Kauli ya P.Chagonja inamaanisha Polisi wameshindwa kazi yao?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
P.Chagonja alitoa tamko la kumshauri Mbowe apeleke ushahidi kwa Amiri Jeshi Mkuu kama hawaamini Polisi hii ina maana hawana namna nyingine ya kumpata mtuhumiwa hadi wategemee ushahidi wa Mbowe hata baada ya Serikali kutangaza dau la sh: 100 milioni? Kwa maana hiyo sasa jeshi la Polisi limeshindwa kazi maana hata kwenye video ya Lwakatare badala ya kufanya uchunguzi waliitegemea video ile? Kama jeshi la Polisi halijashindwa kazi na kama Chagonja si msemaji wa Jeshi la Polisi kwanini asijiuzulu au awajibishwe?
 
Nani anaimani na huyo amiri jeshi, hii swala waliweke JF, wananchi ndiyo watalitolea majibu, maana hii nchi ni ya watanzania na Si ya amiri jeshi wa CCM.
 
Nkubaliana na wewe kwa kuwa kama Waziri Mkuu anatoa kauli ya kuamuru watu wapigwa na asiwajibishwa si ina maana anaungwa mkono.
 
P.Chagonja alitoa tamko la kumshauri Mbowe apeleke ushahidi kwa Amiri Jeshi Mkuu kama hawaamini Polisi hii ina maana hawana namna nyingine ya kumpata mtuhumiwa hadi wategemee ushahidi wa Mbowe hata baada ya Serikali kutangaza dau la sh: 100 milioni? Kwa maana hiyo sasa jeshi la Polisi limeshindwa kazi maana hata kwenye video ya Lwakatare badala ya kufanya uchunguzi waliitegemea video ile? Kama jeshi la Polisi halijashindwa kazi na kama Chagonja si msemaji wa Jeshi la Polisi kwanini asijiuzulu au awajibishwe?
polisi yetu uwezo wake ni mdogo sana,wapo wapo tu hakuna tukio likatokea wakafanya kazi wananchi tukafurahi....jiulize ni mara ngapi umesikia tukio furani limetokea na polisi inawashikilia watu 200 wakati mashuhuda wanasema wahusika walikua wawili au watatu nk lkn polisi yetu ni kukamata na kufanya torture mpaka basi.cha msingi cha kujiuliza hivi mtu aliyefeli shule na kuingia polisi kijanja janja leo hii akawa mpelelezi anaweza kweli kuunganisha matukio na kumpata mhusika?
 
Back
Top Bottom