Kauli ya Makonda inapoweza kugeuzwa kuwa FURSA kwa vijana

Stv Mkn

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
328
273
Mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji yanayoongoza kwa uchafu Tanzania.
Siku chache zilizopita Rais Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wapya wa Mikoa, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliteuliwa kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Dar es
Salaam.
Baada ya uteuzi huo na kuapishwa ikulu,
Makonda alifanya mkutano kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambao uliwajumuisha wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam na wadau wengine wa maendeleo.

Agenda ya uchafu ndiyo ilishika nafasi kubwa kwenye mkutano huo. Mh Makonda aliwataka wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza usafi kwenye mitaa yao, pia aliahidi kutoa zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi
milioni 20, na zawadi ya pikipiki kwa wajumbe wake ambao mitaa yao itaonekana ni misafi.

‘Kidole kimoja hakivunji chawa’, ushirikiano pekee na umoja ndiyo unaweza kufanikisha hili kutimia. Vijana wengi wapo mitaani wanalalamika hakuna ajira, lakini kwa hili inaweza ikawa neema na fursa pekee ya ajira
kwao.
Vijana wanaweza kuunda vikundi vyao kwa ajili ya kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuweka unlizi kwa pamoja, siamini kuwa kama kutakuwa na mwenye muda kila siku wa kufanya usafi na kumsimamia mwenzake kwenye hili.
Viongozi wa serikali za mitaa na wananchi wao wanaweza kupanga kuchangishana fedha fulani ili kuwapatia vijana hao ambao watakuwa
wanafanya usafi na ulinzi kwenye mitaa yao.

Hakuna kiongozi anayeweza kukutafutia kazi, ila anakutengenezea misingi ya kuweza kujiajiri mwenyewe kama hili lililotokea sasa.
 
Nakumbuka tulishashindania tenda ya uwakala wa kuzoa taka ndani ya manispaa moja...Watu walionga hadi 20m ili wapate ile tenda..Ila ukiwa kwa nje unaona ni kazi ya kijinga jinga tu kumbe inalipa mno..Kwa wk unazoa mara 2 ili mradi uwe na malori na vijana wa kufanya hivyo kazi..Inalipa ile mbaya..
 
Vp ulifanikiwa kupata hiyo tenda mkuu?
 
Nakumbuka tulishashindania tenda ya uwakala wa kuzoa taka ndani ya manispaa moja...Watu walionga hadi 20m ili wapate ile tenda..Ila ukiwa kwa nje unaona ni kazi ya kijinga jinga tu kumbe inalipa mno..Kwa wk unazoa mara 2 ili mradi uwe na malori na vijana wa kufanya hivyo kazi..Inalipa ile mbaya..
PCCB mpooo pitieni kipande hii?
 
PCCB mpooo pitieni kipande hii?
Nadhani kwa vijana wakiungana katika vikundi na waende kwenye manispaa zao wao watapewa kipaumbele sana kuliko watu binafsi...Hivyo badala ya kuita PCCB ita vijana wajiunge kwenye vikundi wachangamkie hii fursa..
 
Back
Top Bottom