Kauli ya Mkapa inatufundisha nini watanzania kuhusu viongozi wetu?

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Mkapa ni mmoja wa marais wenye msimamo ambao Tanzania imewahi kuwapata. Ni katika kipindi chake ndiyo Tanzania imeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiuchumi hasa katika kuuza na kubinafsisha mashirika ya uma. Kuna mazuri na mabaya anayotuhumiwa kuyafanya wakati wa utawala wake, hata hivyo unapokuwa kiongozi huwezi kumridhisha kila mtu kwani maadui hawatakosena kwa njia moja ama nyingine.

Ndiyo maana viongozi wetu wastaafu bado wanapatiwa huduma zote muhimu ikiwemo ya kulinda maisha yao kutokana na maadui mbalimbali wanaojulikana na wasiojulikana. Kitendo cha Mkapa kutamka wazi kuwa anaogopa kusema ni maamuzi gani magumu aliwahi kuyatoa kwani "bado nataka kuishi" ni ishara mbaya kwa usalama wa viongozi wetu ambao wanatoa maamuzi kwa niaba ya watanzia wote siyo kikundi cha wa watu wachache.

Kwa maana hiyo basi sisi kama Taifa hatuna budi kuwalinda viongozi wetu kwa kutumia kila uwezo tulionao ili kuwafanya wasihofie maisha yao kwa sababu tu walichukua maamuzi magumu kwa faida ya nchi yetu kabla na baada ya kustaafu. Vinginevyo tutakuwa na viongozi "dummy" na hata puppet wakiangalia zaidi kulinda maisha yao kuliko kutumia taifa kwa moyo wa dhati bila hofu toka kwa mtu yeyote.

Nchi kama Tanzania inahitaji viongozi watakaokuwa tayari kutoa maamuzi magumu kwa faida ya watanzania bila woga, tukifikia hapo nina hakika kuwa Tanzania itasonga mbele. Utamaduni wa woga tuliona watanzania (wananchi na viongozi wetu) ni sababu kuu ya Taifa letu kuwa nyuma kimaendeleo, kwani hatuna uthubutu wa kufanya mambo kwa kuangalia masilahi watanzania walio wengi hata kama yatawauzi wachache wenye nguvu badala ya kufanya kwa kuangalia usalama na kiulaji binafsi.

My take: Watanzania tuwe na ujasiri, kwani hata baba wa taifa kwenye sherehe za CCM kitaifa 1988 pale Tabora Ali Hassan Mwinyi Stadium, alisema "Taifa lolote litakalokosa wananchi walio tayari kujitolea basi, taifa hilo lisahau kupata maendeleo". Kama mtanzania unaona huwezi kujitolea iwe maisha, nguvu, akili zako basi unakuwa umekosa sifa za kuongoza wengine kuelekea kwenye maendeleo. Viongozi wetu wanatakiwa kuwa ni watu waliojitolea zaidi ili kufanikisha lengo hilo, vinginevyo tutakuwa tunatumikia woga na vitisho toka kwa wahalifu wachache.

Kama mtu huwezi kutoa maamuzi magumu kwa hofu yoyote ukiwa kama kiongozi, Inakuwa ni jambo la busara zaidi kama utafuta mawazo ya kuomba "UONGOZI"- Kwani uongozi ni ujasiri ukiwa mwoga kila siku unaowaongoza watadhurika
http://www.globalpublishers.info/video/bado-nataka-kuishi-mkapa source GPL
 
Hivi umetafakari kwa kina kabla ya kutoa maoni yako? Vipi umfajilie mwizi wa mali ya umma? Kauza migodi, mashirika ya umma na karuhusu kuibuka kwa wimbi la wezi wa mabenki huyo ndiye Rais Mkapa unayemtetea
 
Haya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na ubinafsihaji wa mashirika ya umma ulimsaidia nani? Inasikitisha sana kuona viongozi wanakuja na kutoka maisha ya mtanzania bado ni ya kubangaiza! Miaka 50 ya uhuru, with all these people and the abundant natural resources, bado tunalia njaa, hospital ya maana hakuna, barabara vipande vipande reli iliyoachwa na mkoloni enzi za ujima ndio tegemeo la nchi yetu hata mita 5 hatujawahi kujenga! Uwanja wa michezo tumejengewa na wachina!

Unapoangalia nyuma, 10 good years! Wewe kiongozi unaona legacy gani uliyoacha! Sisi Wantanzania tutakukumbuka kwa lipi! How do you feel about that! Simply nil nil cherishable memory despite of many many unpleasant reminiscents!

Hawa viongozi wetu wanaupofu wa aina gani? Roho za aina gani? Je ubinafsi kweli ndio uko hivi? Kila kitu unataka utie mfukoni mwako? Its far beyond my comprehension!!!!!
 
Maamuzi magumu ni kukubali shinikizo la wana mtandao la kutaka apindishe utaratibu uliozoeleka kwenye mchakato wa kutafuta mgombea urais wa awamu ya nne pale Dodoma.

Mzee Karugendo katika makala yake ya Jumapili kwenye Gazeti la Tanzania Daima ameelezea vizuri juu ya uongozi wa Mkapa. Naomba nimnukuu:

Tanzania Daima Jumapili 9/05/2010
Prudence Karugendo

WATANZANIA tuna mambo tunayoyafanya kwa kusukumwa tu na mazoea bila mazoea hayo hutuachia fursa ya kuupima umuhimu wa mambo yenyewe tunayohangaika kuyafanya.
Mfano, tumezoea kufanya Uchaguzi Mkuu kila baada ya miaka mitano. Huo ni utaratibu tuliojiwekea na baadaye ukazoeleka na kugeuka mazoea. Kwahiyo tumezoea kwamba kila baada ya miaka mitano tunafanya uchaguzi, hayo ni mazoea.
Kwa vile tumeishazoea hivyo hatujiulizi tunafanya uchaguzi ili iweje. Tunafanya uchaguzi kwa vile ni mazoea ya kila baada ya miaka mitano kufanya hivyo. Kwahiyo kinachojionyesha hapa ni kwamba umuhimu wa kufanya uchaguzi hauzingatiwi ila kinachozingatiwa ni mazoea ya kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.
Katika uchaguzi tuliozea kuufanya kila baada ya miaka mitano, kitu cha kwanza tunampata rais wa nchi. Tukishampata rais katika taratibu za kumtawaza ni lazima tumuapishe.
Vilevile kumuapisha rais nako tumeishakugeuza tendo lililo katika mazoea ambayo Waingereza huyaita ‘just formality'. Mazoea hayo yanatunyima fursa ya kuuelewa umuhimu wa kumuapisha rais.
Marais wetu wanaelewa kwamba tunawaapisha tukiwa hatutilii maanani umuhimu wa kitu hicho, ndiyo maana tunaona wanafanya mambo mengine yaliyo nje ya kiapo chao, bila woga wala wasiwasi wowote, wakiwa wameziegemea sheria za ajabu zinazowalinda.
Sheria kama zile za kuwa rais aliye madarakani au rais mstaafu haruhusiwi kushitakiwa. Iwapo kiapo hicho kingekuwa kinazingatiwa na kutiliwa maanani, sioni hizi sheria za kumlinda rais asishitakiwe akiwa madarakani au baada ya kustaafu zingetungwa kwa ajili gani.
Rais angekuwa anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa utaratibu alioapa kuulinda. Kwa hiyo kama ingetokea mtu mkorofi akampeleka rais mahakamani, ingebidi rais aende akajitetee, maana yeye si Mungu, ili ukweli ubainike na ukorofi wa mtu husika uwekwe wazi.
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza, tunamuapisha rais ili iwaje kama hatuwezi kumshitaki akiwa madarakani au baada ya kustaafu? Na kwa nini rais akubali kuapishwa huku akielewa kwamba akishakuwa rais yeye ndiye mwanzo na mwisho wa kila kitu?
Kwa hiyo ni kwamba tunamuapisha kwa mazoea na yeye anakubali kuapa kwa vile tendo lile ni la mazoea tu, ingawa ukweli ni kwamba haliathiri chochote katika matendo ya rais akiwa madarakani. Vilevile rais anakuwa na uhakika kwamba kiapo hicho hakiwezi kuvuruga starehe zake baada ya kustaafu.
Hayo yote nayaongelea juu ya suala la kashfa zilizomzonga Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Yapo mawazo ya baadhi ya wananchi, mimi nikiwa mmojawapo, kwamba rais huyo mstaafu afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi zinazomkabili.
