Kauli ya Mkapa yarudiwa--"Msiwe wavivu wa kutafiti"

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Siku ya November 24, 2001, Rais Mkapa alipokuwa anatunuku degree huko SAUT jijini Mwanza, aliwaasa wahitimu wa Journalism kwamba waingie mtaani wakiwa ni watu wanaoandika wakionyesha kwamba ni watu wanaojua kufanya research kabla ya kuandika.

Akaonya kwamba matunda ya chuo hicho yasiwe ni kutoa waandishi ambao ni WAVIVU WA KUTAFITI. Maneno haya matatu ya mwisho yaani WAVIVU WA KUTAFITI yaliwakera watu wengi yakazua mjadala kwa watu hata wasio waandishi kwamba watu wamekejeliwa kuwa ni wavivu wa kutafiti kana kwamba Mkapa alikuwa mwongo katika hilo.

Juzi tena, katika mazingira kama yaleyale aliyotamkia Mkapa, Pope Francis karudia kauli kama hii alipokuwa akiwahutubia student wa Universities mbalimbali za Rome, waliokuwa wamekusanyika pale Vatican.

Yeye kawaasa kama Mkapa kwa kuwaambia kwamba "wanatakiwa kuacha kuwa watizamaji tu bali wanatakiwa kuwa watu wa kuongoza jamii (protagonist) katika kufunua ukweli".

Kopi halisi ya alichosema Francis hiki hapa {Click Here}
 
Back
Top Bottom