nahavache
JF-Expert Member
- Apr 3, 2009
- 871
- 246
Kinana: Hatuungi rasimu ya katiba kwa 100%. Hii ni kauli ya Kinana kama ilivyoandikwa na magazeti mengi ikiwemo lile la Nipashe. In fact, ameitisha kikao cha CC kujadili rasimu hii na kutoa msimamo.
Kwa kauli kama hii, ina maana kuwa ama anakataa maoni ya wananchi kwa asilimia 100 ambao ndio waliyatoa na yakafanyiwa uchambuzi na kuwekwa kwenye summary ikatoka hii rasimu, au ana maana kuwa wajumbe wa kuandika rasimu hii walitoa yao moyoni wakaandika bila kufuata maoni ya wananchi. Mimi sidhani kuwa wajumbe wa katiba walitoa yao kichwani, hapana bali walifanya uchambuzi wa yale ambayo ni maoni ya wananchi. Hivyo, kauli ya Kinana kuwa kwa asilimia 100 % CCM inaipinga rasimu hii maana yake kubwa ni kuwa CCM haitaki maoni ya wananchi na hivyo inataka mambo yaendeshwe kama anavyojua yeye Kinana na sio maoni ya wananchi. Hii ni dharau kubwa na udikiteta wa hali ya juu.
CCM hasa Kinana anajua kuwa kwa rasimu hii, wananchi wanakuwa washirika wakubwa katika kujiamulia mambo yao ndio maana wana uwezo wa kumpumzisha mbunge ambaye hafanyi yale waliyomtuma bungeni. Hii inajuikana kabisa kuwa, wabunge wa CCM wengi kwa sababu mara nyingi bungeni wameonekana kuwa hawawakilishi wanachi bali wanawakilisha chama. Hii rasimu inaongeza uwajibikaji wa wabunge kwa sababu, mbunge anaweza akafukuzwa chama na akaendelea kuwa mbunge. Ina maana kuwa watu kama Filikunjombe hawataogopa tena kuikosoa serekali wakihofia kufukuzwa chama. Hivyo ni dhahiri kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wabunge wa CCM wakawa mwiba kwa CCM yenyewe kwa manufaa ya wananchi.
Kauli ya Kinana inaonyesha dhahiri kuwa CCM inataka kuendeleza udikiteta na hivyo isipopingwa vikali, inaweza ikaleta machafuko nchini. Kumbuka, wajumbe pale ambao wanaegemea upande wa CCM ni kama 80 % ya wajumbe wote ikiwa ni pamoja na mwenyekiti, mwenyekiti msaidizi na katibu. Na bado ushaihidi uliotolewa na Tundu Lissu bungeni unaonyesha ukaribu wa tume kwa mwenyekiti wa CCM. Bado Kinana anasema haikubali kwa 100%.
Waacheni wananchi waamue! Tumechoka kuamuliwa na watu wachache