Kauli ya mwana siasa huyu huwa nikiikumbuka nafurahi sana

Big Eagle

JF-Expert Member
May 3, 2020
592
625
"Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu maana hakuna namna nyingine wote lazima tukubaliane nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria sasa kama wewe unakaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndie jeuri zaidi watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu, kwasababu hakuna namna nyingine"

CHADEMA walipiga sana wakapiga kelele sana sasa walichokifanya wao kwa wabunge wao kuwatimua kina tofauti gani na kauli hii!!! Ndo maana huwa naipenda sana.

Mmeambiwa acheni kutupa pleasure na taarifa za uongo za corona tulieni na fuata maelekezo bado mnakaidi...
 
JK nae alikuwa ni wale wale tu sema hakujiachia kama huyu aliejisahau kupitiliza.

Ukiacha kauli hii ya Pinda aliyoitoa Bungeni,watu kama kina Mwigulu walitumika vibaya sana kuhujumu na kunyanyasa wapinzani na upinzani kwa ujumla na waliachwa utadhani walikuwa juu ya sheria.
 
Ccm haijawahi kuwa na watawala wenye akili, Pinda mwenyewe ndio mfuasi mkuu wa utawala huu anatumwa mpaka china anamshauri jiwe kuongeza muda kiufupi hamna kitu alipata u PM kwa ushawishi wa TISS kumbeba membe wao tu.
 
Jinsi mnavyosapoti ccm ndivyo mnavyozidi kuchelesha maendeleo yenu.
 
Back
Top Bottom