Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,772
Siku Magufuli alipotamka hadharani kwamba Kabudi na Lukuvi hawatagombea Urais kwa sababu ya umri wao mkubwa, wengine walicheka wakiichukulia kama ni kauli ya ghafla. La hasha, hii ilikuwa ni kauli ya kimkakati ambayo Magufuli alikuwa ameitafakari na kupanga kuisema kabla hata ya kuingia Uchaguzi Mkuu.
Ni kauli ambayo iliwashangaza sana Kabudi na Lukuvi, kuwashitua, kuwakatisha tamaa na hatimae kuwaudhi sana. Ilibidi tu wajichekeshe mbele za watu.
Magufuli ameitoa kauli hiyo akiwa amesoma wazi nia za Kabudi na Lukuvi kutaka kuwa Marais wajao. Ukiangalia kwa makini, Kabudi na Lukuvi wamekuwa waaminifu sana kwa Magufuli, wakiwa nyuma yake kwa 100%, wakimpamba kila wanapopata nafasi, na lengo lao ilikuwa kupata kuungwa mkono na Magufuli ili kuwa Rais awamu ifuatayo. Kuna wakati mtu kama Kabudi anajitoa kabisa maarifa na akili (wisdom and intelligence) ili mradi tu ajiweke upande wa Magufuli na Magufuli amuone ndio Waziri anaefaa kuwa Rais ajaye.
Sasa kwa kauli hii Magufuli amefanya kosa kubwa sana. Ametangaza vita na mgogoro ndani ya CCM katika suala la Rais atakaemrithi. Magufuli ameshaanza kumpigia debe "kijana" anaetaka amrithi, kijana ambae Magufuli ataweza kumtawala (kum-influence) kirahisi wakati amemaliza awamu hii. Na watu wanajua ili Magufuli awe na "mrithi" wa kumtawala, lazima awe ni kijana wake mtiifu kabisa kama vile Makonda, au kijana wa kutoka kanda ya ziwa.
Sasa ndani ya CCM kuna watu wameanza kuliona hilo na hawataki kabisa! Kuna watu wanaona Lukuvi au Kabudi ndio Mawaziri "wenye hekima na busara" wanaofaa kumrithi Magufuli.
Magufuli amekuwa na haraka mno kuanzisha vita ya wa Rais ajae, akidhani kuwakatisha tamaa mapema Kabudi na Lukuvi itasaidia kuwaondoa uwanja wa mapambano. Magufuli alipaswa ajifunze toka kwa Kikwete, ambaye alijua kabisa Mwandosya alitaka kuwa kumrithi kiti cha Urais, na Kikwete akajifanya kumuunga mkono Mwandosya hadi dakika za mwisho kabisa ndio akatoa majina yake mfukoni. Mwandosya akawa amepigwa knock out kwa " sucker punch" hakuamini betrayal ya Kikwete! Sidhani hata kama hata wanasalimiana hadi leo. Kikwete mtoto wa mjini, Magufuli mtu wa kuja, ndio tofauti zao.
Sasa athari za Magufuli kuonyesha karata zake mapema ni kwamba ile support aliyopata toka kwa Kabudi na Lukuvi katika awamu ya kwanza hataipata tena! Hilo ndilo kosa kubwa Magufuli amefanya. Sasa Kabudi na Lukuvi hawatampta tena ile 100% waliyompa huko nyuma. Kibaya sana kinachoweza kutokea ni kwamba wataunda makundi yao ndani ya CCM ya kuwa support, lengo likiwa kupanda mbegu ndani ya watu wa CCM kwamba Magufuli ni kiongozi asie na hekima hata kumuunga mkono juu ya chaguo lake la Rais ajae itakuwa ni kosa kubwa!
Kwangu mimi, Hotuba ya Kabudi aliyotoa kwa wafanya kazi wa mambo ya ndani ina kila namna ya viashiria kwamba ameanza mapambano na kujitofautisha ili watu waone anaweza kuwa Rais wa namna gani!
Yajayo ndani ya CCM yatafurahisha sana. Mpambano ndio kwanza unaanza!