nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
a
KITAIFA
[h=1]
SHARE[/h]
Na Diana Maningo
Posted Jumatano,Novemba28 2012 saa 10:11 AM
KWA UFUPI
Kama imefikia hatua mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi tena wa chama tawala akitaka kuandamana na wananchi kuchoma mgodi maana yake, Serikali imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi alisema Ngoto.
KAULI ya Mbunge wa Jimbo la Tarime ya hivi karibuni katika mkutano na wananchi mjini Tarime, Nyambari Nyangwine kuwa ataandamana na wananchi wake kutoka Tarime hadi Nyamongo kwenda kuchoma moto mgodi wa Africa Barrick Gold Mine, endapo mgodi huo utashindwa kuwalipa fidia wananchi waliofanyiwa tathmini ili kuhama maeneo yaliyojirani na mgodi yaibua mapya.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Tarime, Lucas Ngoto amemtaka Mbunge wa Jimbo hilo la Tarime, Nyambari Nyangwine awaongoze wananchi wakiwa na mapanga kwenda hadi Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kudai X-Ray ambayo imekosekana katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime kwa muda wa miezi 8 hali inayowalazimu wagonjwa kwenda mikoa ya jirani na nchini Kenya kupata huduma hiyo.
Ngoto alisema kuwa hashangai kusikia Mbunge Nyangwine akitaka kuandamana na wananchi kwenda kuchoma moto mgodi kwa madai kuwa huenda mbunge huyo kafanya hivyo baada ya kugundua kuwa Serikali imeshindwa kutatua kero zinazowakabili wananchi hususani wa Nyamongo ambao walifanyiwa tathmini na mgodi kuyahama maeneo ambayo mpaka sasa hawajalipwa fidia.
Ngoto alisema kuwa kama kauli ya Mbunge Nyangwine ilikuwa ni ya uchochezi na kuhatarisha amani, kwani kama kiongozi alipaswa kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa aliongea mbele ya mkutano wa wananchi wa hadhara ambao ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali huku walinzi wa mkutano huo wakiwa ni Polisi.

Ngoto alimtaka mbunge huyo kabla ya kwenda kuuchoma mgodi, yeye kama mbunge awaongoze wananchi wakiwa na mapanga hadi Wizara ya Afya kudai X-Ray kwa madai kuwa kukosekana kwa huduma ya X-Ray Hospitali ya Wilaya ambayo imesababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa huduma,huku wagongwa wengine wakitumia gharama kubwa kwenda kupata huduma ya X-Ray mikoa jirani na nchi ya Kenya.
Tunamtaka mbunge kabla ya kwenda mgodini atuongoze wananchi tukiwa na mapanga yetu hadi Wizara ya Afya kudai X-Ray, miezi 8 sasa hakuna huduma hiyo, mimi kama kiongozi wa Chadema nimefuatilia hospitalini tunaambiwa X-Ray ni mbovu na wahusika wa matengenezo ni wizara ambayo inadaiwa na kampuni inayotengeza X-Ray zilizoko katika hospitali za Serikali, alisema Ngoto.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, Justus kamugisha alisema kuwa kwa upande wao kauli ya Mbunge Nyangine ya kuchoma moto mgodi haiwezi kuwaathiri kwa madai kuwa mbunge akifanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa.