Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya ACACIA kutangaza kupunguza Shughuli zake katika mgodi wa Bulyanhulu

jmchimbadhahabu

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
218
106
Kauli ya Mbunge kufuatia Acacia kupunguza shughuli zake Bulyanhulu

Nimepata taarifa ya Acacia kupunguza shughuli zake BULYANHULU na hivyo kuleta tiahio la madhara ya kiuchumi kwa wafanyakazi zaidi ya 1,200; wakandarasi zaidi ya 800 na wananchi kaka maelfiu Kakola na maeneo jirani. Hali hii haipaswi kuachwa hivi hivi.

My immediate reaction kwa hali hii ni KUIOMBA SERIKALI IRUHUSU WANANCHI AMBAO NI WACHIMBAJI WADOGO KWA MAISHA YAO YOTE, WAANZE KUCHIMBA REEF 2 na maeneo mengine yenye madini ndani ya leseni ya Acacia pembeni ya mgodi ili maisha yaendelee.

Ni vema pia seriklai ikasimamia kuhakikisha haki za wananchi, hasa wafanyakazi na wakandarasi wenye mikataba zinalindwa wakati huu. Serikali isiwaache wafanyakazi wakafanyiwa anachopenda mwekezaji. Ni muhimu SERIKALI ifanye hivyo ili wajue there are consequences for any action they take.

Nawasihi wananchi wangu (hasa wafanyakazi, wakandarasi na wengine ambao wamepata madhara ya moja kwa moja) tuendelee kuwa watulivu tukiamini Mazungumzo yanayoendelea kati ya SERIKALI na Barrick yatapelekea haki zetu zilizoporwa siku zote kurejeshwa na neema endelevu kupatikana.

Mawasiliano rasmi kati ya ofisi yenu (ya Mbunge) na SERIKALI kuhusu maombi mnayopenda SERIKALI iyafanyie kazi kwa jinsi mambo yanavyokwenda yanafanyika.
 
Huyo mwekezaji malipo anayolipa kwa kupunguza watu ni zaidi ya sheria inavyosema, sasa sijui tutambana wapi masikini..
 
Busara imuongoze mwenye ,,,,,,,,,, na sio sheria ndo imuongoze mwenye,,,,,,,,,,

Nb: Jaza sehemu zilizo wazi.

Ref: Fill in the blanks
 
Hivi huyu jamaa anaandika hayo akisahau kama alishawahi kuwa waziri ama!!

Ilo ndio linaloshangaza! Na akili ile ile iliyosababisha ma tatizo ndio inayotengeneza tiba.

Mh rais ombi maalum: itisha account za M-PESA , na ma benki za wote walikuwa mawaziri na manaibu na makatibu wakuu WA wizara hii, wizara ya ardhi na wa wizara ya Viwanda na za vituo vya uwekezaji. Anza na waliowahi kukaa wizara ya madini. Apo kwa facts utajua kuwa si ACACIA kuwa adui WA taifa. Adui mkuu wa taifa ni baadhi ya watawala.

Hili ni ombi maalum kwa rais na TISS ndio mjuijue vyema Acacia.

Mh rais, "miluzi mingi....." Samahani sjakuita mbwa ila nawaza msemo huu!
 
Ukijua kwamba na yeye alikuwa Wazir...na je ukishaziitisha ndio muafaka utapatikana na je kuna kiasi maalumu kila mwenye akaunti hiyo anatakiwa kuwa nacho na kikizidi ndio utamuita mwizi? Mbona kuna watu wana shughuli zao nje ya siasa na njia hiyo ni ndefu sana kufikia lengo kama hata yeye mwenyewe hana huo uthubutu wa kutuambia hadharan anapata nini kwa mwezi.
 
Mh unaiujua miiko ya uongozi? Sisemi waziri flani hapana,ila ifanyike intensive financisl checks za waliowahi kuwa watawala ndio utajua maamuzi na mikstaba ilikuwa biase. Pia ni kweli kuwa kipato hakiwezi kuzidi chanzo. Na watawala wengi hawawezi kujustify million dollars walizonazo. Rais atibu chanzo kuliko kuangaika na matokeo
 
hivi wazungu hawa wametuibiaje kwa muda wote huu bila hata watanzania kujua wakati serikali ipo ?ccm ijiangalie isitufanye watanzania ni wapuuz

Wapo watz walioshiba ndio chanzo. Wanampa rais kazi atibu majipu waliyoyajengea vichuguu
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom