Kauli ya Mwigulu kuwa sio shimo lililosababisha ajali ni mwendo wa dereva wa Fuso ni ya kizembe

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,743
Juzi hapa ajali ilitokea kati ya lori la Fuso na basi la City Boys katika harakati za dereva wa Fuso kukwepa shimo barabarani na kuingia upande wa basi na kusababisha wagongane uso wa uso, na watu 12 kufa na 46 kujeruhiwa.

Nilisema humu JF kwamba ajali zinazosababishwa na mashimo barabarani yanayoachwa muda mrefu, TANROADS wanapaswa kushitakiwa. Na kauli hii imerudiwa tena na Mbunge wa Ulanga Mashariki Goodluck Mlinga kuwa TANROADS wawe wanapigwa faini kwa ajali zinazosababishwa na vitu kama mashimo yasiyofukiwa kwa kuwa na wao wanafanya uzembe. Mbunge Mlinga alisema pia TANROADS wanapenda sana kubambikiza watu faini zisizoeleweka wakati upande wao wanafanya uzembe wa kutorekebisha barabara.

Waziri Mwigulu alijibu kauli ya Mbunge Mlinga kwamba ajali hiyo haikusababishwa na shimo bali mwendo mkali wa dereva kwa kuwa magari mengine hayakupata ajali sehemu hiyo!

Kauli hii ya Mwigulu ni ya kizembe haistahili hata kutolewa na mtu ambaye anajiita msomi na kupewa daraka la kuwa waziri. Ni kauli ya kizembe kwa sababu inatetea uzembe wa TANROADS dhidi ya maisha ya Watanzania na mali zao. Najiuliza;
  1. Mwigulu anajuaje kama mwendo wa Fuso ulikuwa kasi? Ukiwa dereva hata kama uko mwendo wa 50km/hr ukakutana na shimo mara nyingi instinct ya kwanza ni kulikwepa. Na hata akimshitaki dereva wa Fuso kwa mwendo kasi, ni uthibitisho gani anao kwamba alienda mwendo kasi, na mwendo kasi wa kiasi gani?
  2. Kusema mbona magari mengine hayakupata ajali hiyo sehemu, je Mwigulu anataka kutuambia kwamba kila gari lililopita hiyo sehemu ya shimo lilipita kukiwa na gari nyingine upande wa pili? Anataka kusema kwamba hata kama kusingekuwa na basi upande wa pili Fuso ingepata ajali?
  3. Mwigulu anasema dereva wa Fuso alipaswa kupunguza mwendo kwenye hili shimo - je Mwigulu bado anatutarajia Watanzania tuelewe na kukumbuka kila shimo lililopo katika barabara za TANROADS ili tupunguze mwendo kila tunapokaribia sehemu yenye shimo?
  4. Kama Mwigulu ni msomi wa kweli basi anajua theory ya cause-effect; anachotaka kusema ni kwamba kama pasingekuwa na shimo na dereva wa Fuso akawa na spidi ile ile aliyokuwa nayo katika ajali hii, pangetokea ajali? Kwa hiyo nini kimesababisha ajali hapa, spidi au shimo?
Nachukua nafasi hii kuungana na Mbunge Mlinga kwamba TANROADS waanze kushitakiwa na hata kupgwa faini kwa uzembe wa kusababisha ajali kwa kushindwa kuchukua hatua kama kufukia mashimo wanayoacha muda mrefu barabarani. Hatuwezi kuruhusu uzembe wa namna hii unaofanywa na TANROADS uendelee kupoteza maisha ya Watanzania na wengineo, au kuwaacha wenye vilema vya kudumu au majeraha makubwa huku viongozi wetu wanaosema tunapaswa kuwa wazalendo na wachapa kazi wakitoa kauli za kizembe kuteteta uzembe wa TANROADS. Hili halipaswi kabisa kukubalika.

Refer:
TANROADS wanapaswa kushtakiwa kwa ajali na vifo vinavyotokana na ubovu wa barabara
 
TanRoads wabuni alama mpya ya barabarani,inayoonyesha kuwa mbele kuna shimo.Ili madereva wapunguze mwendo mapema ili kuepusha ajali.
Hiyo nguvu na bidii ya kuweka alama barabarani kuwa mbele kuna shimo kwa nini isitumike kuyafukia hayo mashimo, hata kwa hatua za muda?

Wewe unakuta chupa iliyovunjia njiani ambayo inaweza kumjeruhi mtu akiikanyaga, badala ya kuiondoa unaamua uweke alama ya kuonya kuwa kuna chupa imevunjika njiani tahadhali?
 
Mwiguru sifa ya uwaziri mbona imeshamtoweka tangia lile tukio la Nape kunyooshewa bastolla hadharani mchana kweupe.
 
Mwigulu kaka mbona unazidi kuharibu hivi ndoto yako ya urais itatimia kweli kwa mtindo huu?
 
Hivi ukipita kwenye shimo na mwendo mdogo je tairi itapasuka?

Hata hivyo pia Tanroads why mnasubiri hadi ajali zitokee ndipo mfanye marekebisho ya barabara? Hamkujifunza kwenye ajali ya Majinjah pale Mafinga?
 
Mwigulu kaka mbona unazidi kuharibu hivi ndoto yako ya urais itatimia kweli kwa mtindo huu?
Ajabu hata mie huko nyumba nilimwona kama presidential material, hata nikamwandikia ujumbe binafsi juu ya hili kwamba anachotakiwa kupata ni experience kwanza na kwa sasa asubiri zamu yake baada ya Magufuri. Na nikamshauri apunguze munkari dhidi ya vyama vya upinzani. Sasa kwa kauli anazotoa siku hizi nina shaka sana na uwezo wake wa kuwa president.
 
Hivi ukipita kwenye shimo na mwendo mdogo je tairi itapasuka?

Mkuu, mwendo mdogo upi? Na unafanya assumption kwamba kila shimo tunajua lilipo? Kama umeendesha gari long trip utajua maana ya kukutana na shimo la ghafla katikati ya barabara upande wako. Au unataka tuwe tunaendesha 40km/hr Dar hadi Mwanza ili kuepuka kuingia shimo la ghafla?
 
Hiyo nguvu na bidii ya kuweka alama barabarani kuwa mbele kuna shimo kwa nini isitumike kuyafukia hayo mashimo, hata kwa hatua za muda?

Wewe unakuta chupa iliyovunjia njiani ambayo inaweza kumjeruhi mtu akiikanyaga, badala ya kuiondoa unaamua uweke alama ya kuonya kuwa kuna chupa imevunjika njiani tahadhali?
VIBAO VITAKUA BORA ZAIDI KULIKO KUYAFUKIA HAYO MASHIMO. NA FAIDA ZITAKAZO PATIKANA NI HIZI ZIFUATAZO:-
1:- WACHORAJI WATAPATA AJIRA,
2:-HARDWARE WATAUZA MATERIAL NA NA KULIPA KODI.
3:- MAFUNDI WATAPATA AJIRA ZA MUDA.
4:- TRAFIKI WATAKUEPO KILA KWENYE KIBAO KULIPISA FAINI, HII ITASAIDIA UCHUMI KUKUA KWA KASI NA KUPELEKEA UUNGWAJI MKONO WA SEREKALI YETU TUKUFU.
 
Ajabu hata mie huko nyumba nilimwona kama presidential material, hata nikamwandikia ujumbe binafsi juu ya hili kwamba anachotakiwa kupata ni experience kwanza na kwa sasa asubiri zamu yake baada ya Magufuri. Na nikamshauri apunguze munkari dhidi ya vyama vya upinzani. Sasa kwa kauli anazotoa siku hizi nina shaka sana na uwezo wake wa kuwa president.
kweli mkuu zamani wakati wa kikwete wakati ule kapewa wizara ya fedha alikuwa Safi Sana lakini nowadays mmmh kimeo.
 
Hiyo nguvu na bidii ya kuweka alama barabarani kuwa mbele kuna shimo kwa nini isitumike kuyafukia hayo mashimo, hata kwa hatua za muda?

Wewe unakuta chupa iliyovunjia njiani ambayo inaweza kumjeruhi mtu akiikanyaga, badala ya kuiondoa unaamua uweke alama ya kuonya kuwa kuna chupa imevunjika njiani tahadhali?
Pia mameneja na/au injinia wao wapewe petroli ya kutosha ili mara kwa mara(angalao mara moja kwa wiki) wawe wanatembelea barabara katika maeneo hao. Wakiona shimo linaanza kujitengeneza wawahi kulithibiti. Ikumbukwe crack ikianza maji yaki-percolate ardhi chini ya lami inalainishwa panatitia zaidi. Usipoziba UFA utajenga UKUTA.
 
