Kauli ya Naibu Waziri Katambi itoshe kufukuzwa kazi

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,657
6,909
Ni fedheha na aibu kubwa kwa naibu waziri ndugu Katambi kutoa majibu yale ya kudhalilisha vijana wa nchi hii Kwa swali aliloulizwa.

Kujibu kuwa vijana ambao hawajafanikiwa kupata mikopo inayotolewa na halmashauri watokako kutokana na fedha kidogo zinazokusanywa na halmashauri ama wingi wa vijana wenye uhitaji kuwa sio wazawa wa Tanzania au ATI ni wakenya haivumiliki na itoshe aiachie ofisi na nafasi yake na ikimpendeza CCM imvue ubunge anaoringia.

Nawashangaa UVCCM wameuchuna kana kwamba kauli hiyo ya Naibu Waziri ni pambio la kusifu na kuabudu.

Mh. Rais Yale mabega uliyoonya yasipandishwe Katambi kaipuuza na kulinanga kundi kubwa la wapiga kura wako ambao kimsingi wanataabika kwa shida mbalimbali zikiwemo kufukuzwa maeneo wanakofanyia shughuli zao na kuharibiwa mitaji Yao ambayo serikali haijui waliipataje.

Nitakushangaa Sana wewe Mh. Rais na UVCCM kumvumilia Naibu Waziri Katambi kwani amejidhihirisha wazi kuwa kati ya viongozi wanaokuhujumu na kukuchonganisha wewe na vijana ambao Kwa wingi wao wakiamua kujibu mapigo itakuwia vigumu mno kuwatuliza! Mtimue aende zake.
 
Ni roho mbaya tu inakusumbua.
Wewe ndiye Katambi?

Unawezaje kutoa kauli ya kijinga vile? Hapo kwenye halmashauri Yako umewahi kupata mkopo tajwa? Na je, ni vijana wote wanaoomba mikopo hiyo hupata? Au wanaokosa ndio hao wakenya? Jiuzulu TU huo unaibu waziri Kwa kuwakosea vijana wazalendo na wavumilivu wa nchi hii!

Huenda naibu waziri umechagua kumvuruga mh. Rais na kuivuruga nchi Kwa kuwananga vijana! Ondoka zako na utaondoka TU Kwa nguvu ya vijana sisi kutoka Kenya!
 
Kale kamtu kanaonekana kashamba sana, kamejaa majivuno na ujinga tuu, huyu na kina Makonda, Sabaya sijui waliwaokota wapi?
 
Waanze kumfukuza Mwigulu Kwanza aliyesema watanzania wasiotaka tozo wahamie Rwanda.
Alisema Burundi, asingeweza kutaja Nchi ya maana yuko makini sana yule Jamaa.

Kwa uzuri gani mlionao Wabongo mpaka awatakie yenye kheri, huenda hata alitamani kusema tuende motoni.
 
Wewe ndiye Katambi?

Unawezaje kutoa kauli ya kijinga vile? Hapo kwenye halmashauri Yako umewahi kupata mkopo tajwa? Na je, ni vijana wote wanaoomba mikopo hiyo hupata? Au wanaokosa ndio hao wakenya? Jiuzulu TU huo unaibu waziri Kwa kuwakosea vijana wazalendo na wavumilivu wa nchi hii!

Huenda naibu waziri umechagua kumvuruga mh. Rais na kuivuruga nchi Kwa kuwananga vijana! Ondoka zako na utaondoka TU Kwa nguvu ya vijana sisi kutoka Kenya!
Una vigezo?

Umeomba?

Haujapata?
 
Ni fedheha na aibu kubwa kwa naibu waziri ndugu Katambi kutoa majibu yale ya kudhalilisha vijana wa nchi hii Kwa swali aliloulizwa.

Kujibu kuwa vijana ambao hawajafanikiwa kupata mikopo inayotolewa na halmashauri watokako kutokana na fedha kidogo zinazokusanywa na halmashauri ama wingi wa vijana wenye uhitaji kuwa sio wazawa wa Tanzania au ATI ni wakenya haivumiliki na itoshe aiachie ofisi na nafasi yake na ikimpendeza CCM imvue ubunge anaoringia.

Nawashangaa UVCCM wameuchuna kana kwamba kauli hiyo ya Naibu Waziri ni pambio la kusifu na kuabudu.

Mh. Rais Yale mabega uliyoonya yasipandishwe Katambi kaipuuza na kulinanga kundi kubwa la wapiga kura wako ambao kimsingi wanataabika kwa shida mbalimbali zikiwemo kufukuzwa maeneo wanakofanyia shughuli zao na kuharibiwa mitaji Yao ambayo serikali haijui waliipataje.

Nitakushangaa Sana wewe Mh. Rais na UVCCM kumvumilia Naibu Waziri Katambi kwani amejidhihirisha wazi kuwa kati ya viongozi wanaokuhujumu na kukuchonganisha wewe na vijana ambao Kwa wingi wao wakiamua kujibu mapigo itakuwia vigumu mno kuwatuliza! Mtimue aende zake.
Naunga mkono hoja,Mamlaka ya Uteuzi ifanye yake
 
Akili za huyu kijana zimeenda na mwendazake.
 
Back
Top Bottom