Kauli ya Mwigulu Nchemba yaiponza Serikali

Mangapi CCM wametuhumiwa nayo chadema hawajafuta kwa nini muhimu kufuta kauli katika hili tu??????????? JK dhaifu tulikataa kufuta.... haijakaa vizuri.

Mama Porojo naanza kuhisi una undugu na (Mh.) Sophia Simba. We kila siku unaongeaga pumba tuuuuuuuuuu.
Mnyika alisema kauli yake haifuti na akamwambia Ndugai kuwa hata kama atahitaji uthibitisho atampatia. Ndugai akaamua kumtoa nje. sasa ulitaka asemee kwenye gari yake nje?

huyu Mwigulu ni kiazi. wenzie wanaipigania CCM kwa step. akajifunze kwa Nape. Leo anaitetea CCM kesho anaiponda kidogo. Sasa yeye anatetea tuu mpaka upuuzi. Ukikutana nae mwambie, juzi wakati anaitupa bajeti ya upinzani alisema kwenye OC kuna na hela kwa ajili ya malalamiko ya Drs ili wasigome. jana bosi wake Pinda anasema ataenda mahakamani kuzuia mgomo.

huo ni zaidi ya udhaifu. nikitoa neno langu nahisi ntapigwa Ban.
 
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimeitaka Serikali ithibitidhe ama kukanusha habari aliyoisema mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu Nchemba aliyoitoa huko Dodoma kuwa wapinzani wanasukumwa na nchi za nje kuipinga bajeti ili kuleta machafuko nchini ili kuja kuchota mali asili zetu(gesi/madini et.c)Tamko Hilo limettolewa na John Mnyika mkurugenzi na habari akimtaka waziri Membe alithibitishe hilo Kama ndio kauli mbiu ya Serikali na chama ccm.

Source;gazeti la Majira

Huu ni mwendelezo wa propaganda chafu dhidi ya cdm!
Yaleyale ya makomandoo kuingizwa nchini na cdm kuchochea vurugu.
USHAURI WANGU KWA CCM.
Wajitahidi kujenga hoja za ukweli,hata kama itamaanisha wao kushindwa,kwani propaganda chafu zitasukuma nchi yetu kwenye matatizo.
 
Neno foolish umelitumia wewe, maadili yangu hayaniruhusu kuita comment ya mtu foolish...
Sio kila habari ni habari ya kuandikwa kwenye magazeti...
Mwigulu juzi aliponda bajeti ya upinzani kwa kusema kuwa wapotosha taifa na kutafuta umaarufu. Ndani ya masaa 24 anabadilisha kauli na kusema wanakosoa bajeti kwa interest za mataifa ya magharibi. Haihitaji elimu kubwa kupambanua kuwa Mwigulu is now insane na anaongea nonsense...
Kule Arumeru ni Mwigulu aliyesema kuwa CDM wanafadhiliwa na vyama vya kishoga vya magharibi. Alitakiwa athibitishe,hajaweza hadi leo.
Leo anarudia tena pumba zile zile, na mwandishi anakurupuka kwenda kuandika kama habari. Eti wewe unasema kinachotakiwa ni Mwigulu athibitishe!!! Are you really using your mind?
Akili ya Mwigulu haitofautiani sana na akili ya SHIBUDA!!
Huwezi kubishana na Chizi!! ambaye hakumbuki dakika chache zilizopita alisema nini....

SHIBUDA: Nataka JK awe meneja wangu wa Kampeni..........muda mfupi baadae...Nataka Dr. Slaa awe meneja wangu wa kampeni

NCHEMBA: Budget ya upinzani ni rubbish.............dakika chache baadae..........CHADEMA wanasaidiwa na nchi za magharibi ili waje kuchukua gas yetu....

Pumbavu zake huyu dogo......sasa hivi serikali ya CCM inasaidiwa na nani kuuza rasilimali zetu hovyohovyo??

Nani anawasaidia kuuza twiga wetu??.........Mtu dhaifu ki mtizamo na kupambanua mambo kama Nchemba ni hasara kubwa sana kwa Taifa hili........A TOTAL WASTE!!! hata hafai kutengenezea Compost!!!
 
What a foolish coment! Hivi hiyo haikuwa habari? Sasa ipi ni habari kwa gazeti. Kusema kwamba chama kikubwa cha upinzani nchini kinafanya kazi kwa msukumo wa mataifa ya nje na sio matakwa ya wananchi ni habari ambayo wananchi wanapaswa kufahamishwa. Anachotakiwa Mwigulu ni kuthibitisha, akishindwa ni aibu kwake na chama chake, akiweza ni aibu kwa cdm. Wananchi tutatoa hukumu. Otherwise ni hatari sana kwa chama kuongozwa kwa remote kutoka mataifa ya nje badala ya wananchi wake!

Filipo + Nchemba = VAPOUR
 
Hii issue si ndogo kama mnavyofikiria. Inaweza kumfanya Mwigilu aitwe na chama chake athibitishe hayo maneno yake.
 
'USOMI' WA MWIGULU, KAULI NA MIENENDO YAKE KATIKA MEDANI YA SIASA HUACHA CHACHU NA UVUNDO MZITO MIDOMONI KITAIFA

Kuhusu USOMI wa Mwigulu Nchemba na
'A' katika uchumi ambao unatembezwa katika kila jukwaa la siasa hapa nchini hivi sasa huku akibubujika kauli zisizoendana hata kidogo na hayo madai USOMI ILIOTUKUKA, WaTanzania tujiulize mara mbili mbili juu ya huyu kijana si bure na tukamsikilize nini alichokisema Mzee Wasira juu ya huyu mwenzetu.

Hakika kama usomi wenyewe ndio kama huu wa Mwigulu Nchemba na hizo busara tunazozisikia hivi sasa toka kwake, wala sipati shida zaidi kujua kwa nini katika taifa letu Umatonya unaendelea kutung'ang'ania kama ruba kihivi kila kukicha!!

Katika akili ya huyu kijana, aina ya lugha anayotumia na mienendo yake kwa ujumla tulivyoshuhudia kwenye kampeni za kisiasa ndani ya mipaka yetu, nasema KUNA TATIZO KUBWA mno pale ambalo lisipodhibitiwa mapema huenda ikatugharimu kama taifa.
 
Back
Top Bottom