VIBAO VITAKUA BORA ZAIDI KULIKO KUYAFUKIA HAYO MASHIMO. NA FAIDA ZITAKAZO PATIKANA NI HIZI ZIFUATAZO:-
1:- WACHORAJI WATAPATA AJIRA,
2:-HARDWARE WATAUZA MATERIAL NA NA KULIPA KODI.
3:- MAFUNDI WATAPATA AJIRA ZA MUDA.
4:- TRAFIKI WATAKUEPO KILA KWENYE KIBAO KULIPISA FAINI, HII ITASAIDIA UCHUMI KUKUA KWA KASI NA KUPELEKEA UUNGWAJI MKONO WA SEREKALI YETU TUKUFU.

Mmmh, Mkuu unaniacha hoi. Ni sawa na kusema tuache polisi waendelee kuua watu wasio na hatia kwa sababu zifuatazo
  1. Watengeneza majeneza watapata kazi
  2. Wauza mao watauza mbao
  3. Wenye magari watakodishwa kubeba maiti
  4. Wafanya biashara wa chakula na vinywaji watauza chakula na vinywaji kwa ajili ya msiba
  5. Idadi ya watu itaungua na kuokoa fedha za taifa
  6. Polisi wataendelea kuwa na ajira
 
Hiyo nguvu na bidii ya kuweka alama barabarani kuwa mbele kuna shimo kwa nini isitumike kuyafukia hayo mashimo, hata kwa hatua za muda?

Wewe unakuta chupa iliyovunjia njiani ambayo inaweza kumjeruhi mtu akiikanyaga, badala ya kuiondoa unaamua uweke alama ya kuonya kuwa kuna chupa imevunjika njiani tahadhali?
Hii sio ajali ya kwanza kusababishwa na mashimo, na tunaona uhalalishwaji Wa mashimo barabarani basi wayabunie alama mpya ya barabarani kuwa tembea km 80/h ila mbele kuna shimo.Kama kufukia hawawezi
 
VIBAO VITAKUA BORA ZAIDI KULIKO KUYAFUKIA HAYO MASHIMO. NA FAIDA ZITAKAZO PATIKANA NI HIZI ZIFUATAZO:-
1:- WACHORAJI WATAPATA AJIRA,
2:-HARDWARE WATAUZA MATERIAL NA NA KULIPA KODI.
3:- MAFUNDI WATAPATA AJIRA ZA MUDA.
4:- TRAFIKI WATAKUEPO KILA KWENYE KIBAO KULIPISA FAINI, HII ITASAIDIA UCHUMI KUKUA KWA KASI NA KUPELEKEA UUNGWAJI MKONO WA SEREKALI YETU TUKUFU.
Sana mkuu
 
Kwa mara ya kwanza Mlinga kaongea point...Kuna mashimo mengi sana barabarani na yanaharibu magari na kusababisha ajali hasa kwa madereva wanaopita njia mpya....unakuta barabara imenyooka mara unakumbana na shimo
 
Hii sio ajali ya kwanza kusababishwa na mashimo, na tunaona uhalalishwaji Wa mashimo barabarani basi wayabunie alama mpya ya barabarani kuwa tembea km 80/h ila mbele kuna shimo.Kama kufukia hawawezi
Haa! Mkuu, ukiwa 80km/hr ukakutana na shimo la ghafla upande wako na upande wa pili kuna gari bado tatizo liko pale pale! Na usifikiri Fuso na Corola zinasimama kwa namna moja. Ukiwa na Fuso kufunga breki za ghafla ni hatari, kuliingia shimo ni hatari, kulikwepa ni hatari.

Suala ni kwamba barabara zetu hazipaswi kabisa kuwa na mashimo ambayo dereva atakutana nayo ghafla, na TANROADS wanajua ni sehemu zipi za barabara kukiwa na shimo linakuwa ni hatari kwa watumiaji wa barabara.
 
Back
Top Bottom