Kauli ya Ndugai kuhusu mikopo ya serikali inapiga king'ora cha tahadhari kwa taifa

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,215
3,587
Ninaifananisha kauli ya Mhe. Ndugai kuhusu deni la taifa na hadithi hii niliyoghani. Vumilia usome mwanzo mwisho utapata cha kujifunza kwa nchi zetu hizi maskini.

Taifa moja maskini sana duniani huko bara Asia limepitisha sheria ambayo haikuwahi kuwepo duniani na Mbinguni ili kukusanya mapato kwa ajili ya kuendeshea serikali yake na taifa kwa ujumla.

Sheria hiyo inaipa serikali ya nchi hiyo hakimiliki ya magego ya watu wake wote walio hai na wafu na watu wake kuruhusiwa kumiliki meno ya mbele na ya kati tu.

Baada ya Wabunge kukaa miezi mitatu bila kulipwa mishahara na posho stahiki kufuatia hazina ya taifa kukauka (kufilisika), sheria hiyo iliandikwa na kukimbizwa Bungeni kwa dharura na ilipowafikia tu walifanya haraka kuipitisha kwa kura zote za ndiyo (zikiwemo za kambi ya upinzani) na kufanya magego ya binadamu kuingizwa kwenye kundi la nyara za serikali katika nchi hiyo.

Serikali hiyo ilipata habari kwamba taifa moja kubwa (barani Asia) linaloongoza kwa ukubwa wa kijiografia na idadi ya watu duniani (18% ya watu wa dunia) limegundua teknolojia mpya kabisa duniani ya kukeleza (kunakshi) magego ya binadamu kwa ajili ya kutengenezea mapambo ya thamani kubwa ambayo yana soko kubwa nchini humo na kwamba ugunduzi huo utaokoa Tembo wachache waliosalia kwenye sayari ambao wanawindwa kwa ajili ya meno yao.

Idara ya Takwimu Kitengo cha Sensa cha taifa hilo maskini ikafanya sensa na kugundua taifa lina watu 50ml walio hai na Idara ya Kabidhi Wasihi Mkuu wa Serikali ikafanya sensa ya wafu na kugundua wako 40ml waliokufa kabla na baada ya uhuru wake 1960 na kufanya jumla ya watu wa nchi (hai na wafu) kuwa 90ml.

Kwa mujibu wa taarifa za soko la bidhaa hizo (magego) ni kuwa mtu mmoja ana magego 12 yenye thamani ya jumla ya 24ml (kwa fedha za Kitanzania), hivyo kwa watu 90ml (walio hai na wafu), ukizidisha na 24ml unapata jumla ya fedha za Kitanzania 2,160,000,000,000,000 quad (Quadrilioni mbili na trilioni mia moja sitini). Bajeti ya mwaka ya nchi hiyo maskini inafikia trilioni 20 tu kwa fedha za Kitanzania.

Baada ya kubaini chanzo hiki kipya cha mapato makubwa ya nchi, serikali iliamua kwenda kukopa fedha kwenye masoko ya mitaji ya nchi hiyo iliyogundua matumizi ya magego; kwa kutumia sheria hiyo kama dhamana ili kwamba serikali itakuwa inarejesha mkopo kwa kung’oa magego ya wafu na wagonjwa wa meno na kuyapeleka kwenye masoko hayo ya mitaji.

Mkataba wa mkopo huo sasa utayapa masoko yale ya mitaji ya nchi hiyo tajiri barani Asia kumiliki magego ya watu 6,666,666.7ml (ama walio hai au wafu) wa nchi hiyo maskini kwa miaka 15 ijayo ambao ndiyo muda wa uhai wa mkopo kwa mujibu wa mkataba.