Inaonekana zinatengenezwa mbinu mbalimbali za kumlinda Mkapa ili asifikishwe kwenye vyombo vya sheria. Mbinu hizo ni nje ya sheria inayomkinga na mashitaka yanayotokana na makosa aliyoyatenda kwa kutumia wadhifa wake tuliomkabidhi kwa kiapo maalumu.
Katika mbinu za kumlinda Mkapa, wapo wanaodai kwamba tuyaangalie yale mema tu aliyoyatenda, kwa maana ya kwamba yanayoitwa mema yake yayafunike machafu yake.
Hawa watu wanadai ni ukosefu wa fadhila kumlaumu Mkapa kwa machache aliyoyakosea akiwa rais, badala ya kuyaangalia mema yote aliyoyatenda katika kipindi hicho.
Mimi nadhani wenye hoja hizo wanaghafilika katika sehemu fulani. Ni kwamba mtu anapokubalika kwamba ana uwezo wa kukabidhiwa dhamana fulani na kuilinda dhamana hiyo, halafu na yeye akakubali kuipokea, tena kwa kujiamini na kukubali kula kiapo, sioni kwa nini ziwepo fikra za kubahatisha. Sioni kama bahati nasibu ni mahali pake pale. Kinachokuwepo ni uhakika.
Kwa hiyo inapotokea mtu akatimiza kwa mafanikio kile kilichotazamiwa katika nafasi anayokuwa amekabidhiwa, sioni kwa nini ashangiliwe kama mtu aliyeshinda bahati nasibu ya kimataifa.
Hiyo ni kwa sababu aliaminiwa na yeye akajiamini kuwa ana uwezo wa kufanikisha jambo fulani, hilo tayari linakuwa ni deni. Kinyume chake ni kutafutana lawama.
Kitu kingine ni kwamba mtu hapaswi kupongezwa kwa kutekeleza wajibu wake, pongezi zinazotolewa katika hali hiyo ni za kiungwana tu, lakini si zile za kudai fadhila. Mtu anayepaswa kupongezwa ni yule anayekuwa amefanya kitu cha ziada. Kitu ambacho ni nyongeza ya yale aliyotakiwa kuyatekeleza.
Ndiyo, katika awamu ya tatu kuna mambo yametekelezwa yakaonekana zaidi ya maneno ya kuwalainisha wananchi na ahadi zisizotekelezeka kama ilivyo sasa, kama zile wapewazo vifaranga wa kuku kwamba watanyonya mpaka wakiwa wakubwa, lakini hata hivyo mambo hayo ni sehemu ya majukumu ya serilaki yoyote.
Yanaposhindikana kutimizwa, serikali inawajibika kujibu ni kwa nini. Na yanapotimizwa katika kiwango cha kawaida hayapaswi kuonekana maajabu.
Wapo wanaosema wakati wa Mkapa barabara nyingi zimetengenezwa, hilo ni sawa, ila ni katika kiwango cha kawaida tukichukulia kwamba asilimia kubwa ya barabara za nchi yetu hazijawa katika kiwango kinachoendana na karne hii tuliyomo ya 21.
Kwa hiyo kwa upande huo sioni kama kuna chochote kilichofanyika kiasi cha kutufunika macho tusiweze kuyaona maovu ya Mkapa kama inavyodaiwa na watetezi wake.
Pamoja na hiyo, bado pesa iliyotumika kuyafanya hayo tunayotakiwa kuyashangilia huku tukiwa tumeyafumbia macho machafu yote yaliyotendwa wakati ule, ni ya walipa kodi ambao ni sisi wenyewe.
Hata kama ni mikopo, wanaopaswa kuilipa mikopo hiyo vilevile ni sisi wenyewe. Kwa hapa ni kitu gani kinachoweza kumpa Mkapa sifa ya ziada?
Wengine wanasema aliweza kuongeza makusanyo ya kodi na kudhibiti mfumko wa bei. Mimi naamini kwamba huo ni wajibu wa kiongozi yeyote ambaye watu wanakuwa wamemuamini na kumpa jukumu la kuyasimamia na kuyalinda masilahi yao. Sioni kazi ya ziada iliyofanyika.
Tuelewe kwamba kukusanya ni tofauti na kutoa, Mkapa alikusanya kodi hakutoa au kuleta pesa kwa wananchi. Alikusanya kile kilichokuwa kinahitajika kukusanywa. Hilo lilikuwa jukumu tulilompatia tukiamini kwamba angelitimiza. Sasa kama aliweza kulitimiza maajabu yanatoka wapi?
Maajabu yangepaswa kuonekana iwapo Mkapa angeweza kufanya miujiza ya kuongeza kipato cha nchi kutoka kusikojulikana.
Wakati kuna wanaosema kwamba Mkapa aliongeza makusanyo ya kodi, wengine wanasema makusanyo ya Mkapa yalibaki katika tarakimu bila makusanyo hayo kuleta unafuu wowote kwa wananchi.
