwenye upeo wa kutosha kuweza endesha vyombo hivyo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom