Kauli ya Mdude Nyagali ni sahihi, ni muafaka na CHADEMA wasiingie mtego wa kuikana

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,090
Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza kijana mdude Nyagali, ameonyesha uthabiti wa nia wa kupambana na udikteta na uvunjifu wa sheria na katiba nchini.

Mdude ni aina ya vijana jeuri ambao mwalimu Nyerere alisema anataka kuwaona katika nchi hii, ambao wakimuona Bwana mkubwa anakosea basi wamuambie bila kupepesa jicho kuwa wamekosea!

Kauli thabit na Makbuli kabisa ya Mdude Nyagali kuwa, Iwapo Rais Samia ataendeleza mambo ya kidhalimu ya Mtangulizi wake basi wembe uleule aliotumua kumnyoa Magufuli atamnyoa nao Rais Samia, imewatoa mafichoni MATAGA na kuanza kumshambulia.

Mimi nina ushauri ufuatao kwa Chadema

1.Chadema isiingie katika mtego wa kumshambulia Mdude kwa kauli yake
Lengo la MATAGA na CCM ni kujaribu kuwaweka CHADEMA kwenye defensive mode, yaani badala ya kuendeleza madai halali ya msingi ya katiba mpya, basi CHADEMA ikae kujitetea kwa kauli isiyo na shida hata kidogo ya Mdude.

Wanachokifanya CCM ni kuwafanya CHADEMA watoke kwenye reli, waanze kujitetea halafu CCM watumie muda huo kujaribu kuwaconvince watu kuwa movement ya CHADEMA siyo ya Staha na hivyo by association ionekane kuwa madai ya katiba mpya hayana msingi

2. CHADEMA ishikilie hapohapo kwenye kauli ya Mdude na iuunge mkono waziwazi
CHADEMA iwaambie makada wake wake kuwa Waache kucheza ngoma ya CCM na hivyo waache kumshambulia Mdude.
Makada wa CCM wamewahi kutoa kauli mbaya mno huko nyuma zikiwemo za kupiga wanawake, kupiga wapinzani, Lini umewahi kuona kada wa CCM akiungana na Kada wa Chadema kukemea matamshi ya kada mwenzao wa CCM kwenye mitandao ya jamii?

CHADEMA iache wananchi wenyewe watoe comments juu ya hili suala lakini iwaombe Makada wake wawe thabiti na Waiunge mkono, kwa sababu ni kauli Thabiti ya kisiasa, Isiyo na matusi yoyote zaidi ya Emotion tu za watu ambazo CCM wanataka kuzitumia kudivert mjadala wa katiba mpya.

Kila mwanachadema asimame na aseme bila wasiwasi kuwa kama Samia ataleta udikteta basi wembe uleule uliotumika dhidi ya Magufuli utatumika kwa Samia pia!

3. Kauli ya Wembe kunyoa ni kauli ya kisiasa tu haina tatizo lolote
Haina tofauti na kauli ya Kepteni komba kwenye wimbo wake wa "Wembe ni uleule", Au Lissu akisema "tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea" , Au Nyerere akisema "Mtu anashauriwa na mkewe hatujui kesho atamwambia nini".

Kauli ya mdude siyo kosa la jinai, Ni tamathali ya semi tu aina ya tashbiha, ambayo anaufananisha wembe na "harakati" thabiti zisizoyumba za kupambana na udikteta nchini

4. Chadema inapaswa kuwa na Bad cops na good cops
Muacheni Mbowe awe good cop, atoe kauli za kidiplomasia, Lakini lazima wawepo watu ndani ya Chadema wenye kauli za Kukera madhalimu, Za kukera wasiotaka haki, Lissu anafanya kazi hii vizuri, Na wakitokea watu wa aina hii pia ni vizuri. Ndugu Wanachadema, Msimdekeze huyu mama, mpigeni Spana kwelikweli pindi akianza kufanya mambo ya ajabuajabu.

Kama nilivyosema, Wawepo watu wa siasa za kidiplomasia katika ranks zenu lakini wawepo watu wa kupiga spana zinazouma. Msimwendeshe kilainilaini huyu mama, maana hatotupa reforms zozote za maana zaidi ya kutupigisha marktime huku akifanya cosmetic changes.

5. Chadema ijiulize kwa nini CCM inamshambulia Mdude zaidi na si Lissu
Kwa sababu inajua, Wakimshambulia Lissu, Lissu atajibu forcefully, na hatorudi nyuma na atawaanika na atawashinda kawa hoja nzito. Kwa hiyo CCM inatafuta soft link ili kuigeuza launching pad ya mkakati wao wa kudiscredit movement yenu makini ya kudai katiba mpya.

Hivyo basi wanamshambukia Mdude kwa sababu ni easy target na wanatafuta uungwaji mkono wa haraka ili kujenga momentum na eventually kama nilivyosema kudiscredit movement yenu ya katiba.

Nashauri badala ya Uongozi wa Chadema kujidistance na Mdude basi imuunge mkono kauli yake, iitambue kauli yake na iiadopt agenda yake, Namna hiyo Chadema itawageuzi kibao CCM, Na Wananchi watajua kuwa CHADEMA iko serious kwenye kudhibiti udikteta na uvunjaji wa katiba nchini.

Ili CHADEMA iweze kuheshimika na kuonyesha kuwa inamaanisha biashara, Basi ionyeshe ungangari mapema.
kama Samia ataingia mtego na kufanya udikteta wa Kimagufuli ni kwa hasara yake yeye kisiasa na kwa chana chake, na eventually watakubali tu kuwa ni lazima kuheshimu katiba ya nchi

Mdude yuko sawa nampongeza sana kwa kauli yake thabiti
 
Instagram_post_by_BAVICHA_&_CHASO_•_Jul_4,_2021_at_11:15am_UTC%22_.jpg
 
Kauli ya Wembe kunyoa ni kauli ya kisiasa tu haina tatizo lolote.

Haina tofauti na kauli ya Kepteni komba kwenye wimbo wake wa "Wembe ni uleule", Au Lissu akisema "tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea" , Au Nyerere akisema "Mtu anashauriwa na mkewe hatujui kesho atamwambia nini".

Kauli ya mdude siyo kosa la jinai, Ni tamathali ya semi tu aina ya tashbiha, ambayo anaufananisha wembe na "harakati" thabiti zisizoyumba za kupambana na udikteta nchini
 
Kauli ya Wembe kunyoa ni kauli ya kisiasa tu haina tatizo lolote...
Naam, ni ya kisiasa tu.

CCM wanajua hiyo kauli haina Shida ila wanataka kuwageuzia kibao CHADEMA mbele ya umma kuwaportray kuwa ni mabully, yaani kujenga hisia kuwa wanamuonea Samia kwa sababu ni "mwanamke", kwamba hawana shukrani serikali yake imewafutia kesi (Japo ni mahakama anyway).

Kiufupi ni kuwa kama Samia katenda mazuri, basi ni wajibu wake na wala haipaswi kuonekana ni hisani. Kutenda kwake vizuri hakuzuii yeye kupewa makavu akizingua.

Samia akituzingua sisi Wananchi kwenye mambo ya haki zetu za msingi na sisi tutamzingua kweli.
 
CCM haijawahi kuzijibu hoja kwa hoja na haina Makada wenye uwezo wa kujenga hoja. Siku zote wamekuwa wakiwatisha watoa hoja. Wamekuwa watumiaji wazuri sana wa Vyombo vya Dola kuwaumiza wenye hoja zenye mashiko kwa lengo la kuwanyamazisha.

Suala la Katiba liko pale pale. Hawatafanikiwa kutuyumbisha bali watakuwa wanatujenga kisiasa zaidi.
 
Wananchi wanataka maendeleo...hizi siasa za mchongo Magu alishazizimaga sijui zimeludi kwa maslahi ya nani.
 
Haki na Uhuru na Demokrasia ni nyenzo kuu za maendeleo
Kama uanadhani maendeleo ni ugali, nguo na nyumba basi kajitafutie mwenyewe hakuna atakayekuletea ugali mezani
 
Very good analysis. Hujawahi niangusha. Kauli ya Mdude imewalaza na viatu juzi😅😅
 
Tunajiuliza tangu lini CCM wamekuwa na kauli nzuri,fikiria kauli za kina Kheri James kwamba tutampiga sindano za sumu Lissu,Fikiria kauli za kina Bulembo kwamba kina Zitto ni wasaliti wauawe na watu wakapiga makofi bungeni,Wakati Mbowe kashambuliwa waliongea maneno ya ajabu sana tena bungeni kwa kupeana muda.

Wakati Lowassa kahamia Chadema,kina Msukuma walimtukana matusi ya nguoni kabisa,Mara kajinyea,sijui mnapeleka maiti Ikulu

Mifano ipo mingi mno,sasa iweje leo wanashangaa kauli ambayo imetumia lugha ya picha tu?wamesahau yakwao?Mi nasema mbegu waliyopanda ndio imeanza kuota watulie tu,

What doesn't Kill you makes you stronger,

walipowafunga na kuwatesa wapinzani wajue kabisa ndio walikuwa wanawakomaza zaidi sasa wapambane tu waache kujificha hoja dhaifu.
 
Kwanza nichukue fursa hii kumpongeza kijana mdude Nyagali, ameonyesha uthabiti wa nia wa kupambana na udikteta na uvunjifu wa sheria na katiba nchini.

Mdude ni aina ya vijana jeuri ambao mwalimu Nyerere alisema anataka kuwaona katika nchi hii, ambao wakimuona Bwana mkubwa anakosea basi wamuambie bila kupepesa jicho kuwa wamekosea!

Kauli thabit na Makbuli kabisa ya Mdude Nyagali kuwa, Iwapo Rais Samia ataendeleza mambo ya kidhalimu ya Mtangulizi wake basi wembe uleule aliotumua kumnyoa Magufuli atamnyoa nao Rais Samia, imewatoa mafichoni MATAGA na kuanza kumshambulia.

Mimi nina ushauri ufuatao kwa Chadema

1.Chadema isiingie katika mtego wa kumshambulia Mdude kwa kauli yake
Lengo la MATAGA na CCM ni kujaribu kuwaweka CHADEMA kwenye defensive mode, yaani badala ya kuendeleza madai halali ya msingi ya katiba mpya, basi CHADEMA ikae kujitetea kwa kauli isiyo na shida hata kidogo ya Mdude.

Wanachokifanya CCM ni kuwafanya CHADEMA watoke kwenye reli, waanze kujitetea halafu CCM watumie muda huo kujaribu kuwaconvince watu kuwa movement ya CHADEMA siyo ya Staha na hivyo by association ionekane kuwa madai ya katiba mpya hayana msingi

2. CHADEMA ishikilie hapohapo kwenye kauli ya Mdude na iuunge mkono waziwazi
CHADEMA iwaambie makada wake wake kuwa Waache kucheza ngoma ya CCM na hivyo waache kumshambulia Mdude.
Makada wa CCM wamewahi kutoa kauli mbaya mno huko nyuma zikiwemo za kupiga wanawake, kupiga wapinzani, Lini umewahi kuona kada wa CCM akiungana na Kada wa Chadema kukemea matamshi ya kada mwenzao wa CCM kwenye mitandao ya jamii?

CHADEMA iache wananchi wenyewe watoe comments juu ya hili suala lakini iwaombe Makada wake wawe thabiti na Waiunge mkono, kwa sababu ni kauli Thabiti ya kisiasa, Isiyo na matusi yoyote zaidi ya Emotion tu za watu ambazo CCM wanataka kuzitumia kudivert mjadala wa katiba mpya.

Kila mwanachadema asimame na aseme bila wasiwasi kuwa kama Samia ataleta udikteta basi wembe uleule uliotumika dhidi ya Magufuli utatumika kwa Samia pia!