Ukali wa maisha kwa wananchi ulibaki uleule au kuzidi, pamoja na kuambiwa kwamba Mkapa anakusanya mabilioni ya shilingi kwa kila dakika.
Kwa mwananchi wa kawaida ni kitu gani anachopaswa kukishangilia katika hali kama hiyo?
Kodi zilikusanywa na kubaki kwenye tarakimu, mabilioni ya shilingi kila baada ya kipindi fulani. Tunaweza kusema kwamba pengine hiyo ilikuwa ni rekodi ya makusanyo, lakini cha muhimu ni lazima tuangalie makusanyo hayo yalitumika kufanya nini, kulipia rada?
Kununulia ndege ya anasa ya rais ambayo wananchi waliambiwa kwamba hata kama wanakula majani kama mbuzi ni lazima ndege hiyo ya rais inunuliwe?
Sikatai kwamba Mkapa alifanya juhudi za kukusanya kodi, swali langu ni kwamba kodi hiyo ilikusanywa kwa manufaa ya nani kama wananchi walibaki kuisikia tu kwenye tarakimu wakati wao wanatakiwa wakale majani?
Kauli ya kwamba "hata kama wananchi wanakula majani", ingewezaje kumtoka Waziri wa Fedha, Basil Mramba, katika hali ya neema inayodaiwa kutengenezwa na Mkapa?
Kauli ya kikatili kama hiyo inadhihirisha ni jinsi gani watawala walivyokuwa wamedhamiria kujistarehesha pasipo kujali ugumu wa maisha uliokuwa unawakabili wananchi.
Lakini bila aibu sasa hivi wanataka watuaminishe kwamba hali ilikuwa nzuri tena kupita kiasi!
Hivi kweli kuna mtu mwenye akili timamu anayepaswa kushangilia ukusanyaji wa kodi wa Mkapa wakati waziri wake wa fedha anadiriki kusimama bungeni na kutoa kauli ya kinyama kwamba ndege ya anasa ya rais ni lazima inunuliwe potelea mbali hata kama wananchi wanakula majani?
Hiyo ilitupa picha gani? Nashawishika kuamini kwamba kodi aliyokuwa anaikusanya Mkapa, kwa kutukamua hadi tone la mwisho la damu, huku wananchi tukitakiwa kula majani wakati pesa hizo zikifanya mambo wanayoyajua wao wakubwa, zilikuwa ni kwa ajili ya anasa zake binafsi na wateule wake wachache. Hivi kweli hicho ni kitu cha kushangiliwa na wananchi?
Nayasema hayo ili kuonyesha kwamba ukuta anaotaka kuutumia Mkapa na wale wote walio upande wake kuyaficha maovu yake aliyoyafanya akiwa rais ni wa kioo unaoonyesha uchafu wote ulio ndani.
Mambo yote yanayotumika kuukinga uovu wa Mkapa yakifanyiwa tathmini moja kwa moja nayo yatageuka uovu mwingine na kujiongeza kwenye uovu unaotakiwa kufunikwa.
Kwa hiyo ni bora wanaomtetea Mkapa wakatumia njia nyingine, kama kweli zipo, kuliko kutumia hizi zinazotutia kichefuchefu.Vinginevyo wakamwachie Mkapa akajitetee yeye mwenyewe. Hatutakuwa wa kwanza kufanya hivyo.
Kuna hoja nyingine za kwamba tunamkosesha Mkapa raha ya kustaafu, kwamba tukamuache apumzike. Ieleweke kwamba mahali pekee ambako mtu anapumzika kwa starehe ni kaburini. Lakini mtu ambaye bado yuko hai, anaendelea kuhesabika kama mtumishi, hoja ya kwamba tumuache apumzike kwa starehe au kwa amani hapa haipo kabisa!
Tunachokitafuta hapa ni tiba na kinga sawia. Tukiifanya tiba hii kwa Mkapa itakuwa ni kinga kwa rais aliye madarakani au ajaye asiweze kupatwa na tatizo kama lililompata Mkapa.
Tutakuwa tumemuepusha rais wetu na kuinusuru nchi yetu na matumizi mabaya ya madaraka.
Na kwa Mkapa, ambaye ni muamini mzuri wa Kikristo, kama anaamini kwamba anayotuhumiwa nayo si makosa yake ya kweli, basi akubali kusulubiwa kama alivyofanya Kristo ili nchi yetu ipate wokovu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi umetafakari kwa kina kabla ya kutoa maoni yako? Vipi umfajilie mwizi wa mali ya umma? Kauza migodi, mashirika ya umma na karuhusu kuibuka kwa wimbi la wezi wa mabenki huyo ndiye Rais Mkapa unayemtetea

