Kauli ya Mwigulu Nchemba yaiponza Serikali

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,558
7,156
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema kimeitaka Serikali ithibitidhe ama kukanusha habari aliyoisema mbunge wa Iramba mashariki Mwigulu Nchemba aliyoitoa huko Dodoma kuwa wapinzani wanasukumwa na nchi za nje kuipinga bajeti ili kuleta machafuko nchini ili kuja kuchota mali asili zetu(gesi/madini et.c)Tamko Hilo limettolewa na John Mnyika mkurugenzi na habari akimtaka waziri Membe alithibitishe hilo Kama ndio kauli mbiu ya Serikali na chama ccm.

Source;gazeti la Majira
 
Mi naona kama catalyst kwenye haya malumbano uchwara ni gazeti la Majira. Hawakuwa na sababu ya kuandika pumba alizoongea Mwigulu juzi walipomhoji. Hili gazeti limekuwa kama la udaku vile...
 
Itakuwa vizuri people have to take accountability for their words,watu wanaropoka 2 inabidi watu wafundishwe nidhamu ya kuongea,
 
Mwigulu ni wale vijana Malimbukeni. Sijui lini ushamba utamtoka. Eti "SPESHO" Nikapata A nikasoma Masters nikapata A ptuuuuuu my Foot. Huyu dogo ni bonge la mshamba
 
Ngoma ndiyo imeanza, sasa tuangalie ni hatua gani za kinidham atachukuliwa
 
Alete ushaidi kuiokoa nchi bcs cdm wanaweza chukua nchi wananchi tukijua mchemba alilopoka tu.
 
Mi naona kama catalyst kwenye haya malumbano uchwara ni gazeti la Majira. Hawakuwa na sababu ya kuandika pumba alizoongea Mwigulu juzi walipomhoji. Hili gazeti limekuwa kama la udaku vile...

What a foolish coment! Hivi hiyo haikuwa habari? Sasa ipi ni habari kwa gazeti. Kusema kwamba chama kikubwa cha upinzani nchini kinafanya kazi kwa msukumo wa mataifa ya nje na sio matakwa ya wananchi ni habari ambayo wananchi wanapaswa kufahamishwa. Anachotakiwa Mwigulu ni kuthibitisha, akishindwa ni aibu kwake na chama chake, akiweza ni aibu kwa cdm. Wananchi tutatoa hukumu. Otherwise ni hatari sana kwa chama kuongozwa kwa remote kutoka mataifa ya nje badala ya wananchi wake!
 
Wakuu siku hizi nashindwa kuandika kwasababu kila nikijaribu tu haifikii mchana au usiku kabla sijala ban

Pole mkuu, sikuhizi kila neno linaudhi! Hata ukisema raisi ni dhaifu, kanuni zinakushukia!
 
Mi naona kama catalyst kwenye haya malumbano uchwara ni gazeti la Majira. Hawakuwa na sababu ya kuandika pumba alizoongea Mwigulu juzi walipomhoji. Hili gazeti limekuwa kama la udaku vile...

Mkuu kwa nini tuilaumu catalyst wakati tunaiacha source yenyewe? suala ni ku deal na Nchemba perpendicularly!
 
Mi naona kama catalyst kwenye haya malumbano uchwara ni gazeti la Majira. Hawakuwa na sababu ya kuandika pumba alizoongea Mwigulu juzi walipomhoji. Hili gazeti limekuwa kama la udaku vile...

Unalolisema ni sahihi lakini tayari gazeti limeandika na wapo baadhi ya wananchi walioamini habari ile,hiichi walichofanya Chadema ni sahihi na hili pengine litapunguza wale waropokaji ovyo Wa mambo dhidi ya vyama vingine
 
Mi naona kama catalyst kwenye haya malumbano uchwara ni gazeti la Majira. Hawakuwa na sababu ya kuandika pumba alizoongea Mwigulu juzi walipomhoji. Hili gazeti limekuwa kama la udaku vile...

nakubaliana nawe mkuu. ile habari ilikuwa nyepesi na ya kidaku. haina lolote chochote. nilitegemea ingekuwa kwenye uhuru si majira. binafsi imenifanya nipunguze thamani ya gazeti la majira.
 
Mbona hayo Madini tayari yanachukuliwa hata bila faida yoyote kwetu na ni chini ya wachumi kama yeye alivyojigamba na Chadema ndio wanaopiga kelele juu ya hilo? Iweje wasukumwe wao na mataifa ya nje ili walete machafuko ili hayo mataifa yaje kuchukua madini?
 
Huyu mwigulu ni chemba kumjadili mnampa ujiko

Mkuu, apate ujiko mara ngapi? mumpe ujiko mara ngapi? mbona mshampa na sasa anapeta nyie ndo mnabaki kupiga kelele zisizo na mashiko tu humu?
 
Mkuu, apate ujiko mara ngapi? mumpe ujiko mara ngapi? mbona mshampa na sasa anapeta nyie ndo mnabaki kupiga kelele zisizo na mashiko tu humu?

Duh? Hivi anapata ujiko kusemwa vibaya? Hii nayo kali!
 
Back
Top Bottom