3. Kauli ya Wembe kunyoa ni kauli ya kisiasa tu haina tatizo lolote
Haina tofauti na kauli ya Kepteni komba kwenye wimbo wake wa "Wembe ni uleule", Au Lissu akisema "tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea" , Au Nyerere akisema "Mtu anashauriwa na mkewe hatujui kesho atamwambia nini".

Kauli ya mdude siyo kosa la jinai, Ni tamathali ya semi tu aina ya tashbiha, ambayo anaufananisha wembe na "harakati" thabiti zisizoyumba za kupambana na udikteta nchini

4. Chadema inapaswa kuwa na Bad cops na good cops
Muacheni Mbowe awe good cop, atoe kauli za kidiplomasia, Lakini lazima wawepo watu ndani ya Chadema wenye kauli za Kukera madhalimu, Za kukera wasiotaka haki, Lissu anafanya kazi hii vizuri, Na wakitokea watu wa aina hii pia ni vizuri. Ndugu Wanachadema, Msimdekeze huyu mama, mpigeni Spana kwelikweli pindi akianza kufanya mambo ya ajabuajabu.

Kama nilivyosema, Wawepo watu wa siasa za kidiplomasia katika ranks zenu lakini wawepo watu wa kupiga spana zinazouma. Msimwendeshe kilainilaini huyu mama, maana hatotupa reforms zozote za maana zaidi ya kutupigisha marktime huku akifanya cosmetic changes.

5. Chadema ijiulize kwa nini CCM inamshambulia Mdude zaidi na si Lissu
Kwa sababu inajua, Wakimshambulia Lissu, Lissu atajibu forcefully, na hatorudi nyuma na atawaanika na atawashinda kawa hoja nzito. Kwa hiyo CCM inatafuta soft link ili kuigeuza launching pad ya mkakati wao wa kudiscredit movement yenu makini ya kudai katiba mpya.

Hivyo basi wanamshambukia Mdude kwa sababu ni easy target na wanatafuta uungwaji mkono wa haraka ili kujenga momentum na eventually kama nilivyosema kudiscredit movement yenu ya katiba.

Nashauri badala ya Uongozi wa Chadema kujidistance na Mdude basi imuunge mkono kauli yake, iitambue kauli yake na iiadopt agenda yake, Namna hiyo Chadema itawageuzi kibao CCM, Na Wananchi watajua kuwa CHADEMA iko serious kwenye kudhibiti udikteta na uvunjaji wa katiba nchini.

Ili CHADEMA iweze kuheshimika na kuonyesha kuwa inamaanisha biashara, Basi ionyeshe ungangari mapema.
kama Samia ataingia mtego na kufanya udikteta wa Kimagufuli ni kwa hasara yake yeye kisiasa na kwa chana chake, na eventually watakubali tu kuwa ni lazima kuheshimu katiba ya nchi

Mdude yuko sawa nampongeza sana kwa kauli yake thabiti
Hiyo kauli ya wembe haina shida wala siyo tusi. Hata ccm wenyewe wameitumia Mara nyingi dhidi ya wapinzani.

Pili, rais ni mtumishi (siyo mungu) wa umma na analipwa kutokana na kodi za wote. Kama akikosea hataki kukosolewa aachane na kazi ya kutumikia umma
 
CHADEMA ikiikana kauli ya Mdude maana yake imechagua kauli lainilaini za kubembeleza, na itawapa shida huko mbeleni pindi ikilazimika kuwa wakali

Samia anatakiwa aambiwe maneno yote, wakati mwingine aambiwe ya upole kulingana na situation ya wakati huo, lakini wakati mwingine aambiwe ukwleli mchungu kwa maneno makali yenye kukera, yenye kukereketa ili aone kuwa ana wajibu wa kuongoza nchi kwa haki.

Ninaposema maneno makali simaanishi matusi,bali namaanisha maneno makali ya kisiasa!
 
Back
Top Bottom