Aidha, sheria hii ya serikali kumiliki magego ambayo sasa (sheria) imewekwa bondi/dhamana katika masoko hayo ya mitaji, masharti ya mkataba wa mkopo yanaibana nchi hiyo maskini kutoifanyia marekebisho yoyote sheria hiyo kwa miaka 15 ambayo ndiyo uhai wa mkopo huo, huku Mashirika ya Haki za Binadamu yakianza kampeni kubwa ya kufa na kupona duniani kote kuichagiza serikali hiyo kufutilia mbali sheria hiyo dhalimu ili kurejesha utu wa watu wake.

Yafuatayo ni mojawapo ya masharti magumu katika mkataba wa mkopo huo kwa nchi mnufaika:-

1. Kutumia sheria hiyo mpya kama moja ya dhamana za mkopo ambapo nchi mkopaji hairuhusiwi (ima faima) ama kuifuta au kuifanyia marekebisho yoyote sheria hiyo.

2. Masoko ya mitaji (wakopeshaji) wanayo haki 100% na mamlaka makubwa ya mwisho kudurusu sheria hiyo ya nchi mkopaji ikiwemo kuiongezea muda wake wa kuwa dhamana kwenye mkataba wa mkopo bila kuingiliwa na mamlaka yoyote ya nchi mkopaji zikiwemo Bunge na Mahakama.

3. Masoko ya mitaji ndani ya miaka miwili ya mkataba wa mkopo, yataleta azimio la kuiagiza nchi mkopaji kuanzisha na kutekeleza sera ya kuongeza kiwango cha kuzaliana (Birth Rate) wananchi wake ili malighafi za magego zipatikane kwa wingi kukidhi mahitaji ya viwanda vya nchi mkopeshaji. (Masoko haya ya mitaji yana hisa za jumla ya 51% katika kundi la viwanda vinavyotumia malighafi za magego).

4. Nchi mkopaji hairuhusiwi kujenga kiwanda cha kuchakata malighafi za magego ya binadamu.

5. Nchi mkopaji hairuhusiwi kununua teknolojia hiyo ya kukeleza (kunakshi) magego ya binadamu kwa ajili ya kutengenezea mapambo (hairuhusiwi kujenga kiwanda hicho).

Kufuatia ukata ulioingia kwenye rekodi ya dunia unaokabili hazina ya serikali ya nchi mkopaji; hali inayotishia usalama wa taifa kutokana na kwamba hazina hiyo sasa imebaki na fedha za kulipa mishahara ya majeshi tu, Baraza la Mawaziri na kuendesha Ikulu kwa 50% na kwa mwaka mmoja wa fedha tu, bado serikali hiyo haikusita kuridhia masharti hayo magumu kwenye mkataba ili tu iweze kupata mkopo huo.

Aidha, serikali mkopaji imegundua kwamba inaweza kuendesha nchi kwa ziada kwa kutumia sekta moja tu ya magego bila kugusa rasilimali zingine za nchi.

Wakati mkopo ukisubiriwa kwa hamu kubwa kuidhinishwa baada ya kukidhi masharti na vigezo vyote vya mkataba wa mkopo, serikali hiyo maskini imeandaa na kukimbiza Bungeni Mpango wa Serikali wa Maendeleo ya Taifa kwa miaka mi5 ukibainisha na kuainisha maeneo ya kipaumbele ambayo itabuniwa miradi mikubwa ya kimkakati ya thamani ya jumla ya fedha za Kitanzania 100,000,000,000,000 (Trilioni mia moja) huku ikikimbizana kuandaa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2021-2041.

Mashirika hayo ya Haki za Binadamu tayari kwa pamoja yamekubaliana kuwasilisha kwenye Mahakama ya Biashara ya Dunia hati ya dharura ya kuweka zuio kwa makampuni ya kikandarasi duniani kutowania zabuni za ujenzi wa miradi ya kimkakati ya maendeleo katika taifa hilo maskini.

Wanadiaspora wa nchi mkopaji wameungana na Mashirika hayo ya Haki za Binadamu kuipinga serikali ya nchi yao wakisisitiza kwamba nchi yao imeuzwa.

