Uchaguzi 2020 Kauli ya Msigwa kuhusu Urais na kumuachia jimbo Steve Nyerere

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1591365287346.png

MBUNGE wa Iringa Mjini kupitia CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa, baada ya kueleza kuwa anayo nia ya kugombea nafasi ya Urais ndani ya chama chake, amepata kigugumizi kulijibu swali la kwamba hivyo ndivyo ataachana na wananchi wake endapo ataingia kwenye nafasi kubwa ya Urais.

“Ni kweli nimepeleka barua siku ya jana, mimi sijasema kwamba nataka kuwaaga wananchi wa Iringa hayo ni maneno yako, halafu ukisema nataka kumkimbia Steve Nyerere kwani yeye ni nani, na ndani ya siku nne nitaongea na vyombo vya habari kueleza kwanini naitaka nafasi hiyo” amesema Mchungaji Msigwa.

Juni 3, 2020 Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alitangaza rasmi kufungua mlango wa watia nia ya kugombea nafasi ya Urais, waanze kupeleka barua ofisini kwake, zoezi ambalo litahitimishwa Juni 15, 2020.
 
View attachment 1469496

Big Up Msigwa kwa KUWAPIGISHA NGOMA WACHEZE MDUNDO wakija kustuka UMESHAINGA BUNGENI 2020-2025.
 
Hiv jaman Urais ushaakua mwepesi kiasi hiki? Yaani hata Msigwa anahisi kua anatosha kua Rais? Tuache utani jaman na haya mambo embu tuiheshimu nchi hii bwana alaah
 
Kaole ndiyo eti itunge sheria za nchi...hivi nchi hii imefikia kiwango cha chini sana cha dharau kiasi hiki
 
Back
Top Bottom