Kauli ya mkuu wa nchi kuhusu mgomo wa wafanyakazi;Ni ubabe au busara?

Kapo Jr

JF-Expert Member
Jan 31, 2011
996
280
Wana jf,nakumbuka wakati wa vuguvugu la wafanyakazi wa serikalini kutangaza mgomo wengi mtakumbuka kauli ya mkuu wa nchi aliposema,'mie ndiye mwajiri mkuu kwa upande wa watumishi wa umma,mkimfuata mgaya mtapoteza ajira zenu na mgaya hamtamuona tena"..nawasilisha kwenu wana jf kwani kila nikitafakari nakosa muafaka mchango wenu muhimu,naona matukio ya kutisha yanatokea kila kukicha,tuijadili kiundani kauli hii.

MY TAKE..ushabiki haufai ili tulinde vizazi vyetu
 
Nasubiri nione kama hao wafanyakazi wa Umma watavumilia Pension zao ziliwe na Ridhwan huku wao wakisubiri miaka 55-60 ya kustaafu
 
Kila niisikiapo kauli hii na kuichambua kisha kuilinganisha na umuhimu wa rais na majukumu yake hapa nadhani hakututendea haki watanzania wote,si wafanyakazi pekee kwani wafanyakazi hutumikia jamii yote,hivyo matamshi yenye utata yanaongeza /pandikiza chuki kwa wananchi mfano wanapokosa huduma stahiki,yawezekana ndo chanzo cha migogoro isiyokwisha serikalini
 
'mie ndiye mwajiri mkuu kwa upande wa watumishi wa umma,mkimfuata mgaya mtapoteza ajira zenu na mgaya hamtamuona tena"
Hii imekuwa kama yule ngamia aliyekuwa anaomba kwa unyrnyekevu aruhusiwe kuingia kwenye hema kujificha baridi. Aliomba kuruhusiwa aingize sikio, badae pua, kichwa, miguu....alipoingia mzima ndani ya hema akamtoa nje mwenye hema kwa mateke.

Hivi ndivyo anavyofanya Mkuu wa Nchi, asisahau kuwa Watanzania ndio waliomwajiri yeye kwa kumpara ridhaa ya kuongoza sio kutawala; leo anajisifu kuwa yeye ndiye mwajiri mkuu. Haya zake zimehamia kisogoni.
 
Kila niisikiapo kauli hii na kuichambua kisha kuilinganisha na umuhimu wa rais na majukumu yake hapa nadhani hakututendea haki watanzania wote,si wafanyakazi pekee kwani wafanyakazi hutumikia jamii yote,hivyo matamshi yenye utata yanaongeza /pandikiza chuki kwa wananchi mfano wanapokosa huduma stahiki,yawezekana ndo chanzo cha migogoro isiyokwisha serikalini
kama ufreemason ndivyo unavyolipa basi kila mtu atakuwa freemason. lakini iko siku ataanguka kama KANUMBA MSHIKAJI WAKE KWENYE KUNDI HILO KANDA YA TANZANIA
 
Wafanyakazi wote tumetoswa hasa wa kada za chini,maisha magumu na mkuu wa kaya hatutaki njia ni mgomo baridi,madkts karibu ss walimu ni wazoefu na matokeo ake mnayaona.
 
Unapokuwa kiongozi unatakiwa uwe strong na kauli zako, kwa hiyo rais ni shupavu sana. angekuwa mwingine nchi ingewaka moto. na Pinda naye ni moooooooooooto.
 
Wana jf,nakumbuka wakati wa vuguvugu la wafanyakazi wa serikalini kutangaza mgomo wengi mtakumbuka kauli ya mkuu wa nchi aliposema,'mie ndiye mwajiri mkuu kwa upande wa watumishi wa umma,mkimfuata mgaya mtapoteza ajira zenu na mgaya hamtamuona tena"..nawasilisha kwenu wana jf kwani kila nikitafakari nakosa muafaka mchango wenu muhimu,naona matukio ya kutisha yanatokea kila kukicha,tuijadili kiundani kauli hii.

MY TAKE..ushabiki haufai ili tulinde vizazi vyetu
hapo kwenye bold/red unataka kusema nini mkuu, kutomuona kwa kuhamishiwa kwenye 'mahandaki' ya Mabwepande au!!??
 
hapo kwenye bold/red unataka kusema nini mkuu, kutomuona kwa kuhamishiwa kwenye 'mahandaki' ya Mabwepande au!!??
hapo nabaki dillema,cjui lengo na mantiki yake mkuu kwa wananchi ikiwa yeye ndo kiongozi wa juu kabisa
 
"....mkimfuata mgaya mtapoteza ajira zenu na mgaya hamtamuona tena"..

MY TAKE..ushabiki haufai ili tulinde vizazi vyetu

Nmimi nadhani statement ile ilikuwa inatabiri issue hii ya madaktari....some Drs.wamefukuzwa kazi, and Mgaya is Ulimboka ambaye ameponea chupuchupu! Huyu ni chinja chinja, kwa mambo haya bado ninaamini serikali inahusika na Dr.Ulimboka saga
 
Back
Top Bottom