Kauli ya Kinana kwa CCM-NEC kusimamia watendaji wakuu wa serikali inathibitisha udahifu wa JK

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Messages
5,405
Points
0

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2008
5,405 0

Swahiba wangu aliyeula CCM-NEC hivi karibuni amenieleza mambo mazito kuhusu hili suala la CCM, kupitia NEC kuisimamia vizuri watendaji wa serikali, kutokana na Kauli ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Kinana.

Swahiba wangu huyo anasema suala la NEC kuwawajibisha watendaji wa serikali wakiwemo mawaziri kwa utendaji wao usioridhisha, pamoja na kuwataka waachie ngazi siyo sahihi kabisa.


Anasema hao watendaji huteuliwa na Rais hivyo ni Rais mwenyewe ndiyo anayeweza kuwawajibisha, pamoja na kuwafukuza. NEC inaingiaje hapa?

Anasema kwa NEC kuwawajibisha watendaji wa serikali linawezekana tu iwapo NEC itawathibitisha kwanza (vetting) wote wale watendaji wakuu wanaoteuliwa na rais.

Anasema haina maana rais anateuwa watendaji lakini wanapoboronga anashindwa kuwawajibisha., kwani huu ni udhaifu mkubwa anaoonyesha JK.
 

Forum statistics

Threads 1,389,540
Members 527,958
Posts 34,027,619
Top