Mkuu Fungu, naomba usiniweke kwenye fungu la watetezi wa Mkapa mi si "Chitarilo type" - kwa mweledi atakuwa amefahamu kuwa maoni yangu yana maanisha nini?. Always try to read between the lines mkuu, usiwe simple minded kiasi hicho. Asiyejua maana haambiwi maana.
 
Haya mapinduzi makubwa ya kiuchumi na ubinafsihaji wa mashirika ya umma ulimsaidia nani? Inasikitisha sana kuona viongozi wanakuja na kutoka maisha ya mtanzania bado ni ya kubangaiza! Miaka 50 ya uhuru, with all these people and the abundant natural resources, bado tunalia njaa, hospital ya maana hakuna, barabara vipande vipande reli iliyoachwa na mkoloni enzi za ujima ndio tegemeo la nchi yetu hata mita 5 hatujawahi kujenga! Uwanja wa michezo tumejengewa na wachina!

Unapoangalia nyuma, 10 good years! Wewe kiongozi unaona legacy gani uliyoacha! Sisi Wantanzania tutakukumbuka kwa lipi! How do you feel about that! Simply nil nil cherishable memory despite of many many unpleasant reminiscents!

Hawa viongozi wetu wanaupofu wa aina gani? Roho za aina gani? Je ubinafsi kweli ndio uko hivi? Kila kitu unataka utie mfukoni mwako? Its far beyond my comprehension!!!!!