Aidha, kiongozi wa taifa hilo maskini ameyaonya na kuyashutumu vikali mataifa tajiri ya Magharibi kwa kuwa nyuma ya mpango huo wa Mashirika ya Haki za Binadamu Duniani; akiyatahadharisha kwamba kitendo hicho ni sawa na kumzukia Chatu mwenye njaa kali.

Katika hatua nyingine iliyoishangaza dunia ni kwamba duru zinasema kufuatia umaskini wa kupindukia unaokabili serikali ya nchi mkopaji na watu wake, taifa hilo tajiri barani Asia, limetangaza uhamiaji-huria (free entry without visa) kwa raia toka nchi mkopaji kwa sharti la kuuza magego yao wanapoingia kwenye taifa hilo tajiri na kupandikiziwa magego bandia.

Uamuzi huu wa taifa tajiri umezua mgogoro wa kidiplomasia na taifa mkopaji ambapo taifa mkopaji linajiandaa kupitisha sheria itakayowataka raia wake wote kukaguliwa magego mpakani na kudaiwa cheti cha taifa kitachoonyesha ni wapi uling’olewa magego ambapo wale watakaoshindwa kuthibitisha watashitakiwa kwa kuhujumu nyara za serikali (magego yao).

Adhabu itakuwa ni kufilisiwa mali ili kufidia mapato ya serikali yatokanayo na mauzo binafsi kwa siri ya magego hayo na kwamba serikali haitakuwa na uwezo wa kuwafunga jela maana taifa halina kasma ya kulisha wafungwa.

Lengo la sheria hii mpya ya nchi maskini ni kudhibiti uhamiaji haramu na halali wa raia wake kutorokea/kuhamia nchi hiyo tajiri ili kuuza magego yao (ambayo ni nyara za serikali yao) kwa nia ya kujipatia utajiri na kuondokana na umaskini uliowatesa kwa zaidi ya nusu karne bila serikali yao kuwa na jitihada zozote madhubuti na za makusudi za kuwaokoa na lindi la umaskini chini ya msitari.

Aidha, kwenye sheria hiyo mpya, serikali imesisitiza kwamba raia wake walio diaspora magego yao ni nyara za serikali yao hadi hapo watakapokana urai wa nchi yao.

Tetesi za sheria hii mpya zilizua wimbi kubwa la raia wa nchi hiyo maskini kuomba uraia wa nchi tajiri–mkopeshaji na kukana uraia wa nchi yao maskini ambapo serikali yao ililazimika kutunga kanuni mpya ya Uhamiaji inayoitaka idara hiyo kuridhia idadi ya watu wanaokana uraia wao wasiozidi watatu tu kwa mwaka kama namna ya kudhibiti wimbi hilo kubwa la raia wanaokana nchi yao hiyo maskini iliyotaifisha magego yao.

Na Douglas Majwala.

1640762273887.png

Serikali inachukuwa chake unabakishiwa chako.

1640762329213.png

Tayari serikali imeondoka na donge lake nono na unapandikiziwa bandia. Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa kiwango cha kuwa tayari kuifia kama mpiganaji kwenye medani.

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
View attachment 2061423
Serikali inachukuwa chake unabakishiwa chako.

View attachment 2061426

Alichotakiwa kufanya Mhe. Ndugai ni kupinga ilani ya chama wakati inaandaliwa kwamba italiingiza taifa kwenye madeni ya kuweza kuifanya ikanadiwa, kama chama kisingemsikiliza basi angeibana serikali Bungeni akipinga miradi hiyo ya thamani kubwa kuliko uwezo wa nchi, sasa mama afanyeje leo ambapo miradi iko kwenye ujenzi? Job ana washauri wote wa kisekta walitakiwa wawe wanamuandaa Spika vizuri katika kila anachokifanya na kukisema. Ukim-fire Job fire na washauri wake.
 
Inatisha!
 
Umemwelewa mghani au? Nimegundua kuna shida sana kiwa na fellowship na watua mbao hawajui tafakari tunduizi...Critical thinking...
 
Back
Top Bottom