Efraiz Pole sana mkuu, Mtu anapoongelea mapinduzi, anamaanisha ni mageuzi ambayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya
 

Kwanini Mkapa ana insist on private sector to be given first priority???

Na hawa wamiliki wa hizi private sectors ni asilimia ngapi ni wazawa kweli wa nchi hii na wasio na Raia mbili?

Je ni anakili kwamba katika uongozi wake na wa mwinyi ulishindwa kabisa kuja na mbinu mbadala wa kuikomboa nchi kiviwanda,Kilimo na Kiuchumi?

Wajua siwaelewi kabisa hawa viongozi wetu wao ni kushinda kwenda Ulaya tuuu na wanachorudi nacho ni porojoooo weeee na hakuna kitu kibasa wakirudi hawana cha ku implement wanchi wakione ni kusema tumeomba misaaada hiivi ni mpaka lini hii swala la kuomba misaaada lita kwisha? its a shame kwetu na viongozi wetu tunao wachagua kwakweli, eg JK alipo kuwa rais na ikawa ni safari nadhani ya kwanza au ya pili kwenda ulaya aliulizwa kwanini nchi yako ni maskini ingwa ina resources nyingi za kutosha na isiwe maskini akajibu hata yeye hajui kwani nchi inaendelea kuwa maskini. nashukuru mungu alijibu hilo swali nadhani hajui kweli ni kwanini nchi mpaka leo ni maskini regardless tuna resource za kumwaga.

ndio haya haya ya Ben ati bado nataka kuuishi it means when u tell the truth to ur people u'll be killed any time any where or u'll be threaten by a group of people who run this country sasa hii kwangu nasema there's no longer a free democracy in TZN's politics.
 
Machozi ya Mkapa!
Ex-president of Tanzania Benjamin Mkapa nicely summed up his experience and that of many other countries: "We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us."

Written by Roberto Savio / Inter Press Service
Wednesday, 19 August 2009 21:16

Maneno kwamba asibinafsishe bila uangalifu aliambiwa lakini akawa kichwa ngumu. Kumbuka baba wa Taifa alivyokemea kubinafsishwa NBC, lakini wapi.
Leo tumsifie mkapa eti kuna mambo mazuri ya kuhitaji sifa? Kama yapo ni machache na si muhimu sana, Kumbuka kila alivyoelezwa aliishia kutuita eti tuna wivu wa kike, ni wavivu wa kufikri nk. Leo yanajitokeza wazi yakiwemo ya rada (akin Slaa walipiga sana kelele lakini hawakusikilizwa), EPA ni kipindi cha mkapa nk.
Huyu CCM ikitoka madarakani kabla hajafa, hakika atakiona cha moto; hivyo visheria vya kumlida rais aliyestaafu wanavitafsiri vibaya; ni kwa makosa aliyofanya kwa manufaa ya nchi lakini yale aliyofanya kwa manufaa binafsi hayana kinga (kiwira)
-
How a president and his minister robbed the nation


-Using their powerful positions in government, Mkapa and Yona
sold 4bn/- coal mine to their own company for just 700m/-

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

NEW documents have surfaced showing that ex-president Benjamin Mkapa and his energy and minerals minister, Daniel Yona, sold the formerly state-owned Kiwira Coal Mines Limited to their own private company for a mere 700m/- in 2005 while the mine was actually built at a cost of over 4bn/-.
 
Ulimuelewa mwishoni alipoulizwa na mwandishi wa habari kuwa nini kifanyike? Alijibu TUWE WAAFRICA
Which means I guess determination. Think about it. Tusimlaumu tu huyu mzee kuna mengi alifanya hata kama kuna mabaya yalifanyika. Tunamlaumu kwa kufanya biashara akiwa Ikulu but kama mna data basi mnapaswa kujua kuwa Sindibadi wetu ana vitega uchumi vya maana sana A-Town subirini akitoka madarakani mtaona media itakanyopiga kelele!
 
Back
Top Bottom